Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 67,110
- 173,850
Wazee wa battle ndio wengi humu! Mahusiano yamefanywa kama sehemu ya kuoneshana nani zaidi!Hii dhana ya feminism binafsi huwa naona haijaeleweka kwa watu wengi.
Unamkuta mtu wanaume sijui walinfanya nini, hana mahusiano nao mazuri basi anatumia kichaka cha feminism kujenga uadui kati ya mwanaume na mwanamke.
Sasa wasichana wakiwasikikiza hawa ni ngumu sana kuishi kwenye ndoa.
Kwasababu badala ya ndoa kuwa sehemu ya kushirikiana, inakuwa sehemu ya kuoneshana nani zaidi, au nani mwamba.
Kikubwa ambacho mwanamke alitakiwa kufanya ni ku neutralize misuguano ila wao wanaona kufanya hivyo kama ni kutufanyia favour😁😁😁 tabu itaendelea tu!