Siku walimu watakapogundua kuwa wanafunzi ni wateja wao ufaulu utaongezeka na watoto makini watazalishwa. Taifa litasonga

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,119
Habari!

Kuna kitu hakiko sawa kwa watumishi wa umma karibu kada zote.

Wanahudumia watu ili liende tu wakijua mshahara na posho viko palepale.

Leo ngoja niwazungumzie walimu.

Mwanafunzi ni mteja wa mwalimu hivyo inapaswa amhudumie kama vile costomer care wa mitandao ya simu wanavyohudumia wateja wao wanapopiga simu au kwenda ofisini kwao.

Kwakuwa serikali na mzazi ndio wabeba majukumu basi walimu wanasahau kuwa uwepo wao umetokana na watoto wanaowafundisha bila kujali wamelipiwa ada na mzazi au serikali.

Mtoto anatakiwa aone shule ni mahali salama.

Kuna shule moja ya msingi ya serikali (Shule ya msingi Mvuti) iko Mvuti Ilala Dar es salaam. Yule mkuu wa shule ni kama chizi, hata ukipita njiani karibu na ile shule utamsikia anabwabwaja kama kichaa.

Sijui walimu na wanafunzi wa shule ile wana hali gani.

Private schools kidogo wanajitahidi, watoto wanawapenda walimu wao na wanawaona kama wazazi wao.

Wakati tunasoma primary na sekondari miaka ya 2000"s kulikuwa na walimu walikuwa wanatafuta sifa kwa kuchapa wanafunzi.

Ilifika wakati wengine waliacha shule kisa walimu hao. Yaani hujaja jana ni mwendo wa fimbo za kutosha bila kuuliza sababu iliyopelekea kijana kutokuja shule. Na hata ukijitetea ni fimbo tu.
 
Back
Top Bottom