Habari wanajukwaa,
Kuna ka usemi nilikua nakasikia tangu nikiwa shule O-level ila nilikua siamini eti walimu hawazeeki haraka. Kwa kweli nimekuja kushuhudia na kuchunguza juu ya hilo na kuona ni kweli kwa 100% maana juzi kama bahati nimekuta na mwalimu wangu ambaye alinifundisha vidudu(chekechea) sikuweza kuamini kwani haikunipa tabu kumtambua nilivyomuona mara moja niliweza kumfahamu.
Kiukweli yupo vilevile na bado anafundsha na ameweza kufungua center yake mwenyewe sio huyo tu na wengine wengi kuanzia primary mpaka secondary sijajua kiiman kwamba mwenyezi Mungu amewabarki ama vipi au niikwanini inakuwa hivyo.
NAWASILISHA
Ninakuunga mkono zaidi ya 1000%.
Mfano upo kwangu mie na mwalimu wangu wa "awali".
Kuna mwalimu wa kike alinidhulumu haki yangu ya "mashoto" na kunifanya nijifunze kuandikia "kulia" bila kupenda!
Wakati nikiwa la kwanza, ndiye alikuwa mwalimu wa mwandiko.
Sasa sielewi alikuwa na chuki gani ama upeo wake mdogo!
Tulivyoanzia kuchora chini ananiangalia tu, tukahamia kwenye tablets(mbao) ananiangalia tu na shoto langu.
Eti tulipoanza kuandikia karatasi ndipo aliponidhalilisha: vuta masikio yangu yote kwa kuninyanyua juu kisha akanikita konzi hadi nikaona nyota nyota na kunisindikiza kwaa maneno: "ukome kuandikia hilo kono lako la mavi"!
Niliumia, sikuwa na ka kufanya, lakini nikawa na kinyongo cha kutokumsamehe kwa uonevu.
Nilipomaliza mizunguko ya masomo na kupata ajira, nikaja nikakutana naye sehemu nikamuona bado kijana tena mbichi bado, nikamficha identity nikamuelewa na kumtokea.
Lengo ni kutoa kinyongo cha kisasi cha miaka mingi juu yake na kisha tukawa wapenzi.
Ndiyo ninasapoti hoja hii, kwamba walimu hasa wa kike hawazeeki haraka, aidha kwa kutofanya kazi za suruba ama "dongo" lao lao ni zuri.