Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,932
- 985
Niliulizwa swali hilo baada ya kufanya kosa nisilolijua. Niliombwa na kijana ninayemfahamu siku nyingi kwamba tuwe na muda wa mazungumzo juu ya masuala mbalimbali ya maisha yanayomsibu.
Tukiisha kuongea naye mambo kadha wa kadha, ndipo akaniambia "Brother, ninajambo muhimu nahitaji ushauri wako. Umri wangu unakwenda lakini pia unaniruhusu kuwa na familia. Nimekwisha mpata msichana, kiukweli anaonyesha kunipenda. Japo si muda mrefu toka kufahamiana naye, amekuwa akinisaidia hata pale ninapokwama katika mambo fulani fulani na kifedha pia. Kiukweli ananipenda"
Nikamuuliza anafanya shughuli gani,anaishi kwake ama anaishi kwa wazazi wake? Ndipo akaniambia " Yeye ni askari Polisi wa kituo cha ...... , annaishi kwenye nyumba aliyopanga maeneo ya ..... Wazazi wake wapo hapahapa Dar, maeneo ya...."
Nikakosea (japo lengo ni kupata uhakika wa kile nilichokisikia) kumuulizs tena, umesema ni Polisi? "Ndiyo" alinijibu kwa upesi. Nikatulia kimya kwa muda. Nilipotaka kusema akaniwahi kwa kuniuliza " Kwanini watu wanashituka ninapowaambia "nataka kuoa Polisi?" Wewe ni mtu wanne unasita kidogo ninapokwambia jambo hili hasa niliposema nataka kuoa Polisi. Kwani Polisi wanamatatizo gani? Niliwahi kuongea na Mama Sarah (si jina halisi) yeye akaniambia si waaminifu, nikioa nikubali kushirikiana na wengine. Sasa sielewi kuna nini?"
Binafsi niliweza kumweleza kwanini nilikuwa kimya kwa muda na sikupenda kuingia kwa undani juu ya mitazamo ya wengine kwasababu sijui, na sikupenda kumweleza nisichokijua.
Lakini swali hilo aliloniuliza, ndilo haswa limebeba tafakuri yangu nahitaji kujuzwa.