Kwanini wanawake waliotendwa wanapenda kusali?

Kwanini wanawake waliotendwa wanapenda kusali?

Wengine tumekua tukisali tangu nimepata akili ya kuelewa mambo tena kuanzia primary huko. Hiyo research haipo general ila ni heri wamtafute Mungu kuliko kuendelea kubahatisha na kuendelea kuumizwa
 
Nadhani ndio sababu wanaume wwnye kutenda wanawake hujikuta hawajielewi. Wanahangaika kila panty inamuita anajikuta tu anaenda. Ni sala zinajibu. Hata wakijitahidi kuoa hawapati raha.
Ukiona mtu wako hatulii ujue kuna sala zinamtembelea. Bila kujinyenyekesha na kuomba msamaha wa dhati laana itaendelea tu na vizazi vyake vinavyokuja.

Ni hivyohivyo kwa wasichana
 
aiseee yani umenifurahisha na umenigusa sana rafiki kweli kimbilio letu ni Mungu pekee kwake kuna pumziko na upendo wapatikana kwake

hahahaaaaaa..... hivi kweli ee? mie kabla ya kupigwa kibuti nilikuwa naenda kanisani kama muumini wa kawaida tu kila jumapili. Kwaya nilikuwa napenda na nilikuwa nikiimba kwa kuwafatilizia nikiwa kwenye viti vya waumini ila nilikuwa naogopa kujiunga kwa kujiona mdhambi na busy. Baada ya kupigwa kibuti nikawa na stress za kuua mtu kama miaka mitatu hivi. kanisani nikakata mguu, kutembelea ndugu na marafiki nikasitisha, kazi nikawa nafanya basi tu kwa kujisukuma ili nipate mshahara . Nikawa napenda mitoko mitoko kule calabash na kwingineko na mvinyo kidogo na nakadhalika. Katika hicho kipindi cha miaka mitatu ya msongo nilikuwa nahangaika kujinasua hivyo nilikuwa nasoma machapisho mbalimbali na kujifariji kwa nyimbo za dini na za secular. Taratibu nikaanza kubadilika nikaanza kurudi kwenye maisha ya kabla ya kibuti na nikawa na ari ya kufanya yale yote niliyokuwa napenda kufanya au niliyokuwa najiona siwezi kufanya. Nikarudi kanisani, (kule kule nilikobatizwa sijawahi kuhama) safari hii kwa kishindo zaidi maana nilienda mpaka kuimba kwaya (Kwaya nilikuwa nikiimba toka sunday school mpaka ukwata o na a levels ila nilivyofika chuo kikuu nikaona ni kupoteza mda. Mwe!) Basi nilivyorudi huko kanisani wakadai wanaona roho ya uongozi ndani yangu wakanipachika vyeo humo basi kwa kuwa nilishakataa ile sauti inayoniambia siwezi, sina muda... mi nikakubali majukumu na naendelea nayo.

Nafurahia maisha, siogopi tena kuachwa wala changamoto yoyote hainitishi maana huku kanisani tunakutana na kina mtume paulo wakituambia majaribu hayana budi kuja...Mungu hataruhusu jaribu kubwa kutushinda.....majaribu yanajenga perseverence na perseverence inajenga character n.k. Haya maneno nilikuwa nayajua tangu utoto wangu ila niliyaelewa baadae sana. lol. Kuna wakati tunaamini Mungu anatuacha tupigike, tuhangaike wenyewe, tushindwe ndo tumkumbuke. Kusamehe si kazi ndogo atii ila ukifanya kwa nguvu ya imani inawezekana. Kila mtu ana jinsi yake ya ku-handle stress. Wanawake wenye masahibu wapo kila mahali: baa, saluni, nyumba za wenyeji, kanisani na barabarani. Na si walioachwa tu bali hata walioolewa na waume pasua vichwa. Wamama wanapanda mpaka ndege jamani kwenda kwa nabii nanii kuombea hubbies na kuchukua mafuta wanapaka kwenye boxer za kina baba lakini wapi! Wengine wameona Mungu wa kanisani anaweka usiku wameamua kuhanja kwa waganga. Acheni tu jameni! Wengine wanakuwa kwenye mpito, wengine wanapotelea humo moja kwa moja. Hivi wanaume wakikumbwa na vibuti au ndoa ngumu wanaendaga wapi? huwa naona kama wakifilisika ndo wanapuyanga kwenye makanisa maana hata hela ya bia wanakuwa hawana.
 
huwa wanatafuta faraja tu,kwani kama wangekua wanampenda mungu toka mwanzo wasingefanya maamuzi ya kuwa na mtu bila kumuweka mungu mbele kwanza,alafu wengi wao wanaotendwa ni wale wenye kujiona sana na kudharau watu,sasa huwa wanajidai wamempenda mtu kwa fedha au umaarufu kumbe yule mtu anakua hayupo nae anapiga tu,kwa kuwa amejileta mwenyewe kwa kutaka ubabu kubwa.
 
Hii nimeiona sana, mabinti au wanawake wengi waliotendwa na wanaume wanapenda sana kusali, na wanasema Mungu yupo, atanisaidia tu hata nisipopata Mume nitaendelea kumwabudu Mungu wangu, wengine husema.

Sasa nimemgeukia Mungu wangu na yeye ndiye jibu la moyo wangu.

Wengine inawabidi waimbe mapambio/kwaya tena kwa sauti kubwa kuliko zile za kawaida zinazoruhusiwa, wengine huwahi ibadani mapema na kukaa viti vya mbele au kati kati.

So what? No value added here.
 
Waangalie rafiki zako au jirani zako 10 tu utakuta 7 au zaidi walishatendwa na hukimbilia kwenda kusali makanisa ya kilokole.

Kwanza sina marafiki ambao wana imani dhaifu zaidi yangu, pili personality ya mtu pia play a role
 
amesema wanawake wengi sio wote hivi kuna watu mna comment mkishasoma heading tu.
No one asked for your opinion. Pili hiyo research yake kama haiko documented facts haina nguvu.
 
Hii nimeiona sana, mabinti au wanawake wengi waliotendwa na wanaume wanapenda sana kusali, na wanasema Mungu yupo, atanisaidia tu hata nisipopata Mume nitaendelea kumwabudu Mungu wangu, wengine husema.

Sasa nimemgeukia Mungu wangu na yeye ndiye jibu la moyo wangu.

Wengine inawabidi waimbe mapambio/kwaya tena kwa sauti kubwa kuliko zile za kawaida zinazoruhusiwa, wengine huwahi ibadani mapema na kukaa viti vya mbele au kati kati.

Mimi tatizo langu na hawa wazushi wapo fasta ku declare wapo close na Mungu lakini hawaishi maisha matakatifu na kama wanafanya hivyo wanapenda kutangaza kwa kila mtu as if wamelazimishwa, inshort sidhani kama wapo seriously committed na Mungu.
 
Back
Top Bottom