Kwanini watanzania wengi wana majungu na fitina?

Kwanini watanzania wengi wana majungu na fitina?

Ni vyema kuwa Watanzania mnajielewa, nashukuru Mungu, mimi ni Mtanganyika. Watanganyika huwa tunampa mtu wazi wazi. kavu live, akimeza ameze akitema ateme. Tukitoka hapo yameisha.
mtanganyika gani mnafiki mkubwa.
 
bora vita za bunduki kuliko vita za mdomo
 
Kuna jambo linasikitisha hasa ili la watu kuwa na majungu na kusema watu vibaya bila sababu yoyote na kuwasingizia watu vibaya .

Maisha yakienda vibaya utaambiwa umefulia, ukiwa na pesa utaambiwa fisadi au mjenzi huru .

Hata habari nyingi zinazosambaa kwa kasi kwenye sms ni zile za majanga lakini kwa yale mazuri wala hayazungumziwi.

Kuna baadhi ya mikoa tumeshuhudia inadumaa sababu ya majungu na fitina. Ukitembea hata na dada zako ambao watu hawajawafahamu utaitwa kiwembe.

Habari za kusemana uongo na kupakaziana ndio imekuwa kawaida. Ukifanya maendeleo watu wananuna na kukusema vibaya.

Majungu na fitina yanadumaza maendeleo

kwa kawaida watu wenye majungu na gubu ni wale walio masikini wa fikra hawana cha maana cha kuwaza au kudebate sasa wanakalia tu kusema wenzao ili siku ziende.. binaadam wamezaliwa wanasema ukiwasikiliza hutofika mahali.

Pia ni wivu na roho mbaya tuu..mtu atafurai vipi wewe upate wakati yeye hana? Not everyone can give you a hand or support you on something they have been longing for and it hurts them ... they secreatly admire you hawataki kuaccept tuu.. na hii ni moja ya strategy ya kukufanya wewe ushidwe kufikia malengo yako na kukushushia heshima yako mbele za watu. we kaa angalia watu wajungu ni wale uliowapita katika jambo flani it is very rare mtu alie juu yako kuwa na majungu.
Ni watu wachahe wenye roho nzuri na wanaweza kuona na kufurahia mafanikio yako na in most cases ni Baba na mama yako mzazi na mkeo/ mume kama unaishi nae vizuri..
 
majungu yanasababishwa na uvivu wa kazi, kama ukiwa bize na mambo yako huo muda utaupata saa ngapi.
 
Maisha yangekuwa magumu sana bila umbea na majungu. Russian President Vladimir Putin
 
Umbea na majungu tumefundishwa na ccm.
 
sababu hawana kazi za kufanya na hii yote inachangiwa na ukosefu wa elimu na wivu wa maendeleo.
Lakini pia tukumbuke mfumo uliowakuza karibu % kubwa umechangia sana majungu na fitina zisikuwa na maana yoyote.
Hata mfumo wetu wa siasa umekaa kimajungu majungu tu na panapokuwa na ukweli kusemwa ni dhambi au kuonekana msaliti.
Mara nyingi wafanya majungu na fitina wanaposhindwa mahala uamua kutumia shirki.
 
Majungu ndio kipaji chetu na fitina ni tunu ya Taifa hili na ni moja ya nembo za taifa
 
Mbele za Mungu fitna ni jambo kubwa sana,,,watu wanachukulia mzaha.Mtu anayemfitini mwenzake mbele za mungu ni sawa na kula kipande cha nyama yake,siku ya mwisho utaambiwa umrudishie sijui utamrudishiaje.
Kuna kisa kimoja jamaa alikuwa ndio mkuu wa fitna enzi hizo katika nchi fulani,basi mfalme akamwambia chagua zawadi yeyote nikupe lakini mwenzako nitampa mara mbili yako,,,jamaa akashusha pumzi,Akamwambia mfalme nitoe jicho moja ili yule mwenzake atolewe macho mawili.Hiki ni kisa cha kweli.Athari za fitna hizo.
 
Kuna jambo linasikitisha hasa ili la watu kuwa na majungu na kusema watu vibaya bila sababu yoyote na kuwasingizia watu vibaya .

Maisha yakienda vibaya utaambiwa umefulia, ukiwa na pesa utaambiwa fisadi au mjenzi huru .

Hata habari nyingi zinazosambaa kwa kasi kwenye sms ni zile za majanga lakini kwa yale mazuri wala hayazungumziwi.

Kuna baadhi ya mikoa tumeshuhudia inadumaa sababu ya majungu na fitina. Ukitembea hata na dada zako ambao watu hawajawafahamu utaitwa kiwembe.

Habari za kusemana uongo na kupakaziana ndio imekuwa kawaida. Ukifanya maendeleo watu wananuna na kukusema vibaya.

Majungu na fitina yanadumaza maendeleo

....Kwa sababu ni watanzania na wana majungu na fitna...simple.
 
Majungu ndio kipaji chetu, wakianzisha mashindano ya dunia, mbona tunabeba world cup kila msimu?

The Oscar goes to Tanzanians.Kwa uzushi,umbea na uharibifu wa maisha ya wenzao ndio wenyewe.Uliaikia mtu anaongelewa sana tu ujue huyo yupo juu wanataka kumshusha .
 
Thats poverty culture and thoughts. Inapokuwa kupata kunafikiriwa kwa misingi ya fatalism people resort to all sort of irrational beliefs and thoughts.

Why would you be believe on something which you haven't witnessed, maana hili majungu yafe muambiwa nae lazima awe na uwezo wa kujiridhia kama kinachosemwa kina ukweli. Lakini unapoambiwa kitu na kukichukua kizima bila ya kujua motive za msemaji bila ya kupata facts, na wewe kukiongelea kwa mwengine outright without a balanced story ya mtu aliewekewa majungu you are as much of the problem kama msemaji.

Kwa level yetu ina maana kama jamii si watu wa kujiuliza sana hapo ndipo tulipo na majungu hayawezi isha mpaka jamii iwe ya watu wa kujiuliza kwanza au walau kutafuta ushahidi wa wanachoambiwa. In other words kuna watu wachache wenye uelewa Tanzaniakuliko wasio nao (unfortunately wasio nao ndio wenye influence kwenye jamii).

Moja ya sifa kubwa ya jamii za namna hii dunia ya leo ni kuwa high religious societies kwa sababu zilezile za kutouliza na kujiridhia kuhusu maswala ya mungu.
 
Back
Top Bottom