Kwanini Walimu hawazeeki kama wanafunzi wanaowafundisha?

Kwanini Walimu hawazeeki kama wanafunzi wanaowafundisha?

Nilikutana na Mwalimu wangu wa Darasa la kwanza nikiwa nimeshaanza kazi. Yeye alinikumbuka mimi sikumkumbuka ilikuwa barabarani tu Dar. Basi akaanza kuniambia alipo wakati ule Wizara ya elimu nami nikamwambia nilipo na nilisomea wapi O na A level na chuo HOLAAA. Akaniambia alikuwa wapi sekondari HOLAAA! Nikamwambia nilisoma shule ipi msingi. Hapo ndiyo akaniambia alikuwa Mwalimu wa shule ya msingi pia Mwalimu wa darasa kwenye darasa langu la kwanza. Nilishangaa sana kwani alikuwa bado anadai sana na anavyojipenda ningeweza kabisa kumpigia speed. Basi tukaagana akaniambia kama una shida Wizarani karibu sana nipo pale muda mrefu na nimewasaidia wengi sana.
 
Aah pamoja na maudhi ya watoto ila wana vituko jamani. Yaani kikitoka kituko hiki kinakuja kingine hadi unasahau kama baba mwenye nyumba anakudai. Halafu pia walimu wengi tunaishi maisha ya vipato vyetu, hivyo tumejiridhikia na shida zetu. Ugali wako na dagaa saafi unalala unaota umekuwa rais wa nchi, ukiamka unapiga kitenge chako mpauko huyooo kucheza na watoto.
 
Nlikutana na mwalimu wangu wa shule ya msingi kipindi nasoma alikuwa kijana, mwaka juzi nlipomuona bado Yuko vilevile Kama vile kanizidi mwaka au tumelingana. Wakati enzi hizo akija kuanza kazi nlikuwa na miaka 8. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwanini radhi wakati unakula vyakula vya kujenga afya na kukuepusha na magonjwa mengi kama shinikizo la damu
Umeandika wanakula hivyo kwakuwa mshahara nu mdogo Jambo ambalo SI kweli
 
Mazingira yao ya kaz pia yanachangia. Japo ni magumu ila yanawapa furaha mda mwingi
 
Ukiona bado anafanya kazi ujue bado hajazeeka kawatafute waliim waliostaafu utaona wamezeeka
 
Jamani Mimi huwa najiuliza Nini kipo ndani ya ukuaji wa walimu? Nimefatilia walimu hawazeeki nikiwaona walimu wangu wa primary wapo vilevile pia hata wakistaafu hawafi mapema Kama wafanyakazi wengine hivi ni kwanini
Mkuu umeongea ukweli mtupu alafu naongeza kingine , walimu wengi hawana mavitambi
 
Mimi Ni mwalimu kuna mwanafunzi darasani kwangu yupo kama Paula ananikwamisha ..Wajuzi vipi hivi kuna mtu kafungwa 30yrs kweli nchi hii
mwalm mwalm,unamezea mate watoto wetu tena.nikijua shule unayofundisha simleti mwanangu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom