Amebadilika nataka niachane naye niishi maisha yangu

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Jul 11, 2017
1,014
1,896
Wakuu kijana wenu nimekwama.

Mwaka Jana mwanzoni nilimpa ujauzito mdada ambaye tulikuwa kwenye mahusiano Ila hayakuwa serious.

So Yule Dada alikuja kupata ujauzito na nikamwambia asitoe nitalea maana nilijiwekea nadhiri ya mwanamke kutotoa ujauzito wangu.

Kiukweli mambo hayakuenda rahisi kama nilivyotarajia Ila nilipambana kadri ya uwezo wangu kuhakikisha namlea mwanamke huyo kwa dhati na nikaanza kuishi nae pamoja.

Nilimfungulia biashara ,na Mimi nikaendelea na kazi ya mkataba.

Kufupisha stori mwanamke alipokaribia kujifungua nikaenda kwao kutoa barua nikapangiwa mahali nikahaidi kutoa na nyumbani wakaendelea kunipa sapoti ya kukubaliana na hali.

Mwanamke amejifungua Ila kiuhalisia ameanza kuwa real tofauti na mwanzo nilivyomuona dharau,kuburi,majibu ya ovyo ,kununa muda wore.

Kiukweli mwanzo nilijua changamoto za kulea Ila naona mambo ni yaleyale sasa mtoto Ana miezi 10.

Kiukweli kama kijana ambaye hata sijafika miaka 30 nimekuwa nikiumia na hizi tabia maana huko nje nafurahia maisha kuliko hata nikiwa na Yeye.

Sioni Future nimewaza nimewazua ..

Nataka nikalipe mahali tu.

Kuhusu KUOA ASAHAU.

Vituko vinavyoendelea naona bora tulee watoto.

Maana Sioni kama nitaenda kuufurahia Moto unaokuja mbele yangu.

Japo namuonea huruma sana mwanangu
 
Mkuu umechanganyikiwa au unatumia akili zote?

Kwanza unasema hukuwa serious nae

Pili ukasema unalea. Ila ukasogeza ukaishi nae

Tatu ukaenda kwao.

Nne ameota pembe mapema kabla ya ndoa.

Tano unataka ukatoe mahari tuu×3

Mkuu sitisha hilo swala la mahari kwanza mpaka upate mwafaka mzuri wa hilo jambo lenu.

Na kama itashindikana bora uchukue 50 zako nae zake we baki kulea mtoto
 
Usilipe mahari, kufanya hivyo itakufunga maana atahitaji taraka baadae.

Mimi nakuomba mtafute Baba mkwe kama yupo faragha, muite sehemu mkae (wote ni wanaume), mueleze yote kuhusu mtoto wake na pia mwambie hatua unayoenda kuchukuwa, msikilize maoni yake, peana muda baadae chukuwa maamuzi kulingana na makubaliano.

Kama Baba mkwe haeleweki wewe piga chini, hiyo mahari itakusaidia baadae ndugu yangu
 
Wakuu kijana wenu nimekwama.

Mwaka Jana mwanzoni nilimpa ujauzito mdada ambaye tulikuwa kwenye mahusiano Ila hayakuwa serious...
Sasa kama huna mpango wa kuoa mahari unalipa ya nini, ukilipa mahari umejiingiza kwenye kifungo, na the earlier the better, kqmq unaona hakuna future kati yenu jinasue mapema usimpotezee muda wala usipoteze muda wako kuendelea kuishi na mtu ambae unaona hamuendani

Ila namuhurumia huyo mtoto atakua pasipo malezi ya wazazi wote wawili
 
Mlishakaa unamwambia kuhusu hizo tabia zako zinakukwaza? Au ndo unaongea nje tu ukifika ndani unakua bwege kila kitu ndiyo
 
Wee bwege nini yaani anakuletea upumbav wote huo bado unataka kwenda kutoa mahali... Umemzalisha inatosha muache abaki singo maza tafuta mwanamke mwingine.

Kijana mdogo hutakiw kuish na mwanamke mpumbavu... Halafu acha upuuzi mtoto mdogo unakimbilia kuoa kwani wew sio rijali..? Kaa jenga maisha yako ukifika miaka 35 ndio ufikirie kuoa... Zalisha tu
 
Wee bwege nini yaani anakuletea upumbav wote huo bado unataka kwenda kutoa mahali... Umemzalisha inatosha muache abaki singo maza tafuta mwanamke mwingine.

Kijana mdogo hutakiw kuish na mwanamke mpumbavu... Halafu acha upuuzi mtoto mdogo unakimbilia kuoa kwani wew sio rijali..? Kaa jenga maisha yako ukifika miaka 35 ndio ufikirie kuoa... Zalisha tu
Umeanza vizuri huko juu umeshauri vizuri sana. Hapa chini hapa ndo umeenda nje kabisaa ya mambo haya
 
Back
Top Bottom