Kwanini Wazanzibar wanafanana majina????????

Kwanini Wazanzibar wanafanana majina????????

Mkuu sio Zenji pekee...

Kure kwetu kure kuna akina

- Mwita Chacha Marwa wengi mno....

- Robhi Ryobha Wankuru n.k

Hebu jaribu kuchunguza hata katika kabila lenu pia kuna majina ambayo yanajirudia rudia mengi tu.

Wakati tunasoma kuna watu walilazima kubadili ubini kwa sababu ya kufanana majina matatu kwa watu watatu tofauti.

1. Mwita Chacha Wambura

2. Mwita Chacha Wambura

3. Mwita Chacha Wambura

Hapo unakuta ni watu watatu tofauti!!!
 
Na nyie hamchoki kutujadili.

Hii siyo kuwajadiri kwa mabaya hiki kitu kweli kipo ila mimi natamani nifahamu maana kumekuwa na maelezo mengi ya chini chini kwamba eti ni kwasababu mababu zenu walikuwa wanaoa wake wengi hivyo kupelekea vizazi kutumia majina yanayo fanana fanana lakini sikutaka kuamini kwamba hiyo ndo sababu kuu
 
Vuai, Jecha, Makame, Pandu, Mashavu, Mtumwa, majina haya pia ni yakikoloni?

Hata hili pia lina maelezo yake kwa kuwa nilijua tu watu kama wewe mtani-quote pasipo kufikiria exceptions...

Kwani wewe ukiona Surnames zenye majina kama Massawe, Mushi, Matechi, Urio, Mbowe, Lema akili yako itatoa tafsiri gani?

By the way, jina la mtu huundwa na mjumuiko wa majina mangapi??
 
ni shida kweli mkuu hapa kwa ofisi majina haya yapo kibao na mengi yanafana unajikuta wakati mwingine transaction ya mwingine imeenda kwa mwingine.
 
Yani hapo ina kuwa hivi..... Wewe kama baba wa kipemba, kwa kawaida mpemba kama mpemba huwa hana watoto wachache,mara nyingi huwa na watoto wengi sana hata kumi na saba au zaidi,hao watoto kumi na saba hapo nikutoka kwa wake wawili tu ambao huyu mwanaume ndo anaishi nao pale nyumbani. Hapohapo huyu huyu mwanaume ana wake wengine wawili nje ambao hawajuani na hapo kila mwanamke utakuta ana watoto watano ambao ukichukua na wale kumi na saba utapata jumla ya watoto kama ishirini na saba,watoto wote hao alafu sasa mtoa jina ndo huyo mzee wa kizenj mwenye watoto wote hao, hapo ndo utakuta anarudiarudia majina kwa watoto zake bila kujua na hapo ndo utakuta watoto wanafanana mpaka majina ya babu zao. Cha kufahamu hapo ujue hao ni ndugu ambao hawafahamiani ila anawafahamu pekee ni baba yao. Sasa kama wewe hao ambao ulikutana nao ungewaambia wakuoneshe baba zao ungelikuta wanakuuoneshea baba yao huyohuyo mmoja ila walikuwa hawajuani. Tena Sometime huwa wanaoana ndugu wenyewe kwa wenyewe......................
 
Wadau nimelazimika kuuliza hili swala kwasababu ni zaidi ya mara tatu nakutana na Wazanzibar wasiofahamiana ila wanafanana majina tena majina matatu, nina rafiki yangu wa Mtandaoni yeye yupo Zanzibar tulikutana mitandaoni enzi hizo za Secondary School tukiwa tunasaka marafiki kwenye Mitandao, huwa ananisaidia sana kunipa Kampani, ninapokwenda Kikazi Zanzibar namimi huwa nafanya hivyo hivyo anapokuja Dar.

Nitatumia majina yasiyo harisi kuepuka usumbufu, Huyu rafiki yangu anaitwa Arafa Suleiman Husein, siku moja nikiwa nafanya kiproject flani kilichoni nilazimu kutafuta vibarua watatu kwa ajiri ya kukusanya taarifa, nikajikuta nina kibarua mmoja anaitwa Arafa Suleiman Husein na hata nilipowakutanisha na rafiki yangu ni kwamba hakuna anayemfaham mwenzake, nikiwa huko huko Zanzibar nikakutana na Jamaa aitwaye Hamad Hassan Makame, hili jina lilinikumbusha jamaa mmoja Mzanzibar nimesoma naye Kozi moja mwaka 2007 aitwaye Hamad Hassan Makame, nilipouliza kama anamfaham nayeye akawa anashangaa tu.

Kitu kilichonifanya niandike hii thread, ni kwamba pale Tanga nimekutana na mtu mwingine ambaye anakuwa ni watatu sasa kufanana jina na rafiki yangu yaani anaitwa Arafa Suleiman Husein, na hata hafahamiani na rafiki yangu Arafa Suleiman Husein aishiye Zanzibar,naye huyu pia ni Mzanzibar lakini maisha yake kwasasa anayaendeshea Tanga.

Sasa wadau naombeni kujua ni kwanini hawa ndugu zetu wanafanana sana majina? Nauliza hivyo kwasababu kwa huku Bara ni vigumu sana kuwakuta watu wanafanana majina tena majina yote matatu.

Nikwa sababu huwa kwa kawaida hawatumii majina ya Kibantu bali ya Kiarabu tu.
Majina hayo ya Kiarabu mara nyingi huwa ni ya ndugu zao kama babu, bibi, shangazi na mjomba.
Katika hali hiyo ni lazima majina wakati mwingine hadi la nne yawe yamefanana.

Huku bara nako hali hiyo ipo maeneo ya Pwani kwenye Waislamu wengi
Pia kwa Wagalatia wanaotumia zaidi majina ya Kizungu.

Bazazi!

Bazazi
 
Znz ndogo compare na tz bara, halafu kuna common names za makabila yani za mashamba, kama makame, pandu, vuai, nahoda, nahodha, simba, nk. Pia kuna majina ya kiislam, kama Ally, Muhammad, sawed, Hassan, Ramadan, issa, khadija, fatma, aisha, Maryam, arafa, nk. Ambayo pia ni ya kiarabu. Sasa kutokana na kupeana majina ya urithi, kama babu, bibi, uncles na aunts ndo unakuta yanajirudia.
Mfano mimi mama yangu anaitwa maryam Ahmed, nkinahatika kuolewa na mume anaeitwa Ahmed nkizaa mtt nkamwita Maryam jina litajirudia. Vile vile znz hatutumii majina ya kibantu ambayo yako mengi sana, ndo mana tunarudia apo kwa apo.
 
Znz ndogo compare na tz bara, halafu kuna common names za makabila yani za mashamba, kama makame, pandu, vuai, nahoda, nahodha, simba, nk. Pia kuna majina ya kiislam, kama Ally, Muhammad, sawed, Hassan, Ramadan, issa, khadija, fatma, aisha, Maryam, arafa, nk. Ambayo pia ni ya kiarabu. Sasa kutokana na kupeana majina ya urithi, kama babu, bibi, uncles na aunts ndo unakuta yanajirudia.
Mfano mimi mama yangu anaitwa maryam Ahmed, nkinahatika kuolewa na mume anaeitwa Ahmed nkizaa mtt nkamwita Maryam jina litajirudia. Vile vile znz hatutumii majina ya kibantu ambayo yako mengi sana, ndo mana tunarudia apo kwa apo.

Well said Angel Nylon....hujanipasha urojo ilikuaje juzi pale mlandege
 
Last edited by a moderator:
na vichwa vyao mbona ni bapa yani hawana VICHOGO
 
Back
Top Bottom