Kwanini watu wanakula Kasa licha ya wengine kufa kwa sumu waliyonayo?

huyu samaki niliwahi kumla kama miaka mitano iliyopita nikiwa kisiwani pemba,ni mtamu sana na akipikwa nyama yake inakuwa kama ya ngombe ila huyu amezidi utamu mara dufu aisee na ukishakula basi hata uambiwe samak hawa wana sumu huwezi kukubali yani kama wana arosto fulani huelew wala husikii ukimpata utamla tu hata kama kwa wasiwasi ni kama yule mwingine wanamwita bunju..siku izi wamegundua njia mpya kabla ya kumla wanampa paka au kuku halafu wanamsikilizia kama atakufa au atapona,basi kama akipona watu wanaweka jibu huyu hana sumu msos unaendelea kuliwa.

yan hata hapa naandika nimesikia wana sumu lakini wallahi itokee amevuliwa sasa hivi basi naenda kununua nimle.Sasa sijui ni ujinga,arosto ama upumbavu gani huu wakat nyama zipo kibao tu.!

Nashauri wataalam wa hawa viumbe watoe elimu na vitengo husika viweke mikazo haswa na adhabu juu kwa watakaowavua wanyama wa hivi wawarudishe tu majini ili tuachane nao kwa lazima.
 
Kasa wapo wa aina nyingi kuna wenye sumu na wasiokuwa na sumu utakae bahatika ndo huyo huyo.
 
Kasa mtam sana akipikwa anakua kama supu ya nyama ya ng'ombe aliyenonaaa sana! Ukija kwangu nikakupa kasa wala hutojua labda utofautishe ladha!

Na siye wavuvi tunajua kasa mwenye sumu ni yup! Pwan tunamla saana! Ukisikia watu wamekufa jua ni bahat mbaya tu! Kama ambavyo unaweza sikia watu wamekufa kutokana na food poison. Karibu pwan
We jamaa bana
 
kwanza kabisa kassa hana sumu ila yupo samaki ana fanana sana na kassa anaitwa ng,amba kama sio mjuzi unaweza ukadhani wote sawa ng,amba ana sumu tena kali tofauti yao nyama ya ng,amba ikiwa mbichi inawasha mikononi ila kasa haina muwasho huku kwetu hao waliopewa ulinzi kuwalinda kasa ndio tuna kula nao
Inashangaza, maana wanaokufa,na watu wa maeneo ya uvuvi/bahari inakujae wasijue kuwatofautisha?..
 
Kasa mtam sana akipikwa anakua kama supu ya nyama ya ng'ombe aliyenonaaa sana! Ukija kwangu nikakupa kasa wala hutojua labda utofautishe ladha!

Na siye wavuvi tunajua kasa mwenye sumu ni yup! Pwan tunamla saana! Ukisikia watu wamekufa jua ni bahat mbaya tu! Kama ambavyo unaweza sikia watu wamekufa kutokana na food poison. Karibu pwan
Unavulia wapi!?
 
Hakuna samak wala mnyama ambaye n halili kuliwa mzur kama kasa alafu utengenezaj wa kasa ni mtwara na visiwa vya mafia kojani nd wanajua hyo nyama achana nayo
 
Kasa mtam sana akipikwa anakua kama supu ya nyama ya ng'ombe aliyenonaaa sana! Ukija kwangu nikakupa kasa wala hutojua labda utofautishe ladha!

Na siye wavuvi tunajua kasa mwenye sumu ni yup! Pwan tunamla saana! Ukisikia watu wamekufa jua ni bahat mbaya tu! Kama ambavyo unaweza sikia watu wamekufa kutokana na food poison. Karibu pwan
Aisee
Sasa tunamjuaje mwenye sumu na yupi asiye na sumu?

Nataka nianze kuwafuga wa nyama
 
Back
Top Bottom