Kwanini wanawake hawaruhusiwi kuuza nyama buchani?

Kwanini wanawake hawaruhusiwi kuuza nyama buchani?

bucha nyingi za kajamba nani wanauza wanaume haohao ila kuna zile viwango sana aisee
unakutana na wadada wazuri anakuuzia nyama utadhani imeiva tayari
ulikuwa unachukua nusu unashangaa mkeo anakuuliza mbona umeleta kilo mbili?

wanauza ila sema wachache wanabahatika kupata mazingira rafiki
 
Haha sijawai kujiita aisee, kwani sifa za kuwa mwanamke wa shoka ni zipi?

Butcher la kigogo na mashoka ni kwa wanaume tu 😂
Sifa za kua mwanamke wa shoka nizijuazo mimi ni pamoja na
Kujiamini,
Uwezo wa kuendesha maisha yako/Kutokua tegemezi,
Ujasiri.......
 
Tatizo lako bucha unayo ifahamu ni ile yenye mapanga, mashoka, na ile mgogo mkubwa ambao sasa umekatazwa na serikali.

Kwa bucha kama hizo hutakaa uone mwanamke akifanya kazi hapo.

Bucha za kisasa zipo na wanawake ndio wanafanya kazi humo.. nyama inakatwa kwa mashine, friji za nyama, chumba usafi wa ukweli.. etc.

Pale mlimani city mbona nyama inauzwa na wanawake au nini maana ya bucha kwako?
Umejibu vizuri nenda bucha yeyote uchukue nyama nakuja kulipia
 
Hakuna athari wala katazo lolote kwa kina mama kuuza nyama buchani
 
Kama mwanamke anaweza kua doctor,engineer,pilot wa ndege za kijeshi,rais etc sioni kwanini ashindwe kufanya kazi ya kiboya tu kama ya buchani yaani(kukata nyama,kupima na kuidumbukiza kwenye mfuko).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom