Kwanini wanawake waliotendwa wanapenda kusali?

Hii nimeiona sana, mabinti au wanawake wengi waliotendwa na wanaume wanapenda sana kusali, na wanasema Mungu yupo, atanisaidia tu hata nisipopata Mume nitaendelea kumwabudu Mungu wangu, wengine husema.

Sasa nimemgeukia Mungu wangu na yeye ndiye jibu la moyo wangu.

Wengine inawabidi waimbe mapambio/kwaya tena kwa sauti kubwa kuliko zile za kawaida zinazoruhusiwa, wengine huwahi ibadani mapema na kukaa viti vya mbele au kati kati.

We ulitaka wafanyeje mkuu?
 
ndo kawaida ya binadamu tulio wengi, yakishatukuta ndo tunamkumbuka Mungu
 
Mbona mimi sijatendwa bali namwamini mungu......research yako invalid.....

Waangalie rafiki zako au jirani zako 10 tu utakuta 7 au zaidi walishatendwa na hukimbilia kwenda kusali makanisa ya kilokole.
 
COZ Waliokutana nao mwanzo ni mapepo hawataki kukutana nao tena...ndio wanaona bora wasali ili waepushwe nao

ivi unaimba sauti ya ngap vile?mungu atakusaidia hautokutana na mapepo......
 
Kwani wangekuwa walevi au malaya baada ya kutendwa ungeuliza hapa? Ujinga tu kukaa unafuatilia maisha ya watu makanisani fanya yako tafiti za hivyo hazitusaidii ktk jamii. Kwa hiyo wafanyaje?
 
Ha ha ahaaa!!!!
Ugomvi mwingine huu!!

Vipi kuhusu status zao mitandaoni
1. Bwana ndio tegemeo langu. . . .
2. Hakuna mwanaume kama Yesu!!
3. Hakika sasa nimepata tegemeo la kweli. . . .
 
Mwanamke anapokuwa na mwanaume huweka akili yake yote hapo. Na mwanaume huwa yuko nusu nusu hawataki kuwa na mwanamke mia kwa mia. Humwacha saa yoyote akiamua na adui mkubwa wa mwanamke ni upweke. Kanisan anaenda kupunguza upweke na stress
 
hahahaaaaaa..... hivi kweli ee? mie kabla ya kupigwa kibuti nilikuwa naenda kanisani kama muumini wa kawaida tu kila jumapili. Kwaya nilikuwa napenda na nilikuwa nikiimba kwa kuwafatilizia nikiwa kwenye viti vya waumini ila nilikuwa naogopa kujiunga kwa kujiona mdhambi na busy. Baada ya kupigwa kibuti nikawa na stress za kuua mtu kama miaka mitatu hivi. kanisani nikakata mguu, kutembelea ndugu na marafiki nikasitisha, kazi nikawa nafanya basi tu kwa kujisukuma ili nipate mshahara . Nikawa napenda mitoko mitoko kule calabash na kwingineko na mvinyo kidogo na nakadhalika. Katika hicho kipindi cha miaka mitatu ya msongo nilikuwa nahangaika kujinasua hivyo nilikuwa nasoma machapisho mbalimbali na kujifariji kwa nyimbo za dini na za secular. Taratibu nikaanza kubadilika nikaanza kurudi kwenye maisha ya kabla ya kibuti na nikawa na ari ya kufanya yale yote niliyokuwa napenda kufanya au niliyokuwa najiona siwezi kufanya. Nikarudi kanisani, (kule kule nilikobatizwa sijawahi kuhama) safari hii kwa kishindo zaidi maana nilienda mpaka kuimba kwaya (Kwaya nilikuwa nikiimba toka sunday school mpaka ukwata o na a levels ila nilivyofika chuo kikuu nikaona ni kupoteza mda. Mwe!) Basi nilivyorudi huko kanisani wakadai wanaona roho ya uongozi ndani yangu wakanipachika vyeo humo basi kwa kuwa nilishakataa ile sauti inayoniambia siwezi, sina muda... mi nikakubali majukumu na naendelea nayo.

Nafurahia maisha, siogopi tena kuachwa wala changamoto yoyote hainitishi maana huku kanisani tunakutana na kina mtume paulo wakituambia majaribu hayana budi kuja...Mungu hataruhusu jaribu kubwa kutushinda.....majaribu yanajenga perseverence na perseverence inajenga character n.k. Haya maneno nilikuwa nayajua tangu utoto wangu ila niliyaelewa baadae sana. lol. Kuna wakati tunaamini Mungu anatuacha tupigike, tuhangaike wenyewe, tushindwe ndo tumkumbuke. Kusamehe si kazi ndogo atii ila ukifanya kwa nguvu ya imani inawezekana. Kila mtu ana jinsi yake ya ku-handle stress. Wanawake wenye masahibu wapo kila mahali: baa, saluni, nyumba za wenyeji, kanisani na barabarani. Na si walioachwa tu bali hata walioolewa na waume pasua vichwa. Wamama wanapanda mpaka ndege jamani kwenda kwa nabii nanii kuombea hubbies na kuchukua mafuta wanapaka kwenye boxer za kina baba lakini wapi! Wengine wameona Mungu wa kanisani anaweka usiku wameamua kuhanja kwa waganga. Acheni tu jameni! Wengine wanakuwa kwenye mpito, wengine wanapotelea humo moja kwa moja. Hivi wanaume wakikumbwa na vibuti au ndoa ngumu wanaendaga wapi? huwa naona kama wakifilisika ndo wanapuyanga kwenye makanisa maana hata hela ya bia wanakuwa hawana.
 
Hahahahahaaaaa well said aiseee. Umenikuna sana wa kwangu niliyeachana nae nasikia kajifungua mwezi uliopita. I wish angesoma hiki ulichokiandika hapa
 
na kuandika meseji za mafumbo kwenye whatsapp status zao
 
Kwani wangekuwa walevi au malaya baada ya kutendwa ungeuliza hapa? Ujinga tu kukaa unafuatilia maisha ya watu makanisani fanya yako tafiti za hivyo hazitusaidii ktk jamii. Kwa hiyo wafanyaje?

Anataka waende kwa waganga wa kienyeji
 
si wanawake tu, hii ni hulka ya wanadamu walio wengi hata wanaume. Akishaona hali ni ngumu ndo anamkumbuka Mungu
 
Back
Top Bottom