Kwanini wanaume watu wazima hampendi kupewa shikamoo?

Kwanini wanaume watu wazima hampendi kupewa shikamoo?

Umeona sasa Zombi huo ndio ukweli shikamoo haina haja ya kukataliwa.

Sema sasa kuna wengine hata ikitokea hivyo bado shikamoo yako wanakupa tu.
emmyta acha zako hizo mbona kama unanizungumzia mimi vile kwa comment yako hii
 
Nishauri sasa, nikutanapo na mtu mzima umri kama baba yangu, je nimpe salamu gani?
Subiri akuanze! Akikuambia hujambo, shikamoo ni mahali pake.

Ukiona mzee anakuambia mambo, ujue hafagilii shikamoo!

Unaweza kutumia salamu za dini kwa unayemfahamu imani yake kama hapendi shimamoo.

Salamu za makabila pia zinafaa kwa mzee unayejua kabila yake!

N.B Salamu hii "Shikamoo ~ Marahaba" imeleta migogoro katika jamii. Tuitumie kwa uangalifu.
 
Kwa hiki walichoandika kuanzia post ya pili mpaka hapa nilipofika inaonyesha dhahiri wanaume walio wengi hawapendi shikamoo.

Poleni sana sababu sidhani kama inapunguza kitu muwage mnazipokea tu jamani.


"Shikamoo" maana yake nipo chini ya miguu yako. Waarabu walikuwa wakiamkiwa na watumwa wao.
 
Back
Top Bottom