Kwanini Watendaji na wenyeviti wa mitaa/Kijiji huuza huduma za kiutawala kwa wananchi?

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
2,345
4,168
Wadau mtakubaliana na Mimi haya mazoea yamekuwa Kama uhalali na Sheria kwamba ukiingia kwenye ofisi ya afisa mtendaji au mwenyekiti lazima uandae sh 2000-5000-20000 kwa ajili ya kupata huduma (mara nyingi huwa muhuri tu wa ofisi)

Miaka nenda miaka rudi haya mazoea hutendeka sijui imeidhinishwa au ni utashi wa watu, na mara nyingi inapotokea madogo wakitaka kuomba mkopo ya elimu ya juu kwenye kuidhinisha taarifa za muombaji hukumbwa na kadhia hiyo wengine ni hawa vijana wanaoenda JKT yaani lazima watozwe hela sijui kwanini ( sio wote ila ni wengi)

Mamlaka tunaomba mtutolee ufafanuzi
 
Wadau mtakubaliana na Mimi haya mazoea yamekuwa Kama uhalali na Sheria kwamba ukiingia kwenye ofisi ya afisa mtendaji au mwenyekiti lazima uandae sh 2000-5000-20000 kwa ajili ya kupata huduma (mara nyingi huwa muhuri tu wa ofisi)

Miaka nenda miaka rudi haya mazoea hutendeka sijui imeidhinishwa au ni utashi wa watu, na mara nyingi inapotokea madogo wakitaka kuomba mkopo ya elimu ya juu kwenye kuidhinisha taarifa za muombaji hukumbwa na kadhia hiyo wengine ni hawa vijana wanaoenda JKT yaani lwzima watozwe hela sijui kwanini ( sio wote ila ni wengi)

Mamlaka tunaomba mtutolee ufafanuzi
Mama alishasema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Kimsingi hakuna sheria inayoruhusu kulipishwa kwa ngazi ya mwenyekiti na kwa mtendaji ila huko kwa kamishna sijui utaratibu, lakini hizi ofisi hazina mafungu ya kuziendeshea, kuna mhuri, peni, ink pad na karatasi zote hizi hununuliwa kwa fedha na wakati mwingine hata ofisi yenyewe pia huwa imepangwa, je ushawahi kujiuliza hizo pesa zinatoka wapi?
Ni watu hujitolea kufanya mambo yaende, lakini ni mazoea watu wamejiwekea, mfano÷ kumuwekea mtu dhamana polisi ni bure lakini lazima upitie kwa mwenyekiti akupe barua ya utambulisho then uende polisi, hiyo barua unafikiri mtendaji au mwenyekiti kapewa bure ndio akupe wewe bure? Mbona hamlalamiki pesa za dhamana mnazotoa?
Wengine huambiwa nenda Kaprint au katoe copy barua then unaandikiwa bure, au hao madogo wa sijui loan au jkt mbona wakienda kwa advocate hutoa hela ya mhuri na kinyume na hapo hupati huduma na hamlalamiki? wabongo tunapenda sana ulalamishi sana, support hizo ofisi hata kwa kupeleka rim ili wengine wasiojiweza nao wasaidiwe
 
Unamaanisha kila Mwanasheria ni mtumishi wa umma?

Ninachofahamu kila mtendaji/Mwenyekiti wa kijiji anafuata sheria za utumishi wa umma.
 
Wadau mtakubaliana na Mimi haya mazoea yamekuwa Kama uhalali na Sheria kwamba ukiingia kwenye ofisi ya afisa mtendaji au mwenyekiti lazima uandae sh 2000-5000-20000 kwa ajili ya kupata huduma (mara nyingi huwa muhuri tu wa ofisi)

Miaka nenda miaka rudi haya mazoea hutendeka sijui imeidhinishwa au ni utashi wa watu, na mara nyingi inapotokea madogo wakitaka kuomba mkopo ya elimu ya juu kwenye kuidhinisha taarifa za muombaji hukumbwa na kadhia hiyo wengine ni hawa vijana wanaoenda JKT yaani lwzima watozwe hela sijui kwanini ( sio wote ila ni wengi)

Mamlaka tunaomba mtutolee ufafanuzi
kwani wanalipwa posho!?????
 
Kimsingi hakuna sheria inayoruhusu kulipishwa kwa ngazi ya mwenyekiti na kwa mtendaji ila huko kwa kamishna sijui utaratibu, lakini hizi ofisi hazina mafungu ya kuziendeshea, kuna mhuri, peni, ink pad na karatasi zote hizi hununuliwa kwa fedha na wakati mwingine hata ofisi yenyewe pia huwa imepangwa, je ushawahi kujiuliza hizo pesa zinatoka wapi?
Ni watu hujitolea kufanya mambo yaende, lakini ni mazoea watu wamejiwekea, mfano÷ kumuwekea mtu dhamana polisi ni bure lakini lazima upitie kwa mwenyekiti akupe barua ya utambulisho then uende polisi, hiyo barua unafikiri mtendaji au mwenyekiti kapewa bure ndio akupe wewe bure? Mbona hamlalamiki pesa za dhamana mnazotoa?
Wengine huambiwa nenda Kaprint au katoe copy barua then unaandikiwa bure, au hao madogo wa sijui loan au jkt mbona wakienda kwa advocate hutoa hela ya mhuri na kinyume na hapo hupati huduma na hamlalamiki? wabongo tunapenda sana ulalamishi sana, support hizo ofisi hata kwa kupeleka rim ili wengine wasiojiweza nao wasaidiwe
Sasa hapa mkuu sijajua unataka kuhalalisha nini
 
Umeandika uharo mtupu kwahiyo ofisi za Umma zinaendeshwa na pesa kutoka mifukoni mwa wananchi? Ile ni ofisi ya serikali inagharamiwa na serikali uko kutozwa pesa ni rushwa namimi nilishakataa Huwa siwapi hizo pesa, Huwa nawajibu kama hii ofisi ni Yako binafsi nitakupa ila kama ni ya serikali sitoi na sijawahi nyimwa huduma zaidi ya kuonekana mtata
 
Nikweli,lakini ndugu tunaangalia wapi kwenye uhuru.
Kwa m/koti inaweza ongea nae na swala lako likaisha ila kwa wenzetu kule! Kuna anayekusikiliza kweli ndugu yangu.
Serikali za mitaa,mda mwingine ni Kama kashukra I tu.
Vp kwenye ile micha go ya ambayo Afisa mtendaji anakulazimisha kuilipa Kwanza micha go ile haya Kama wewe ni ndo umehamia pale.
Na huwezi pata huduma Kama hujalipia.hilo nalo ni kelo kubwa Sana kwenye ofisi ambazo watendaji wanalipwa mishahala.
Nipo na wewe kabisa,lakini Kuna sehemu ni kichefuchefu ndugu yangu.
 
Umeandika uharo mtupu kwahiyo ofisi za Umma zinaendeshwa na pesa kutoka mifukoni mwa wananchi? Ile ni ofisi ya serikali inagharamiwa na serikali uko kutozwa pesa ni rushwa namimi nilishakataa Huwa siwapi hizo pesa, Huwa nawajibu kama hii ofisi ni Yako binafsi nitakupa ila kama ni ya serikali sitoi na sijawahi nyimwa huduma zaidi ya kuonekana mtata
Ujue nimemshangaa sana
 
Wadau mtakubaliana na Mimi haya mazoea yamekuwa Kama uhalali na Sheria kwamba ukiingia kwenye ofisi ya afisa mtendaji au mwenyekiti lazima uandae sh 2000-5000-20000 kwa ajili ya kupata huduma (mara nyingi huwa muhuri tu wa ofisi)

Miaka nenda miaka rudi haya mazoea hutendeka sijui imeidhinishwa au ni utashi wa watu, na mara nyingi inapotokea madogo wakitaka kuomba mkopo ya elimu ya juu kwenye kuidhinisha taarifa za muombaji hukumbwa na kadhia hiyo wengine ni hawa vijana wanaoenda JKT yaani lwzima watozwe hela sijui kwanini ( sio wote ila ni wengi)

Mamlaka tunaomba mtutolee ufafanuzi
Kuna mtu alikulazimisha utoe?
 
Usichukulie kitu Kwa udogo, hata hko unakosemea police kuliaza kama hku unakoona ni jambo dogo, kitu kikiwekewa mazoe mwisho wa siku Huwa ni utamaduni end the day haitakiwa ombi tena inakuwa kama Sheria coz ya kitu kuchukulia Kwa udogo.
Yaani jamaa kwa kuwa yeye kuitoa buku bee ni wepesi kwake anaamini kila mtu anaweza kuwaridhisha Watendaji
 
Kimsingi hakuna sheria inayoruhusu kulipishwa kwa ngazi ya mwenyekiti na kwa mtendaji ila huko kwa kamishna sijui utaratibu, lakini hizi ofisi hazina mafungu ya kuziendeshea, kuna mhuri, peni, ink pad na karatasi zote hizi hununuliwa kwa fedha na wakati mwingine hata ofisi yenyewe pia huwa imepangwa, je ushawahi kujiuliza hizo pesa zinatoka wapi?
Ni watu hujitolea kufanya mambo yaende, lakini ni mazoea watu wamejiwekea, mfano÷ kumuwekea mtu dhamana polisi ni bure lakini lazima upitie kwa mwenyekiti akupe barua ya utambulisho then uende polisi, hiyo barua unafikiri mtendaji au mwenyekiti kapewa bure ndio akupe wewe bure? Mbona hamlalamiki pesa za dhamana mnazotoa?
Wengine huambiwa nenda Kaprint au katoe copy barua then unaandikiwa bure, au hao madogo wa sijui loan au jkt mbona wakienda kwa advocate hutoa hela ya mhuri na kinyume na hapo hupati huduma na hamlalamiki? wabongo tunapenda sana ulalamishi sana, support hizo ofisi hata kwa kupeleka rim ili wengine wasiojiweza nao wasaidiwe
Tunalipa kodi
Hao watumishi wanalipwa mshahara
Bado tulipie huduma
Sio sawa
 
Hivi suala la yeye kutolipwa Mimi mwananchi wa kawaida linanihusu nini?

Na umesema suala la shukran, hizi ofisi zimejichukulia hili Jambo ni Kama utaratibu na sio hisani Kama wewe unavyotaka kuelezea
Inashangaza
Sasa mtu afanye kazi na asilipwe siaache kazi afanye shughuli zingine
 
Kwa watendaji ni kosa kisheria kulipisha huduma kwa sababu wanalipwa mishahara na serikali.

Wenyeviti hawalipwi hivyo wengi wanajiongeza, sasa hapo utaamua usiwape usipate huduma au uende takukuru sababu ya buku 5 Kwa mtu asie na mshahara.

Ila kwa wenyeviti kuna baadhi ya malipo ya huduma yapo kisheria kulingana na Halmashauri husika.
 
Ujue nimemshangaa sana
Wakati anaanza kuandika nilihisi atashuka na nondo za maana sana! Mpaka mwisho ndo nikajua kuwa alikuwa hajui aendako! Tangu mwanzo alishapitiliza kwao na akaendelea kupuyanga mpaka nje kabisa ya dunia hii!
Uchawa unaua uwezo wa kufikiri"
 
Back
Top Bottom