Kwanini wanajeshi wa Marekani wanastaafu utumishi mapema?

Kwanini wanajeshi wa Marekani wanastaafu utumishi mapema?

mugebuka

New Member
Joined
Mar 15, 2026
Posts
3
Reaction score
4
Naomba wajuvi wa mambo wanasaidie nifahamu ni kwanini wanajeshi wa marekani wanastaafu mapema ukilinganisha na huku kwetu?
 
Naomba wajuvi wa mambo wanasaidie nifahamu ni kwanini wanajeshi wa marekani wanastaafu mapema ukilinganisha na huku kwetu?
Marekani ni KAMPUNI.

Hakuna wanajeshi wa kizalendo.

Kuna Watu wanapigana kwasababu WANALIPWA.

Ndio maana MAREKANI inachukua mtu yoyote wa nchi yoyote kuwa MWANAJESHI.

Ni kama MAROBOTI ya VITA, just for MONEY.

With MONEY unaweza kuondoka muda wowote ukiona umechoka au umemaliza.
 
Leo libya,kesho ukraine,kesho kutwa iran wiki ijayo venezuela mwezi ujao mpo mlango wa bahari wapi uko sijui mnatishiana makombola na urusi hizo mbanga zote kwanini usistaafu mapema???
Bongo kungekuwa na kashikashi kama hizo watu jeshi wangeliona kama ukoma
 
Ukifikisha 45 inabidi ukapumzike, teknolojia ya USA inataka damu changa sio lizee

Huku bongo bado JW linavunja matofali Kwa kichwa hvy bado wapo wapo hawana haraka na teknolojia
Hawa Wetu Wamefubaa Sana
 
Ni Ajira...mikataba mna renew kila baada ya miaka minne...so unaweza amua u sign tena.
 
Sio kweli mkuu, mwaka huu wame extend umri wa kuingia jeshini mpaka 42yrs.
Kinachofanya wastaafu ni rank na umri kutoendana pamoja na ujuzi.. sie nashangaa jeshini wanatutenga watu wenye 40 wakati tuna vitu vya kupeleka kule
 
Majeshi yote duniani yana aina mbili za watumishi - Maafisa ambao wanapewa commision hawa wanastaafu kulingana na vyeo wa juu kabisa anastaafu na umri mkubwa zaidi

Brigedia kwenda juu ni 60yrs
Kanali 58yrs
Luteni kanali 56 yrs
Meja 54yrs
Captain 52yrs
Luteni na luteni usu 50yrs
Warrant ofc class 1 58yrs na class 2 56yrs
Sajent na staff sajent kushuka chini 54yrs umri wa lazima ila wanaandikishwa tu hawa hawaajiriwi na wanakuwa mikataba ya miaka 6 tu baada ya hapo wanarenew kwa hiyari kila baada ya miaka 2 hadi wafikie kikomo cha 54yrs

Pia, madaktari wa jeshi hawastaafishwi kwa sababu ya umri pekee mpaka wafikishe miaka 62 bila kujali kafikia cheo gani
 
Leo libya,kesho ukraine,kesho kutwa iran wiki ijayo venezuela mwezi ujao mpo mlango wa bahari wapi uko sijui mnatishiana makombola na urusi hizo mbanga zote kwanini usistaafu mapema???
Bongo kungekuwa na kashikashi kama hizo watu jeshi wangeliona kama ukoma
Umetisha sana maana huku Malawi wananenepa wanaota mpaka vitambi
 
Back
Top Bottom