Kimsingi kusudio la hadithi lilikuwa kwa ajili ya ufafanuzi tu mfano; ukisoma sura/Aya Kwenye Quran kama hujailewa unaweza kutafuta hadithi/ historia ya hicho kifungu kuwa kiletwa wakati gani na maksudi yake yalikuwa nini na kukufanya uelewe kwa undani. Hiyo ndio ilikuwa kusudio la msingi la hadithi;
LAKINI sasa waliingia mamluki wakaandika mila za kiarabu na waposhoshaji waka andika habari za kudhalilisha na kuziita hadithi.....na hata kwa akili ya kawaida ya darasa la nne ukisoma walicho andika utaona kabisa ni upotoshaji wa hali ya juu. Wanao weza kuamini huo upuuzi ni wale walio soma kwa kuunga unga huko mashuleni...
Hivyo zile hadithi zilizo elezea kila sura ilivyokuja na maana iliyokusudiwa ndio sahihi....
Lakini ikumbukwe pia kuwa Mitume wote akiwemo Yesu walikuwa ni watu kama sisi (wanakula, wanaenda choo, wana lala usingizi, wanaumwa, wanaomba kwa Mungu awape uwezo wa kutenda nk ) tofauti yake na sisi ni kuwa, walikuwa na uwezo wa kupokea ujumbe kutoka kwa Mungu.
Kwa mujibu wa Uislamu:
🔹 1. Aliyetunga Muhamad
Waislamu wanaamini kuwa Qur’an ni neno la moja kwa moja kutoka kwa Mwenyezi Mungu (Allah).
Haikuandikwa au kutungwa na mtu yeyote—bali iliteremshwa (wahyi) kwa Muhammad kupitia malaika Jibril (Gabriel).
Hii inakuja kuonekana imeandikwa na wahusika wapo chini. Ni mkanganyiko inajichanganya yenyewe na watu wengi sababu ni Maamuma hawajui wanadanganyika.
“Hakika huu ni ufunuo unaoteremshwa. Umeteremshwa na Malaika mwenye nguvu.”
(Qur’an, Surah At-Takwir 81:19-20)
🔹 2. Muhammad hakuiandika mwenyewe. Sababu hakujua kusoma wala kuandika
Muhammad alikuwa hajui kusoma wala kuandika (Ummi), kama Qur’an inavyosema:
“Wala wewe hukuwahi kusoma kitabu kabla yake, wala kuandika kwa mkono wako…”
(Qur’an, Surah Al-‘Ankabut 29:48)
Alikuwa anasikiliza ufunuo, kisha akiwaambia Maswahaba wake, ambao walihifadhi na kuiandika.
Nani waliandika Qur’an?
🔹 3. Waandishi wa Wahyi (Ufunuo)
Baada ya Muhammad kusoma ufunuo, waandishi wake waliandika Qur’an kwenye vitu kama:
Ngozi ya mnyama
Majani ya mtende
Mifupa mikubwa
Mawe mepesi (slates)
Waliokuwa waandishi mashuhuri wa Qur’an ni:
Zayd bin Thabit
Ali bin Abi Talib
Ubayy bin Ka’b
Mu’awiyah bin Abi Sufyan
Abdullah bin Mas’ud
na wengine wengi
🔹 4. Kukusanywa kwa Qur’an kuwa kitabu
Baada ya kifo cha Muhammad, Khalifa Abu Bakr alianzisha kazi ya kukusanya Qur’an yote na kuiandika katika kitabu (mushaf) kutokana na kumbukumbu za waandishi na walihifadhi.
Kazi hii ilifanywa na Zayd bin Thabit
Qur’an iliendelea kuhifadhiwa na kusomwa kizazi hadi kizazi.
Kisha wakati wa Khalifa Uthman bin Affan, nakala za Qur’an zilisambazwa kwa miji mikuu ya Kiislamu ili kuwe na umoja wa usomaji (qira’ah).
Wengi hudai kuwa Qur’an iliandikwa na watu au "kuiga" kutoka dini nyingine hasa Torati ya Wayahudi na Imani za Kikureshi. Ni kweli pia walisikia hadithi hizo na kuzichukua.
✅ Muhammad alipokea na kusoma ufunuo huo kwa watu
✅ Maswahaba waliiandika na kuihifadhi
✅ Waliandila kadri walivyokumbuka na kukumbushana
“Hakika Sisi ndio tulioteremsha Qur’an, na hakika Sisi ndio tutailinda.”
(Qur’an, Surah Al-Hijr 15:9)