Kwanini wapinzani Tanzania wanatamani kufanya siasa kwenye mazingira laini bila kuyalainisha!?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,003
2,000
Mapambano ya kisiasa hayajawahi kuwa rahisi mahali popote duniani na hii ni kutokana na ukweli kwamba inakupa madaraka makubwa sana kwa njia nyepesi tu yaani kushawishi watu wakuunge mkono.

Ni kutokana na ukweli huo ndio maana ni kazi ngumu sana kumtoa madarakani anayetawala hivi sasa, kuliko ilivyokua wakati wa kumtoa mkoloni.

Cha ajabu ni kwamba wapinzani waliopo sasa hivi wanataka eti chama tawala kiwahurumie kiwarahisishie kufanya siasa, tuwe wakweli msipokuja na hatua serious kuliko hizi za kushinda mnalialia hakika wajukuu zetu na wajukuu wao watatawaliwa na CCM.
 
The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,003
2,000
Upo sawa mkuu haya pendekeza nini kifanyike maana na wewe umishia kuandika andika tu! Hebu taja wachukuwe hatua zipi na zipi?? na utolee mifano yake!
Lazima waanzishe varangati za ukweli hata ikiwalazimu kufungwa jela wafungwe tu, ili dunia na jumuiya ya kimataifa iwasaidie kupiga kelele.

Angalizo langu ni kwamba wajenge hoja zinazoeleweka kirahisi na mwananchi wa kawaida na sio huu msamiati wa katiba mpya ambao umma wa wananchi wa kawaida walio wengi hawaulewi.

Njoo na hoja kama vile kupinga kodi za hovyohovyo kushinikiza bei za mafuta zishuke kupinga upandaji wa gharama za maisha kushinikiza upatikanaji wa mbolea na pembejeo za kilimo kwa gharama nafuu nk nk.
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
14,216
2,000
The Phylosopher

Viongozi wa upinzani wameonesha mfano na wengine walifungwa jela, wamebambikizwa kesi, leseni za uwakili kufutwa, wametekwa, wameumizwa, wako uhamishoni nje, n.k Unaita ni mazingira laini

Wewe ambaye siyo kiongozi lakini unapenda mabadiliko kupitia upinzani umefanya nini? Umetoa mchango gani kupitia majadiliano, ushawishi, kususia, kukemea, kuhamasisha, kutoa elimu ya uraia, maandamano, kupigia kura nyingi upinzani n.k
 
The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,003
2,000
Taja hizo hatua serious
Kwa hiyo unataka mimi mianze kuwafundisha wanasiasa cha kufanya!? Mbona walipokuwa imara walikuja na harakati mbalimbali na tuliwaelewa kirahisi tu!! Wapambane waje na mbinu zitakazowatambulisha kama watetezi wa wananchi!!
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,793
2,000
Kwa hiyo unataka mimi mianze kuwafundisha wanasiasa cha kufanya!? Mbona walipokuwa imara walikuja na harakati mbalimbali na tuliwaelewa kirahisi tu!! Wapambane waje na mbinu zitakazowatambulisha kama watetezi wa wananchi!!
Tutajie hizo mbinu
 
The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,003
2,000
The Phylosopher
Viongozi wa upinzani wameonesha mfano na wengine walifungwa jela, wamebambikizwa kesi, wametekwa, wameumizwa, wako uhamishoni nje, n.k unaita ni mazingira laini

Wewe ambaye siyo kiongozi lakini unapenda mabadiliko umefanya nini?
Mimi napenda mabadiliko ni kweli ila mimi si kiongozi wa chama chochote cha siasa ila Hawa wapinzani wakija na hoja rahisi inayoeleweka kwa umma ni rahisi kuwaunga mkono!!
Ww unaposema walifungwa jela unaweza kuuliza hata mwananchi mmoja juu ya kufungwa kwa kiongozi yeyote kama anajua hata sababu ya kufungwa kwake!!?
 
Mwadilifu Mdhulumiwa

JF-Expert Member
Jul 22, 2021
271
500
Kwa hiyo unataka mimi mianze kuwafundisha wanasiasa cha kufanya!? Mbona walipokuwa imara walikuja na harakati mbalimbali na tuliwaelewa kirahisi tu!! Wapambane waje na mbinu zitakazowatambulisha kama watetezi wa wananchi!!
Mkuu katika andiko lako tayari umeshaonyesha unawafundisha wanasiasa nini cha kufanya ndomana watu wanakubana ukamilishe mada kwa kueleza hatua/mbinu unazoamini wewe kuwa zitawavusha wapinzani!

Kwa hiyo usiishie kukosoa, leta wazo jipya!
 
Leonardo Harold

JF-Expert Member
May 13, 2019
316
500
Mapambano ya kisiasa hayajawahi kuwa rahisi mahali popote duniani na hii ni kutokana na ukweli kwamba inakupa madaraka makubwa sana kwa njia nyepesi tu yaani kushawishi watu wakuunge mkono.
Upinzani wamefanya kila waliloweza, shida ya nchi hii ni wananchi wenyewe...hata wateswe vipi wao wanabaki waoga hawana cha kufanya, ccm inanufaika na ugoigoi wa wananchi.
 
kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,334
2,000
Mapambano ya kisiasa hayajawahi kuwa rahisi mahali popote duniani na hii ni kutokana na ukweli kwamba inakupa madaraka makubwa sana kwa njia nyepesi tu yaani kushawishi watu wakuunge mkono.

Ni kutokana na ukweli huo ndio maana ni kazi ngumu sana kumtoa madarakani anayetawala hivi sasa, kuliko ilivyokua wakati wa kumtoa mkoloni.

Cha ajabu ni kwamba wapinzani waliopo sasa hivi wanataka eti chama tawala kiwahurumie kiwarahisishie kufanya siasa, tuwe wakweli msipokuja na hatua serious kuliko hizi za kushinda mnalialia hakika wajukuu zetu na wajukuu wao watatawaliwa na CCM.

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
14,216
2,000
Mimi napenda mabadiliko ni kweli ila mimi si kiongozi wa chama chochote cha siasa ila Hawa wapinzani wakija na hoja rahisi inayoeleweka kwa umma ni rahisi kuwaunga mkono!!

Tayari unatoa visingizio, hujawaona viongozi wa upinzani wakipitia mapambano makubwa na kupata madhila lukuki huko Mwanza, Mbeya, Hai, Zanzibar, Kilwa n.k

Wewe mwananchi mpenda mabadiliko umefanya nini kuunga mkono viongozi hawa waliojitolea mhanga kwa jasho, damu na Mali zao kuongoza mapambano ?

Mfano mdogo wapi wananchi mmepaza sauti kudai katiba mpya kwa maandamano yasiyo na kikomo yatakayo wahakikishia huduma za maji safi bila mgao, nishati ya umeme usiokatika kwa matumizi ya shughuli za kiuchumi na kijamii pia huduma bora za afya ?
 
Yaani ukija na madai ya katiba mpya kwa siasa ya tanzania hautoboi ukweli ni kwamba wapinzani walitambulishwa na msimamo wao wa kupinga ufisadi na maonezi dhidi ya wananchi kama ukikumbuka vizuri hata zito alipata kufukuzwa bungeni kwa kwa kusimamia hoja za aina hii na ilikuwa rahisi sana kueleweka lkn kwa hoja za hapo juzi Kati mwenyekiti analazimisha wabunge watoke nje kwa kisa cha corona!? Ambayo hakuna mtu alikuwa ana ufumbuzi wake!!

.
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
7,244
2,000
Mapambano ya kisiasa hayajawahi kuwa rahisi mahali popote duniani na hii ni kutokana na ukweli kwamba inakupa madaraka makubwa sana kwa njia nyepesi tu yaani kushawishi watu wakuunge mkono.

Ni kutokana na ukweli huo ndio maana ni kazi ngumu sana kumtoa madarakani anayetawala hivi sasa, kuliko ilivyokua wakati wa kumtoa mkoloni.

Cha ajabu ni kwamba wapinzani waliopo sasa hivi wanataka eti chama tawala kiwahurumie kiwarahisishie kufanya siasa, tuwe wakweli msipokuja na hatua serious kuliko hizi za kushinda mnalialia hakika wajukuu zetu na wajukuu wao watatawaliwa na CCM.
Haaa! uchaguzi wa wabeba mabegi yaliyojaa ndiyo kwanza nimeushuduia 2021
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom