Kwanini watanzania wengi wana majungu na fitina?

Kwanini watanzania wengi wana majungu na fitina?

Kuna jambo linasikitisha hasa ili la watu kuwa na majungu na kusema watu vibaya bila sababu yoyote na kuwasingizia watu vibaya .

Maisha yakienda vibaya utaambiwa umefulia, ukiwa na pesa utaambiwa fisadi au mjenzi huru .

Hata habari nyingi zinazosambaa kwa kasi kwenye sms ni zile za majanga lakini kwa yale mazuri wala hayazungumziwi.

Kuna baadhi ya mikoa tumeshuhudia inadumaa sababu ya majungu na fitina. Ukitembea hata na dada zako ambao watu hawajawafahamu utaitwa kiwembe.

Habari za kusemana uongo na kupakaziana ndio imekuwa kawaida. Ukifanya maendeleo watu wananuna na kukusema vibaya.

Majungu na fitina yanadumaza maendeleo

Hasa ktk kipindi cha miaka kumi ya JK watu wamemuiga tabia yake.si unajua watoto huiga tabia za wazazi.ukwere ndo source ya fitna na majungu
 
Watanzania ndivyo walivyo na waname ndiyo wanaongoza kwa majungu.....majuu huko ndiyo zaidi. Watanzania waishio huko kazi yao ni kupakaziana tu na kuoneana wivu.
 
Sio watanzania tu, lakini kwasababu swali ni kuhusu Tanzania sababu kubwa ya sisi kupiga majungu ni kukosa upendo,, mtu yoyote aliyekosa upendo atakuwa mtu wa majungu, atakuwa mtu wa Chuki, hata penda maendeleo ya mwenzake, tuwe na upendo, tuwe watu wa haki,
 
Si kweli, hii ni tabia ya binadamu kwa asili si watanzania peke yake hata wazungu wasia na waafrika wote, sina uhakika na waarabu maana sijawahi kuishi nao karibu. Majungu ndio chanzo kikuu cha kujenga urafiki. Fanya utafiti utaona.
 
Tatizo hatuna kazi za kutosha simple so muda wa blah blah upo.
Angalia hata hapa JF blah blah nyingi mtu online toka 6.00 am mpk 00.00
 
Mimi naangalia jamii kwa ujumla
Gossip ni business,people all over the world makes money through gossip,and in fact gossip help to uncover and therefore makes good stories.Bila gossip kwenye corridor za white house tusingejua ile scandal ya Clinton na Monica Lewinsky au Escrow even EPA.
 
We dada unatakiwa umwogope Mungu. Tanzania imekukuta wewe kwa umri gani ulionao?

Mbona umekurupuka, ka Tanzania kanaanzishwa mwaka 1964 nnakaona.

Wengine humu ni nyanya zenu hamjijuwi tu.
 
Kuna jambo linasikitisha hasa ili la watu kuwa na majungu na kusema watu vibaya bila sababu yoyote na kuwasingizia watu vibaya .

Maisha yakienda vibaya utaambiwa umefulia, ukiwa na pesa utaambiwa fisadi au mjenzi huru .

Hata habari nyingi zinazosambaa kwa kasi kwenye sms ni zile za majanga lakini kwa yale mazuri wala hayazungumziwi.

Kuna baadhi ya mikoa tumeshuhudia inadumaa sababu ya majungu na fitina. Ukitembea hata na dada zako ambao watu hawajawafahamu utaitwa kiwembe.

Habari za kusemana uongo na kupakaziana ndio imekuwa kawaida. Ukifanya maendeleo watu wananuna na kukusema vibaya.

Majungu na fitina yanadumaza maendeleo



Hii culture imeshamiri kuanzia 2005 hadi sasa kama mmechunguza vizuri na imesababisha watu kutokuwa na uwezo wa kujenga hoja na kubakia na mtazamo mgando
 
Back
Top Bottom