Kwanini watanzania wengi wana majungu na fitina?

Kwanini watanzania wengi wana majungu na fitina?

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,333
Kuna jambo linasikitisha hasa ili la watu kuwa na majungu na kusema watu vibaya bila sababu yoyote na kuwasingizia watu vibaya .

Maisha yakienda vibaya utaambiwa umefulia, ukiwa na pesa utaambiwa fisadi au mjenzi huru .

Hata habari nyingi zinazosambaa kwa kasi kwenye sms ni zile za majanga lakini kwa yale mazuri wala hayazungumziwi.

Kuna baadhi ya mikoa tumeshuhudia inadumaa sababu ya majungu na fitina. Ukitembea hata na dada zako ambao watu hawajawafahamu utaitwa kiwembe.

Habari za kusemana uongo na kupakaziana ndio imekuwa kawaida. Ukifanya maendeleo watu wananuna na kukusema vibaya.

Majungu na fitina yanadumaza maendeleo
 
Majungu sio mtaji useme utanunulia nyumba
 
Kuna jambo linasikitisha hasa ili la watu kuwa na majungu na kusema watu vibaya bila sababu yoyote na kuwasingizia watu vibaya .

Maisha yakienda vibaya utaambiwa umefuria,ukiwa na pesa utaambiwa fisadi au mjenzi huru .

Ata habari nyingi zinazosambaa kwa kasi kwenye sms ni zile za majanga lakin kwa yale mazuri wala hayazungumziwi.

Kuna baadh ya mikoa tumeshuhudia inadumaa sababu ya majungu na fitina.
ukitembea ata na dada zako ambao watu hawajawafahamu utaitwa kiwembe.

Habari za kusemana uongo na kupakaziana ndio imekuwa kawaida.Ukifanya maendeleo watu wananuna na kukusema vibaya.

Majungu na fitina yanadumaza maendeleo

Hata Tu Aliyeligundua Hili Nae Asingejua Bila Na Yeye Kuwa Mtu Wa Majungu. Huo Urithi Wetu Na Utadumu Milele Na Milele Na Vizazi.
 
Wapiga majungu hawana tofauti na wauwaji, wao hufanya kila liwezekanalo kulichafua na kuliuwa kabisa jina la mtu kwa kumnena mabaya. Furaha yao ni pale wanapoona majungu yao yamefanikiwa. Ninawachukia sana!
 
mkuu majungu ndio yanaboresha umaskini wa Tz na ndio maana serikali haikemei ili iendelee kuwaongoza wajinga
 
Ni vyema kuwa Watanzania mnajielewa, nashukuru Mungu, mimi ni Mtanganyika. Watanganyika huwa tunampa mtu wazi wazi. kavu live, akimeza ameze akitema ateme. Tukitoka hapo yameisha.
 
Watanzania wengi ni viherehere khabari haijui but anavyoiongea utadhani alikuwa eyewitness ya hiyo kitu. Nakumbuka waqt wa kadhia ya mtoto wa uganda na house girl kuna mtu aliumbuka baada ya kusema yule mtoto kafa watu wakamuhoji akathibitisha baada ya siku mbili ndo ukweli ukajulikana. So kuna kipaji cha fitna majungu na kujua kwingi achilia mbali vijicho na uvivu, Umekaa na wife wako kibarazani anapita jirani kanunua gari wife anakwambia gari la baba au mama flani kiurahisi kabisa unajibu ndio mafisadi wenyewe hao kama si kusema ndio majizi hayo na kisha unafunga mada na hutaki swali.
 
Back
Top Bottom