Kwanini watu hujivunia sifa nzuri za kabila lao lakini kwenye sifa mbaya wanajitetea kwamba kila kabila lina hio sifa mbaya

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Sifa ya kabila flani hutumika pale kiwango cha kawaida na kilochozoeleka kikizidi kwenye kabila flani, mfano ni kawaida kukuta katika kila kabila kuna mtu moja kati ya 100 ana sifa fulani lakini kuna kabila fulani wamezidi hiki kiwango, unakuta wapo hata watu nane ama zaidi kati ya 100 wenye sifa flani, hapa kiwango cha kawaida kinakuwa kimevukwa kwa hio wanaanza kusifika na kujulikana kwenye hio sifa, kuzidi kipimo cha kawaida ndio huwabatiza rasmi kwamba kabila flani lina sifa flani il

Sasa unakuta kabila flani linaposifiwa lina sifa flani nzuri, basi wanaweza kulazimisha mpaka ionekane ni sifa ya kila mtu katika kabila na hujisikia faraja.

Ila lina pokuja swala la sifa mbaya, hapa hata kama wanajua kweli hio sifa ipo, watajitetea kwamba hio sifa ipo katika kila kabila ila wanasahau kwamba katika makabila mengine unaweza kumkuta mtu moja kati ya watu mia wenye hio sifa (kiwango cha kawaida), lakini kwenye kabila lao wamevuka hiki kiwango maana unaweza kukuta hata watu sita au zaidi katika watu 100 wenye hip tabia mbovu.
 
Pia ni kupoteza mda kabila flani kujisema wana sifa flani, mara nyingi nzuri nyingine ambazo hata hazipo.

Kujipa sifa hizo ni sawa na kuuelezea mgongo wako ambao huwezi kuuona, ni vema utulie watu wakuelezee mgongo wako upo vipi 😂😂
 
Back
Top Bottom