Kwanini watu wanashituka ninapowaambia "nataka kuoa Polisi?"

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Niliulizwa swali hilo baada ya kufanya kosa nisilolijua. Niliombwa na kijana ninayemfahamu siku nyingi kwamba tuwe na muda wa mazungumzo juu ya masuala mbalimbali ya maisha yanayomsibu.
Tukiisha kuongea naye mambo kadha wa kadha, ndipo akaniambia "Brother, ninajambo muhimu nahitaji ushauri wako. Umri wangu unakwenda lakini pia unaniruhusu kuwa na familia. Nimekwisha mpata msichana, kiukweli anaonyesha kunipenda. Japo si muda mrefu toka kufahamiana naye, amekuwa akinisaidia hata pale ninapokwama katika mambo fulani fulani na kifedha pia. Kiukweli ananipenda"

Nikamuuliza anafanya shughuli gani,anaishi kwake ama anaishi kwa wazazi wake? Ndipo akaniambia " Yeye ni askari Polisi wa kituo cha ...... , annaishi kwenye nyumba aliyopanga maeneo ya ..... Wazazi wake wapo hapahapa Dar, maeneo ya...."

Nikakosea (japo lengo ni kupata uhakika wa kile nilichokisikia) kumuulizs tena, umesema ni Polisi? "Ndiyo" alinijibu kwa upesi. Nikatulia kimya kwa muda. Nilipotaka kusema akaniwahi kwa kuniuliza " Kwanini watu wanashituka ninapowaambia "nataka kuoa Polisi?" Wewe ni mtu wanne unasita kidogo ninapokwambia jambo hili hasa niliposema nataka kuoa Polisi. Kwani Polisi wanamatatizo gani? Niliwahi kuongea na Mama Sarah (si jina halisi) yeye akaniambia si waaminifu, nikioa nikubali kushirikiana na wengine. Sasa sielewi kuna nini?"


Binafsi niliweza kumweleza kwanini nilikuwa kimya kwa muda na sikupenda kuingia kwa undani juu ya mitazamo ya wengine kwasababu sijui, na sikupenda kumweleza nisichokijua.

Lakini swali hilo aliloniuliza, ndilo haswa limebeba tafakuri yangu nahitaji kujuzwa.
 
Poooleee saaamaaki poleee wanavyokufaaanyaa. Sio mbaya ukiolea na wenzio pia. Atakwambia anakwenda lindo utajua kinachofanyika? Utalia mikono ikiwa kichwani. Ingawa jiandae kujitoa kwenye ufalme wa mungu kwa kula pesa za rushwa kutoka kwa walala hoi.
 
Nikimkuta polisi yeyote huko peponi natoka nje naenda jehanamu

hii aione Mentor
 
Last edited by a moderator:
kama umempenda nakushauri muoe huyo huyo polic kwani co polic wote wa kike ni malaya wapo wengi 2 wanajiheshimu
 
Kipengele cha lindo na doria umeki consider? Je upo tayari kulala na mto?
 
Nahis hata wao humu wamo! Ngoja waje watoe kauli zao!ila swala la uamanifu ni mwanamke mwenyewe!!cdhani kama ni tabia yao wote!
 
You don't love someone because they're perfect, you love them in spite of the fact that they're not.”. “we accept the love we think we deserve.” ......
 
Kaz sio kigezo cha kipimo cha tabia ya mtu. Ww muoe tu askar hatuna lolote baya ila waTZ wanatuchukulia kivingne. Doria,lindo ni majukumu yakaz kama alivo nes, secretary, na benk. Watanzania wamejazwa upumbaf wakisiasa
 
mbona hata bank offrs wana cv chafu sana na watu wanatangaza ndoa daily? Tabia ni yamtu binafsi ingawaje kunamzingira yanaweza kuchochea ama kumbana mtu. Ila mwisho wa siku kama ni kunguru hata umweke ndani hafugiki.
 
mbona hata bank offrs wana cv chafu sana na watu wanatangaza ndoa daily? Tabia ni yamtu binafsi ingawaje kunamzingira yanaweza kuchochea ama kumbana mtu. Ila mwisho wa siku kama ni kunguru hata umweke ndani hafugiki.

Ha ha ha ila mwanangu bank officers ni noma sema watu hawajui tu.. Wacha tuachie hapa
 
Hongera mimi zamani nilikuwa navutiwa sana na women in uniform especially wale ma trffic wa kike lakini siku hizi naona nimekuwa mkubwa.
 
Enyi kizazi cha maandamano, ikiwa mtautendea hivi mti mbichi (polisi) itakuaje kwa mti mkavu (mwanajeshi)?
 
Back
Top Bottom