Ukweli ni kwamba tunajua kuridhika, hakuna mashindano ya kijinga ofisini...Huyo Mkuu wa shule ana Boda Boda, mratibu Elimu ana baskeli...me nikakimbilie mkopo wa gari kisa cha kujitia stress nini? Akuu
Halafu hatuna stress za ntakula nini, tunakopesheka yani...nimeshuhudia huku nabebembelezwa kukopa nyama kiroho safi...tunaaminika sa we jaribu kukopa uone unavyopigwa cha mbavu.
Halafu hamna stress za kukutana na boss kila siku ofisini yani...unafanya kazi unavyopenda wakaguzi wanakuja Mara moja kwa mwakaaa...
Pia ni lifetime job, yani uumwe, uvunjike, upooze mshahara uko pale pale na kibarua hakipo mashakanii...
Kubwaa kuliko watoto wenu wanatupa raha, yani tukisahisha mitihani tunacheeeka hadi makunyanzi yanaondokaaa...wanajua kuandika pumba Wallahi.....
nimemaliza...