Mfumo wa Ajira kwa watumushi wa Serikali ubadilishwe ili kuleta matumaini kwa Watanzania waliopo shuleni

Baba Ghati

New Member
May 16, 2024
1
0
Kwanza kabisa muasisi wa taifa letu hayati Mwalimu JK Nyerere alisema kila mtanzania anapaswa kupambana na adui watatu ambao ni:

1. Ujinga

2. Umasikini

3. Maradhi

Tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua tulipo fikia maana tumeweza kufaulu lakini sasa badala ya kupunguza maadui hapo basi serikali imejikuta kuongeza adui mwingine ambaye atazaa adui mwingine tena.

Zamani msomi alikuwa na heshima katika hii Nchi kitu ambacho kiliwanfanya watanzania wengi kusoma kwa bidii ili kujenga heshima waliokuwa nayo wasomi, lakini kwa sasa mambo yamegeuka wasomi ambao zamani ilikuwa fahari ya kila mtu kujivunia leo wamegeuka kero ambayo unachukiwa mtaani sasa hivi ukitaja msomi wa shahada ya kwanza na mama ntiliye mtaani mama lishe anaonekana kuwa wa maana sana kuliko msomi wa shahada kutoka chuo kikuu cha Dar-es-salaam je ni kweli kuwa Elimu yetu imeshuka kiwango kiasi hicho jibu ni hapana ila muondo wa ajira uliopo serikalini ndio umefanya Elimu kushuka daraja na kuonekana kitu cha kawaida sana.

Kwa makusudi kabisa serikali umeamua kufanya ajira kuwa mchezo wa bahati na maarufu kama (KUBETI) Kila msomi hana uhakika wa ajira hivi je ni kweli kuwa kuajiriwa ni Kubeti? Jibu ni hapana kwa mfano tukichukulia kada ya Elimu na Afya ambao ndo tuko nao kwa Wingi mtaani Kabla ya kuingia kwa Awamu ya tano madarakani Tanzania ulikuwa hakuna changomoto ya ajira sasa ni nini kilitokea?

Sera ya Rais wa awamu ya tano alisema kuna watumushi wengi fake na hewa jibu ndio ni kweli wakaondolewa na wenye vyeti fake wakatoka lakini nini kiliendelea kama wengi walitoka je nafasi zao zilibwa na nani?

Tunaposema sema kuwa ajira hakuna je ni kweli wote wanasubiri mfumo au Kuna wengine wanaajiriwa nje ya mfumo?

Swali la kwanza kama kweli ajira ni haki ya kila mtanzania aliyehitimu na kuwa na sifa za kuajiriwa inakuwa aliyemaliza chuo 2022 kupata kazi huku Mwalimu au daktari mwenye sifa sawa na huyu wa 2022 anakosa kazi aliyemaliza 2015 au kumi na nane je unaweza vipi kumuaminisha mtanzania wa kawaida akaelewa kuwa wa mwisho kuhitimu amepata alafu mtangulizi amekosa au ndo tunasema bahati haikuwa yako hivi je ni kweli tunaajiliwa kwa bahati au ajira ni haki ya mtanzania kupata?

Mwalimu wa masomo ya Sanaa aliyemaliza 2022 alipata kazi huku Mwalimu wa masomo hayo hayo ya Sanaa aliyehitimu 2018 bado akiichwa mtaani je hapa kuna haki au Kuna jambo nyuma ya Pazia ambalo wengine hawajui au ni vigezo vipi vingine vinatumika kumpa 2023 kazi kumuacha 2018 kama basi ji (GPA) mbona kwenye tangazo huwa hatusikii kuwa wanao paswa kuomba kazi wawe ni kiwango fulani cha ufaulu ili kama mtu hana hicho kiwango asihangaike kutuma maombi kuomba wakati akijua hana vigezo.

Ushauri
Nchini Kenya kwa kuwa wao walitutangulia katika Elimu basi Mwalimu akihitimu chuo cha ualimu hukaa nyumbani miaka minne mpaka mitano lakini anajua **** baada ya hapo ajira ni uhakika sasa je yupi afadhali anayekaa miaka minne lakini akijua kuwa miaka hiyo ikiisha atapata ajira au anayekaa miaka zaidi ya nane kila mwaka anatuma na haupati na hajui aptapa lini? Zaidi ya kuwaza na kuwa msongo wa mawazo?

Siku hizi ukimwambia mtu kuwa Kati ya Elimu na hela kipi bora anajibu bila hata kufikilia hela ni bora maana wasomi siku hizi hawana tofauti na wasio Soma tofauti ni kutembea kwenye jua kali na bahasha yenye vyeti ilichokaa na kuchomekea wakitoka sehemu moja kwenda nyingine na ugumu wa maisha utanikuta hata Mwalimu anaomba kazi ya polisi wakati hana taaluma hiyo je kama tunafanya watu waichukie Elimu wapi tunakwenda?

Kila mtu akiachaa kusoma akatufuta nini mstakabali wa taifa letu kwa miaka hamsini ijayo tutakuwa na watu wanaojua kutafuta hela lakini hawana Elimu je hicho ndo tunakuhitaji?

Kama ni kweli wasomi ni wengi kuliko nafasi za kazi zilizopo basi serikali itenge ajira kwa awamu kwa mfano wanasema mwaka huu wanaopaswa kutuma maombi ya kazi ni kuanzia 2015 hadi 2018 hawa wakisha basi awamu ijayo tuanzie 2019 hadi 2021 ili kila mwenye vigezo vya kupata ajira apate kwa awamu yake ila kumuajili mhitimu wa 2022 na kumuacha wa 2015 ni kumkosea heshima na kunyima haki yake ya msingi na kufanya naamini kuwa bila connection mtu hawezi kupata kazi je vipi kuhusu hawa wananchi ambao hawana baba wala mama mbunge au mjomba nani atawasiadia alafu utasikia serikali inasema wenye vigezo ndio waliopata kazi sasa je kwa nini uliruhusu ambao hawana vigezo kutuma maombi au je kwa nini mliruhusu vyuo kuwatunukia shahada astashada na vyeti kama hawana vigezo vya kupata kazi?

Tunaelekea wananchi watakosa Imani na serikali na watu watachukia shule na kusoma kwa ujumla kwa sababu inaonekana hakuna maana ya kusoma kwa kuwa huko vijijini watu wanajua unasoma ili upate kazi sasa kama kazi hakuna unasoma ili ufanye je si ni bora mda unaoutumia kwenda shule uanze kufunga kuku au ng'ombe huenda ukatoka kimaisha kuliko kupoteza mda kwenda shule?

Baada ya miaka 30 ijayo naiona Tanzania yenye wasomi wachache sana na watu wasiopenda kusoma kabisa je tutaweza kukabilina na ulimwengu wa Teknolojia inayokuwa kwa kasi au ndo nafasi zetu nyeti tutawapa watu wa mataifa mengine kuzikaimu maana wanatanzania wahati tena kusoma maana wanaona hamna umuhimu wa kusoma lakini hivi ni kweli miaka saba shule ya Msingi minne sekondari na miwili Advance jumlisha mitatu minne au mitano haina maana kweli msoto wa chuo pamoja na suplimentary zote pamoja na msuli wa Advance bado tunawekwa sawa na mtu ambaye hata shule ya Msingi hakumaliza kisa tu ajira?

Serikali tafakari chukua hatua hili ni wazo kutoka kwa mwananchi mzalendo ambaye amepata fursa hii adimu ya kuwasilisha mawazo yake.

Mwsho kabisa niombe serikali inapotoa tangazo basi iweke vigezo vyote vinavyotakiwa ili wenye kutuma wawe ni wale wenye sifa zilizotaja maana naona kuwa sifa ya kuhitimu na kuwa na cheti haitumiki kabisa ni bora tukawa wazi tukawambia watanzania ukweli kuliko kila mwaka mtu anatuma maombi anakataliwa anachukuliwa wa nyuma yake yeye anabaki inakatisha tamaa sio vijana tu hata wazazi ambao wengi ni masikini walisomesha watoto wao kwa kijinyima lakini mtoto amehimtimu ana miaka nane nyumbani bado hana kazi utamshauri vipi mwingine kusoma wakati wewe huna tofauti na asiyesoma wote mnasota mtaani?
 
Back
Top Bottom