Kwanini wanaume watu wazima hampendi kupewa shikamoo?

Kivuruge girl

Senior Member
Joined
Jan 18, 2018
Posts
131
Reaction score
160
Habari wana jamvi,

Naamini mko na siku njema. Kuna jambo ambalo huwa linanisumbua nikaona sio vibaya nikashare nanyi huenda nikapata uelewa.

Nimeshawahi kukutana na wanaume, watu wazima ambao kiukweli wamenizidi umri na nastahili kabisa kuwapa salam ya heshima "shkamoo" ila cha ajabu hawa watu wazima either watajifanya hawajasikia salamu yangu au hawataitikia kabisa. Ni umri ambao kiukweli kabisa wanakaribia au huenda wanalingana na baba yangu mzazi. Sasa why wakatae kuitikia salamu zangu??? Je ni kwangu tu au kuna wenzangu pia yashawahi kuwakuta?
 
Shikamoo za siku hizi siyo ishara ya Heshima? Ndiyo maana wanazipotezea
 
Ah..!!.
shikamoo za siku hzi si za heshima ni kama kejeli tu.
binafsia inatokeaga kuamkiwa ila huwa navunga tu
 
Habari wana jamvi,

Naamini mko na siku njema. Kuna jambo ambalo huwa linanisumbua nikaona sio vibaya nikashare nanyi huenda nikapata uelewa.

Nimeshawahi kukutana na wanaume, watu wazima ambao kiukweli wamenizidi umri na nastahili kabisa kuwapa salam ya heshima "shkamoo" ila cha ajabu hawa watu wazima either watajifanya hawajasikia salamu yangu au hawataitikia kabisa. Ni umri ambao kiukweli kabisa wanakaribia au huenda wanalingana na baba yangu mzazi. Sasa why wakatae kuitikia salamu zangu??? Je ni kwangu tu au kuna wenzangu pia yashawahi kuwakuta?
Umeshawahi kujifanyia assessment mwenyewe, Kwa nini hawaitikii shikamoo yako? Pronounciation yako, mavazi, body language etc.
 
Kuna kipindi nilienda mwanza sehemu moja inaitwa buswelu nilikuwa naamkiwa shikamoo na watu wakubwa kbsa wengine umri sawa na mamangu nilishangaa sana
 
Wewe umeona Wanaume tu!?

Je hujawaona wale Wamama (hususan mijini) "wanaosema usinizeeshe tafadhali"
 
Shikamoo huwa haina maana yoyote kwa maana ya salam inayotaka kujua hali asalimiwaye...
Kiingereza
Good Morning sir.....Good morning etc unajua hali yake kuwa nzuri..

Ingependeza kusema Habari za Asubuhi Baba ....Nzuri au Mbaya ndipo shikamoo ifuate...
 
Back
Top Bottom