upupu
JF-Expert Member
- Apr 15, 2008
- 614
- 198
Jamani naomba mnisaidie, hivi hii ni hulka au tatizo au kukata tamaa? Imekuwa tabia ya watanzania wengi kupenda kumuachia Mwenyezi Mungu hata katika mambo ambayo yalikuwa ndani ya uwezo wao, nao ndo walitakiwa kuchukulia hatua;
Mfano:
1. Mtu anatapeliwa pesa, utasikia anasema namuachia Mungu, atanilipia (badala ya kukomaa na aliyemtapeli amrudishie, au nayeye amtapeli kitu kingine).
2. Mtu anaibiwa kitu, utasikia namuachia Mungu, ndiye atakayenilipia, (hachukui hatua yeyote)
3. Mtu anakuvunjia heshima, (hapa napo anamuachia Mungu, yaani hata kumlamba vibao viwili vitatu unashindwa hayo ni machache sana, ila kuna mengi ya namna hiyo, nadhani hata wewe ni mmoja ya wanaomuachia mwenyezi Mungu,
Tuache kumuachia Mungu mambo ambayo tunaweza kuyashughulikia wenyewe!! Tumuachie vile ambavyo vipo nje ya uwezo wetu, mfano mafuriko, kimbunga, ukame na mengine.