Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,157
- 4,457
Wadau nimelazimika kuuliza hili swala kwasababu ni zaidi ya mara tatu nakutana na Wazanzibar wasiofahamiana ila wanafanana majina tena majina matatu, nina rafiki yangu wa Mtandaoni yeye yupo Zanzibar tulikutana mitandaoni enzi hizo za Secondary School tukiwa tunasaka marafiki kwenye Mitandao, huwa ananisaidia sana kunipa Kampani, ninapokwenda Kikazi Zanzibar namimi huwa nafanya hivyo hivyo anapokuja Dar.
Nitatumia majina yasiyo harisi kuepuka usumbufu, Huyu rafiki yangu anaitwa Arafa Suleiman Husein, siku moja nikiwa nafanya kiproject flani kilichoni nilazimu kutafuta vibarua watatu kwa ajiri ya kukusanya taarifa, nikajikuta nina kibarua mmoja anaitwa Arafa Suleiman Husein na hata nilipowakutanisha na rafiki yangu ni kwamba hakuna anayemfaham mwenzake, nikiwa huko huko Zanzibar nikakutana na Jamaa aitwaye Hamad Hassan Makame, hili jina lilinikumbusha jamaa mmoja Mzanzibar nimesoma naye Kozi moja mwaka 2007 aitwaye Hamad Hassan Makame, nilipouliza kama anamfaham nayeye akawa anashangaa tu.
Kitu kilichonifanya niandike hii thread, ni kwamba pale Tanga nimekutana na mtu mwingine ambaye anakuwa ni watatu sasa kufanana jina na rafiki yangu yaani anaitwa Arafa Suleiman Husein, na hata hafahamiani na rafiki yangu Arafa Suleiman Husein aishiye Zanzibar,naye huyu pia ni Mzanzibar lakini maisha yake kwasasa anayaendeshea Tanga.
Sasa wadau naombeni kujua ni kwanini hawa ndugu zetu wanafanana sana majina? Nauliza hivyo kwasababu kwa huku Bara ni vigumu sana kuwakuta watu wanafanana majina tena majina yote matatu.