Kwanini waislamu hawana imani na vitengo vinavyohusika na takwimu?

Umechangi vizuri sana especial mwisho!

Kuhusu kutokupanga uzazi na maswala ya kuoa wake zaidi ya mmoja.... mfano mimi wale tuliomaliza nao Dodoma Sec miaka zaidi ya 12 iliyopita marafiki zangu "wakristo" wengi wao hawajaoa/olewa na walio oa/olewa hawana mtoto zaidi ya mmoja! Lakini rafiki zangu wa kiislam wake kwa waume nikiwamo mimi tuna watoto zaidi ya mmoja! Madhalan mimi nina wake wawili in ten years siwezi kuwa sawa na Rafiki yangu ambae hana mke wala mtoto maana mimi dini yangu hainiruhusu kufunga uzazi kwa njia yoyote ile! that means nitakuwa na watoto wa kutosha tu!

Take from me then zidisha kwa hao waislam wachache uwajuao wewe.

Mkuu kwanza hongera kwa kuwa na wake wawili. Lakini kwanini unaona wawili? kwa sababu dini inakuruhusu? uchumi unakuruhusu? na hao wake waili unaweza kuwatunza vipi? au ndio wanaishi maisha magumu kila kukicha? Do you real think this is smart? Unadhani kwanini wenzako uliomaliza nao sekondari hawajaoa, wana matatizo ya kibaiolojia au?

Ukiangalia kwa undani suala hili unaweza kukuta kuwa ndio linachangia kwa baadhi ya watu kukosa elimu. kuna watu wana wake wanne na watoto 12 lakini hana uwezo wa kumpa chakula bora mtoto mmoja kwa mwaka mzima, au kumsomesha mtoto hata mmoja hadi chuo kikuu cha maana, matokeo yake wanasema eti mtoto anakuja na riziki yake. Kuna wengine mtoto akifika darasa la saba anasema sasa umekua jitafutie maisha. Vicious circle.
 
Kwa upeo wangu na maoni yangu naona kuna tabaka linajaribu kujijenga na litakua na madhara makubwa kwa walijengao.

Mfano katika abuja declaration walikua wanaandaa namna ya kuongeza idadi ya waumini wa dini ya kiislam. Na miongoni mwa njia walizo azimia ni
1. Wanaume/wanawake wa kiislam kuwa na mahusiano na watu wa iman nyingine na baadae huwashawishi wabadili dini.
2. Kuoa wake zaid ya mmoja.
3. Kujitahidi kuwa na idad nkubwa ya watoto na mengineyo.

Sasa hapa najaribu kuona nini kitatokea iwapo baba mmoja atakua na wake watatu, na kila mkeatakua na watoto watatu. Katika mtazamo mdogo huyu baba atakua na watu tisa wa kuwahudumia.

Swali je ataweza kuwapeleka wote katika shule na kuwatimizia mahitaji yao muhimu?

Ikiwa atashindwa hapa linazaliwa tabaka lingine la wasio elimu au wenye kiwango kidogo cha elim.

Sasa katika hili ukutane na mtu wa imani nyingine mwenye mke na mtoto mmoja au wawili hata ikiwa mnalipwa mishahara sawa lazima jamaa maendeleo yake yataonekana kwa urahisi zaid. Hivyo huyu wa iman nyingine huweza kumpatia mtoto wake elimu bora ikiwa ni pamoja na kumudu kutoa huduma za msingi kwa mtoto wake.

Sasa hapo huoni kua kunatabaka la "maisha nafuu" na "maisha ya sio nafuu"

hata ikija kielimu lazima utaona tofauti. Je hili nalo alaumiwe nani? Je ata hiyo sensa itawakomboa na hili?
 
Great Thinker watathaminika mawazo yao tu wataweza kutumia vigezo ktk tafiti zao na sii logic ilokufungia katika kabati la kiimani. Uislaam ama Ukristu ni imani ambazo tumekuja pingana kutokana na fikra za mwanadamu. na hakuna kati yetu anayeweza kunambia Ukristu kwa kutoowa wake wawili au zaidi kunakuweka karibu sana na Mungu iwapo Abrahamu alioa wake zaidi ya mmoja na Yesu hakuoa kabisa.

Hili swala la sensa lisitumike tuonyesha tofauti zetu kiimani isipokuwa bado ni matakwa ya watu fulani kuchagua nini kiwepo na nini kisiwepo na kwa sababu zao wenyewe. Sensa haina maana nyingine zasdi ya kuwatambua wananchi wako kwa tafuti zao zote iwe toka watoto kwa jinsia zao, vijana kwa jinsia, elimu, kazi na makazi yao, watu wazima vile vile, na hata wazee, wanawake kwa waume, vilema, yatima na kadhalika kwa sababu takwimu hizi ndizo hutuandaa sisi wote na sio serikali tu kuandaa mipango ya maendeleo ya wananchi.

Unapoondoa kipengele kimoja ktk ukusanyaji wa takwimu kwa sababu ambazo zinaweza kutumika kuondoa vipengele vyote muhimu, hapa ndipo tunaposhindana wala sii ukweli wa kina nani wengi kuliko wengineo. Binafsi ningependa sana kujua hesabu ya wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara waliojiandika ili kujua ulipaji wao wa kodi. Je, pamoja na kuwezeshwa kwa wanawake tumefika wapi na wapi bado hatujawatazama zaidi.

Maadam tumerudishwa ktk mfumo wa mkoloni ktk sekta ya ELIMU na AFYA waislaam na watu wengineo wote wanayo kila haki ya kutaka kujua takwimu zao ili wajipange kuwezesha jumuiya zao kwa sababu hata mkoloni alipojenga shule alisema ni kwa ajili ya watu wote, lakini kufikia mwaka 1961 tulijikuta tuna madaktari wawili tu nchi nzima. Ubaguzi upo sana tu na hii habari ya kuondoa kipengele cha dini kunadhihirisha wazi wasiwasi ya viongozi kuonyesha ukweli ni upi laa sivyo kama ni uongo hakuna sababu ya kuogopa tuhesabiwe wote kwa makundi yetu.

Mimi ukubwa wa familia yangu mama mkubwa ambaye ni dada yake mama yangu ni mkristu na baadhi ya wanawe lakini hatuchukiani wala kutengana, mapenzi yako pale pale tuna heshimiana.. Kifupi ukoo wangu kuna wakristu wengi zaidi ya waislaam na haijawa tatizo. Kuondoa kipengele hiki kuna sababu zaidi ya kile wanachotaka sisi tuamini..Something isn't right!
 
Mohamed Sosshi, Onga mshi osie, haya ni kwedi Toronto Koogwe!
Umeileta hoja vizuri kwa kuijenga katika takwimu.
Katika post yako# 11 umesema 'nimeleta hoja hii ijibiwe na GT bila chembe za kudhihaki waislam kwa hoja nyepesi''
Kwa bahati mbaya sana wewe mwenyewe umetoka katika mada ya sensa ulioijenga kimantiki na kukaribisha hoja za EAMWS,watoto madaraka, elimu na utumishi na hapo ndipo ulipokaribisha hoja nyepesi.

Kabla sijaingia katika mada yako nikutahadharishe kuwa Ngongo alipoomba reference hakumaanisha uvivu wa kusoma. Alichotaka kama mimi ninavyotaka ni wewe uweke reference ya nani ume quote ili kujibu hoja kutokana na source na maudhui yake. Mfano, Mohamed Said amekariri mara nyingi sana kuwa idadi ya waislamu ni 60% au zaidi. Je tukienda maktaba inatosha kunukuu tu bila kujua nani mwandishi na source zake ni zipi na je zinaamika!
Katika uandishi hatu quote tu contents bali source nzima kwa ujumla wake.

Takwimu ulizoweka zina biasness kutoka kwa wewe mwenyewe.
Sensa ya mwaka 1957 kwa mujibu wako waislam walikuwa 58% wakristo 32% na wapagani 10% kwa uwiano wa 2:1 (aya ya 5).Labda sijui hesabu lakini huwezi kuwa na 58:32 halafu ukawa na uwiano wa 2:1.
Kibaya zaidi umeacha nje 10% ya wapagani ambao ni statistically significant to determine the ratio.
Hadi hapa ni wazi umeongozwa na jazba na si ukweli. Namba zako zinakusuta mwenyewe.

Post# 11 umesema baada ya uhuru waiislam waliandikisha watoto wengi shule baada ya kukandamizwa na mkoloni.
Ukweli wa historia ya wakoloni unaunga mkono hoja yako kabisa na hata rais BWM na wengine wanakubaliana na hilo.
Post# 3 umedai iweje waislam walioandikishwa kwa wingi wawe nyuma kielimu, utumishi na madaraka?
Hapa umesahau kuwa suala la elimu, madaraka na utumishi halitegemei quantity bali quality.
Je, hao walioandikishwa walimaliza shule? walifaulu vizuri? walirudi kuisaidia jamii yao?

Mfano, wakati wa mpango wa MEMKWA Wilaya ya Kilwa iliandikisha wanafunzi wengi. Wengi wakapata nafasi za shule za kata. Miaka minne shule imefungwa kutokana na wanafunzi kukimbia (ref; Mkurugenzi wa halmashuri Kilwa).
Kwa mwendo huo, 10 years down the road utapata Mwalimu kutoka Kilwa? Utapata katibu kata kutoka Kilwa? Utapata Mbunge/Injinia au Daktari kutoka Kilwa? Je wingi umesaidiaje kutatua tatizo la uwiano?

Na hapo inaingia hoja, wazazi wa Kilwa wakishirikiana na Wabunge wa Kilwa, Mkuu wa Wilaya, katibu kata, wanakamati wa shule za Kilwa wametafutaje ufumbuzi wa tatizo hilo?
Nani katika makundi ya Budha, wapagani, wasioamini, wahindi, wajadi na wakristo ametumika kuihujumu Kilwa yenye Waislam takribani 95%?

Mfano wa pili, shule ya Ali Hassan Mwinyi ilikuwa na watoto 250 na walimu 2.
Shule ya Feza Dar es Salaam ilikuwa na watoto 25 na walimu zaidi ya sita kwa Darasa.
Ali Hassan ilifaulisha div 4 mmoja na wengine 0.
Feza ilifaulisha div 1 na 2 watoto 22 na division 3 watoto 3. Kwa mtazamo wako 10 years down the road unategemea kupata mtumishi au kiongozi kutoka shule gani kati ya hizi mbili!

Bongolander, mimi sidhani kuwa na wake 2 au watoto 12 ndilo tatizo pekee kwa waislam. Tena basi inaonekana unaunga hoja ya Mohamed kwasababu huenda unazo takwimu zinazoonyesha kuwa umasikini, ujinga na maradhi ni matokeo ya dini fulani kuwa na utaratibu fulani. Hapo maana yake ulete data za kuonyesha na kuthibitisha hilo.
Kama ni hivyo basi tuletee data ambazo hazitakwepa sensa hata kidogo.

Hoja yangu hapa ni kuwa kwa mimi niliyesafiri Tanzania kwa asilimi 96 tena vijijini nimeona kwa macho yangu kuwa ujinga, maradhi na umasikini upo kwa watanzania bila kujali imani zao. Masikini wa Nyangao Lindi na yule wa Amani Muheza au Shirati Musoma ni waathrika wa mfumo wa utawala na wala si udini.

Lakini pia unatakiwa uliangalie suala hili kisosholojia.
Hivi yule aliyeoa wake 2 na watoto 6 anatofauti gani na yule mwenye mke mmoja na vimada 2 wenye watoto nje ya ndoa 5. Who stands in better position to take care hata kama si kwa kiwango hicho.
Ningependa watu waangalie mambo kwa mtazamo mpana zaidi si kwa hisia, jazba, ushabiki au udini.

Mammamia; Nakubaliana nawe kabisa kuwa watu wanaangalia dini mbili tu hawaiangalii jamii kwa ujumla.
Kwanini tulalamikie utumishi na elimu kwa dini fulani na tuwaache pagans na atheist nje ya majadiliano.
Hivi kuana tatizo gani mtu akiamua kwa utashi wake awe Pagan au atheist.

Kwanini hizi dini badala ya kutuunganisha zinatugawa, ndiyo madhumuni ya dini hayo au ni kutoelewa dini?
Nakubaliana na Mkandara, mimi kama yeye ninaishi katika jamii yenye mchanganyiko sana na wala sijaona tatizo.
Nakubaliana naye pia kuwa sensa ilenge kutatua matatizo ya umasikini,ujinga na maradhi na sina wapi wengi wapi wachache!

Ukiniuliza kati ya umasikini, maradhi na ujinga kipi kipewe kipaumbele, nitakujibu Ujinga kwanza.
Ni ujinga ndio unaotupelekea kusahahu kuwa chumvi hainunuliwi kwa dini, wenzetu wanaopeleka pesa uswiss haziingi katika account za dini, malaria hayachagui dini na wala hakuna ufukura unaofuata dini.

Kama tungeweza kuondoa ujinga, basi ujinga wa nyuzi za kidini usingekuwepo. Tatizo si thread za kidini, tatizo ni ujinga unaozaa thread za kidni na si issue zinazotugusa kama jamii.
 
....

Sensa ya mwanzo ya Tanzania huru iliyoungana iifanyika mwaka 1967 na hii ilikuwa ni sensa ya mwisho kuuliza swali la dini. Sensa zilizobaki zilifanyika mwaka 1978, 1988 na 2002. Sensa ya mwaka huu, 2012 itakuwa ni ya saba katika historia ya nchi yetu na ya tano ya Tanzania huru iliyoungana.

Sensa ya mwisho ya Tanganyika chini ya mkoloni wa Kiingereza katika mwaka 1957 ilionyesha kuwa Tanganyika ina Waislamu 58%, Wakristo 32% na Wapagani 10%. Uwiano kati ya Waislamu na Wakristo ilikuwa ni karibu 2:1 yaani kila penye watu watatu, 2 ni Waislamu na 1 ni mkristo, vile vile unaweza kusema waislamu walikuwa ni karibu mara mbili ya wakristo kiidadi Tanzania.

Mwaka 1967 ndio uliotoa matokeo ya ajabu ambayo mpaka leo sio tu Waislamu bali mtu yoyote aliye na akili timamu ana haki ya kuhoji matokeo hayo. Matokeo haya yalionyesha mgawanyiko wa kidini kama ifuatavyo: WAKRISTO: 33.5% yaani wameongezeka kwa 1.5% kulinganisha na sensa ya 1957. WAISLAMU: 31.4% yaani wamepungua kwa 26.6% katika kipindi cha miaka 10 tu. Hii haikuwahi kutokea sehemu yoyote Duniani iwapo sehemu hiyo haikukabiliwa na janga kama vile vita au jambo lolote lilisababisha idadi kubwa ya watu kufariki. Hata china ambayo imeweka sheria ya kuzaa mtoto mmoja tu basi haikuwahi kupungikiwa na watu au kundi fulani la watu katika nchi yao. WAPAGANI: 34.3% yaani wameongezeka kwa 24.3% kwa kipindi cha miaka 10.
....................

Sisi ni great thinkers tujadili niliyoyaleta jamvini kwa hoja na tafakuri jadidi.

Kuna Kitabu hiki " A Modern History of Tanganyika" By John Iliffe. Pamoja na mambo mengine kimezungumzia sensa ya mwaka 1957. Nimeweka nukuu yake hapa kama image. Bwana huyu anaonyesha kuwa ukristo umekuwa kwa kasi sana na hata serikali ilikuwa haijui namna ambayo ukristu ulivyoweza kukua kwa kasi namna hiyo kutok 2% mwaka 1914, halafu wakawa 10% mwaka 1938, na kufikia 25% mwaka 1957. Utaona kuwa kulikuwa na trend ya ukuaji wa ukristo, siyo upunguaji wa uislamu. Kwa hiyo iwapo sensa iliyofuata ilionyesha kuwa na wakristu wengi, hilo lisingekuwa jambo la kushangaza. Zamani sana kabla ya ukoloni wa kizungu kuingia nchini, sehemu hii ilikuwa inatawaliwa na uslutani wa Zanzibar ambao ulikuwa ni wa kiislamu, kwa hiyo miaka hiyo ya nyuma waislamu ndio waliokuwa wengi, huku pia wasiokuwa na dini wakiwa wengi. Sasa hivi ambapo watu wana uhuru wa kuamua dini wanayoitaka usingetegemea takwimu za miaka hiyo ziwe sahihi hadi leo, kumekuwa na kukua kwa ukristo kuliku ukuaji wa uislamu. Ndani ya nchi,huko vijijini huko wengi ni wakristo, na kama unaamini kuwa asilimia kuwa ya watanzania inaishi vijijini basi utaweza kuliona hilo kwenye dini pia.

Wakati kipengele cha dini kinatolewa kwenye documents zote za serikali, ndicho kipindi ambacho serikali ilipoataifisha taasisi zote za dini na kuzifanya za umma, yaani mwaka 1967. Kulikuwa na taasisi nyingi sana za kikristo kuliko za kiislamu wakati huo, ambapo Nyerere alikuwa akiwaona watu wote kama watanzania, kwa hiyo distinction za dini na kabila hazikuwa sehemu ya sera za serikali yake.

Swali la muhumi kujiiuliza ni je serikali ikishajua idadi ya waislamu itafanya nini?

attachment.php
 
Attachments

  • sensa.JPG
    sensa.JPG
    77.7 KB · Views: 670

@Kichuguu utanisamehe sana kusema ya kwamba hizo taarifa alizoandika huyu mwandishi wetu ndizo zilizotufikisha hapa tulipo leo. Na ni kutokana na mfumo ulokuwepo ndio ulosababisha yote yaliyotokea hivyo lazima upime na wewe hoja za Waislaam kwa kulingana na hali halisi. Mwarabu alikuwa na Uislaam na akaingia Mzungu na Ukristu wote wakivutia kwao lakini ni wapi upande wako wewe Mtanzaaia leo unayekataa Udini lakini unapendelea Ukristu wako au miye na Uislaam wangu - where do we stand really?

Ni maajabu makubwa sana wasomi wengi wanaelewa kwamba Mkoloni ktk utawala wake aliweza sana kutugawa sisi watawaliwa lakini waulize kwetu tanganyika Mkoloni alitugawa vipi ili atutawale? wengi hawatakuwa na majibu kwa sababu itamhusu imani yake ya dini japokuwa wanajua fika Mkoloni alivyowagawa South Afrika, Rwanda na hata Somalia isipokuwa Tanzania hawatasema kuwa mkoloni alitumia DINI kutugawa. Hii kwetu ni imani ya roho hivyo ni haki yetu wala sii ya mkoloni..

Hivyo toka mkoloni hesabu ya wakristu iliongezeka kwa sababu Waislaam walilazimika kuingia Ukristu ili wapate Elimu, walilazimika kuingia Uktristu ili wapate hata huduma bora za Afya, kazi na kadhalika na hakuna maendeleo ya binadamu ambayo hayaanzi na ELIMU..Binafsi yangu Kichuguu unajua nilisoma Namibu shule ya Kanisa pale Kibara na nililazimika kubadilisha jina na kudanganya kutokana na msimamo mkali wa wazazi wangu lakini bila shaka hali hiyo ilikuwa na nafuu zaidi kwetu sisi kwa sababu tulikwisha pata Uhuru..

Sasa fikiria wale waliosoma shule zile zile kabla ya Uhuru na wakitawaliwa na mkoloni halafu unakuja ambiwa baada ya Uhuru tulikuwa na madaktari wawili tu nchi nzima..Lilipokuja azimio la Arusha ndipo sisi wote tulipata nafasi ya kujiandikisha na kusoma bila kubaguliwa na haikuchukua muda tulikuwa na wasomi kibao pasipo kutazama imani zao za dini. Ndipo tuliweza kuona ongezeko la Waislaam mashuleni na katika Ajira baada ya serikali yenyewe kuchukua jukumu la kutoa elimu kwa wananchi wote ktk kufuta Ujinga na Umaskini..

Sasa ukitazama Ubishi uliopo hapa na ktk mada hii utagundua kwamba ubishi huu unatokana na kwanza, kutokuwepo takwimu za ukweli kuhusu idadi zetu, na Je seriikali yetu imefanikiwa kiasi gani kuwapa elimu Waislaam waliokuwa wakitengwa kabla ya Uhuru leo hii hatujui, isipokuwa tunalazimisha kukubali kwamba hawatengwi tena baada ya Uhuru na Azimio la Arusha. Lakini ukweli ni kwamba Azimio la Arusha halipo tena, huduma za elimu na Afya sio jukumu la serikali tena bali kuna vyombo vya kijamii na wawekezaji wanatakiwa kupeleka manendeleo haya kwa wananchi. Ni sawa na kwamba tumeweka jeshi la kukodisha sasa kupambana na Ujinga na Maradhi na sio kazi ya serikali tena kama alivyosema Sitta ktk kujitetea kwake dhidi ya madai ya Dr.Slaa - huu ndio ukweli.

Jeshi hili linapokuwa la Kabila moja au dini moja huwezi kuambia litatoa haki sawa kwa wote ikiwa kazi walokabidhiwa na vatican ni kueneza dini. haikuwa hivyo wakati wa mkoloni na tulifahamu kwamba Kanisa na utawala wa Mjarumani au Muingereza hawakushirikiana kuwatenga waislaam bali mfumo wa kanisa pia unawalenga zaidi wale waliomkubali Yesu (Wakristu) kuliko wasiokuwa na imani. Hili hatuwezi kudanganyana hata kidogo.. Hivyo basi kama tunarudisha mfumo wa Azimio la Arusha na kuwa sote ni kitu kimoja badi mfdhama wa kutoa huduma hizi awe serikali tu kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere na nitakubalaian na sensa ifanyike pasipo kuweka kipengele cha dini..

lakini maadam leo Kanisa linamiliki zaidi ya nusu ya shule na Hospital nchini tena wakipewa fedha za walipa kodi kujiendeleza huwezi kunambia kwamba kanisa litatoa elimu kwa kufuata haki na Usawa wakati nina watu walioachishwa kazi ktk shule za kanisa 1995 kwa sababu ya Uislaam wao. Wapo wanafunzi waliokosa shule kwa sababu ya imani zao za dini lakini huu sii ubishi ulotuleta hapa.

Mimi naamini sana ktk Lisemwalo lipo na najua fika kwamba yapo mashirika ya Umma, Idara za serikali madaraka na waajiriwa wake wametokana na KUJUANA. Iwe ukoo wa mtu, kabila ama dini tumefika hapo sasa hivi na lazia tukubali kwamba Azimio la zanzibar limetutenganisha kwa makundi ya kijamii kama ilivyokuwa wakati wa mkoloni.Hili hatuwezi kuliepuka leo, utapata ajira Tanzania kwa kuwa na refa wako, utapata shule nzuri ukiwa na refa hivyo hizi hadithi za Utanzania wakati watu wanafanya ushenzi mkubwa kwa kutenganishwa kijamii siwezi kuzipokea hata kidogo isipokuwa natazama reality iliyopo mtaani.

Kwa kuelewa hesabu ya watanzani ktk jumuiya zao tunaweza kuelewa picha pana zaidi na kujua kwa undani kama waislaam wanatengwa au laa. Sensa itatupa hesabu ya sio tu Waislaam bali hata wakristu ktk sehemu za ujenzi wa Taifa na pengine kupata majibu yenye uhakika kuhusiana na kero za Waislaam.

Haiwezekani waislaam kulalamikia tu mfumo wa Elimu pasipo kuwepo ushahidi halafu serikali inapinga kutumia sensa kupata majibu haya.. Na kibaya zaidi kuna watu wanaogopa kuweka kipengele cha dini kwa kuhofia chuki hii ina maana kuna jambo linafanyika. Chuki haiwezi kutokea ikiwa kuna haki inatumika. Chuki haiwezi kutokea ikiwa hizi kero za Waislaam ni uzushi na tunawezakuwahakikihsia ukweli ni upi kwa kupitia sensa, lakini tumeogopoa hata kufanya hivyo kwa sababu tunaogopa ukweli ukibainika..

This is the only reason maana haiwajahi kutokea ktk historia ya nchi yoyote inayofanya sensa kwa kuweka kipengele cha dini wakaanzisha chuki baina ya wananchi.. hakuna mfano hata mmoja, hivyo lazima kuna kitu tunajaribu kuficha hapa na ikijulikana ukweli basi kweli chuki itajitokeza lakini kwa nani? bila shaka Utawala wa CCM na sio wakristu au kanisa maana wao wamewezeshwa tu na utawala uliopo.
 
Kaka Mkandara,

pamoja na maelezo yako yote; linakuja lile swali la mwishi: Je serikali ikshajua idaia ya watu na dini zao itakuwaje?

Mimi sina wasi wasi sana na law of trends; lakini hata kama itakuwa imekosea, leo ni zaidi ya miaka 30 tangu tuache kutumia dini kama kigezo cha kutambua uraia wa watu wetu, je kuna faida gani kujua dini za raia? Kama tunataka kujua dini za watu, je ni kwa nini tusitake kujua makabila yao ili iwe dhahiri kwetu kuwa ni makabila gani yenge sauti kubwa kwenye jamii?

Tanzania siyo Jamhuri ya kiisalamu, au Jamhuri ya kikristo au jamhuri ya kubudha, au Jamhuhuri ya Kinyamwezi au Jamhuri ya Kikerewe. Kwa nini tuulize watu dini zao au makabila yao? Hiyo inaanza tena kuleta swala lile la mtu kukosa madaraka na kusingizia kuwa ni kwa sababu ya dini yake au kabila lake. Kuna watu waliokuwa na madaraka wakati wa Nyerere lakini leo wanadai kuwa walificha majina yao ya kiislamu ili watunze madaraka hayo; je kama kungekuwa na kigezo cha kuuliza dini yao ndiyo ingekuwa vipi? Malalamiko ya aina hii hukumbusha tena uamuzi wa Mobutu kufuta majina yote ya kizungu na kiarabu na kuondoa vigezo vya dini kwenye rekodi za raia wake. Kuna mambo tunayoweza kutumia nguvu kuyaongelea lakini siyo mambo madogo kama ya kukuza udini au ukabila ambako tulishatoka.

Tuna mambo mengi ya muhimu kushughulikia kama taifa kuliko kubishana kuhusu dini na makabila ya watu.
 
Kichuguu sensa haifanwyi kwa sababu serikali inataka kujua hesabu ya watu wake. Sensa ni ufunuo wa kile tulichokuwa nacho, WATU wake wenye rangi, jinsi, dini na kadhalika. Hivyo sensa inatufahamisha sisi wote na sio serikali tu kutuwezesha kuandaa mipango ya kulitumikia Taifa. We ghave to think what we can do for the country na sio serikali. Hivyo baada ya Ujamaa ambapo serikali ilitupeleka maendeleo hadi vijijini , leo hii ktk Ubepari kila mtu anabeba msalaba wake na unajua fika ndivyo ilivyo..Hivyo ni jukumu letu ktk nafasi zetu kuijenga nchi na kuboresha mahusiano ya kijamii japokuwa tuna tafauti za kiimani. Tunaweza vipi kuboresha mahusiano ya kijamii ikiwa hatuna ushahidi wa takwimu?..

Muda wote mlotumia hapa kubishana unadhirisha wazi kwamba kila mmoja wenu anabuni numbers tena kwa kunukuu vitu vilivyoandikwa over 50 years ago, hii kweli akili?...Kama tungekuwa na takwimu tungeuweka mjadala huu ktk hali tofauti kabisa wala hakuna ugonvi isipokuwa tungecheza na takwimu zilizopo, ushahidi na hata kukubaliana wapi tunafanya makosa. Iwe Waislaam wengi au Wakristu wengi hii sio hoja wala msingi wa kufanya sensa ya WATU isipokuwa kujua what U have in your pocket iwe dime, quarter, nickel, penny or lonnie it all counts to something.

Wakati wa Nyerere umepita sasa hivi tupo ktk mfumo wa kibepari ambao unathamini elimu na Ujuzi wa mtu hivyo kaa kunamtu kweli ananyimwa kazi kwa ajili ya dini yake ni lazima swala hilo liwe addressed na sio kuficha kutokuwepo kwa kuogopa ghasia. Hii nidhamu ya woga ndiyo ilotuponza miaka yote kuogopa kuuliza tukificha madhambi ya watu na huyo Mwandishi alouawa huko Iringa ni habari ya Upepo utakaopita kwa sababu tunaogopa kutafuta ukweli hata kama Polisi wanaua pasipo hatia tukihofia tutavurugana kumbe ndio tungekomesha ushenzi wa polisi na viongozi wake...

Mnachokosea ni kufikiria kwamba Tanzania (nchi na uongozi wake) sio ya Kiislaam au Kikristu lakini mnasahau wanaohesabiwa sio serikali, uongozi wa nchi ama watumishi wa serikali bali ni WATU wote na katiba inasema WATU wake wana dini zao sasa iweje mnataka tupingane na katiba kuwepo WATU wenye dini zao. Hivi kwani tunahesabu Watumishi wa serikali kwa dini zao au tunahesabu WATU wote wanaotafisiriwa na katiba kuwa na imani zao za dini. Mara zote hapa JF watu ndio wanalia na serikali kwa kusema Waislaam wengi wengine waislaam wachache bila kujua wanazungumzia serikali isokuwa na dini, lakini maajabu inapokuja kwenye WATU wenye dini zao mnapinga vikali kuhesabiwa..

Yes, kwa waislaam tukiwa na hesabu ya waislaam nchini tunaweza kupanga mipango ya dini. Mtashindwa (serikali na utawala) kuzuia benki za kiislaam kwa dhana kwamba hazihitajiki wakati za kikristu zinafunguliwa. Mtashindwa (serikali) kuziuia OIC, kutufunga akili na Bakwata, mtashindwa (serikali) hata kuwaacha watoto wa kiislaam nyuma ktk elimu kama ilivyokuwa kwa wanawake. Ni kutokana na sensa za wanawake duniani ndipo walipokuja shtuka jinsi gani walibaguliwa mashuleni na sehemu za kazi.. Hii haina maana anayepinga ubaguzi ndiye mwenye matatizo.. Laa hasha lisemwalo lipo na kama halipo hakuna sababu ya kuogopa sensa. Nina hakika sensa itaumbua mambo mengi sana yanayofanywa kinyume..

Iweje Waislaam waitake sensa yenye kipengele cha dini lakini wakristu hawaitaki wakati huo huo wakisema Waislaam hawakusoma, hawataki kusoma na kadhalika, Mara JK anafanya Udini wakati ktk hili mnamtetea Maneno haya tumeyasikia sana wakati wa mkoloni na tunaona dejavu ikijirudia miaka 50 baada ya Uhuru..We wonna know how many of our kids are in schools controlled by the church..Why not!
 
Last edited by a moderator:
@Kichuguu sensa haifanwyi kwa sababu serikali inataka kujua hesabu ya watu wake. Sensa ni ufunuo wa kile tulichokuwa nacho, WATU wake wenye rangi, jinsi, dini na kadhalika. Hivyo sensa inatufahamisha sisi wote na sio serikali tu kutuwezesha kuandaa mipango ya kulitumikia Taifa. We ghave to think what we can do for the country na sio serikali. Hivyo baada ya Ujamaa ambapo serikali ilitupeleka maendeleo hadi vijijini , leo hii ktk Ubepari kila mtu anabeba msalaba wake na unajua fika ndivyo ilivyo..Hivyo ni jukumu letu ktk nafasi zetu kuijenga nchi na kuboresha mahusiano ya kijamii japokuwa tuna tafauti za kiimani. Tunaweza vipi kuboresha mahusiano ya kijamii ikiwa hatuna ushahidi wa takwimu?..

Muda wote mlotumia hapa kubishana unadhirisha wazi kwamba kila mmoja wenu anabuni numbers tena kwa kunukuu vitu vilivyoandikwa over 50 years ago, hii kweli akili?...Kama tungekuwa na takwimu tungeuweka mjadala huu ktk hali tofauti kabisa wala hakuna ugonvi isipokuwa tungecheza na takwimu zilizopo, ushahidi na hata kukubaliana wapi tunafanya makosa. Iwe Waislaam wengi au Wakristu wengi hii sio hoja wala msingi wa kufanya sensa ya WATU isipokuwa kujua what U have in your pocket iwe dime, quarter, nickel, penny or lonnie it all counts to something.

....................
Iweje Waislaam waitake sensa yenye kipengele cha dini lakini wakristu hawaitaki wakati huo huo wakisema Waislaam hawakusoma, hawataki kusoma na kadhalika, Mara JK anafanya Udini wakati ktk hili mnamtetea Maneno haya tumeyasikia sana wakati wa mkoloni na tunaona dejavu ikijirudia miaka 50 baada ya Uhuru..We wonna know how many of our kids are in schools controlled by the church..Why not!

Kaka Mkandara,

Wewe nawe upo upande ule ule.

Mimi ninajua sana kutumia muda wangu na wala siwezi kuupoteza kwa kujadili mambo ya dini. Niliweka post moja tu, na wewe ndiwe ukaishupalia. Post yangu ilikuwa inatumia information retrievable kujibu maelezo ya mtoa mada kuhusu kupungua kwa waislamu, nikasema kuwa huenda siyo kupungua kwa waislamu bali ni kuongeza kwa wasilamu kutokana na trend zilzokwisha onekana muda mrefu tangu mwaka 1931. The lwa of trends na historical facts ni toos za kutosha kujibu swali na mtoa mada. Ufutwaji wa matumizi ya dini pia siyo kweli kuwa ilikuwa ni kuficha takwimu bali ni jambo lililotokana na mazingiya ya wakati huo ambapo Nyerere alikuwa anataka watu wote wawe na haki sawa mbele ya huduma za jamii bila kujali dini zao; na akataifisha taasisi zote za dini. Yote hayo yalitokea mwaka huo huo 1967. Kwa hiyo analytically inaonyesha kuwa madai ya mtoa mada huenda siyo kweli kama alivyoweka yeye.

Una haki ya kukubali analysis yangu au kuikataa, lakini usinone kuwa sina la kufanya kuwa nimetumia muda mwingi kwenye thread hii kubuni namba wakati nimeweka quote unayoweza kuipata kutoka maktaba. Mtoa mada alikaribisha michango yenye maana siyo ya kushambuliana kama unavyonifanyia.

Kudai kuwa waislamu wanataka dini ihesabaiwe kwenye sena na wakristo hawataki ni generalization mbaya sana ambayo mtu mwenye akili kama wewe hatakiwi kuitoa. Siyo kweli kuwa waislamu wote wanataka dini ihesabiwa na wala siyo kuwa ni wakristu tu wanaopinga hilo. Generalization za namna hiyo huwa zinasababisha tafsri nyingine ambazo baadaye zinasababisha vurugu. Kikwete aliyepinga kipengele cha pia ni mwislamu tena mwenye power ya kuamua lolote nchini. Hujakagua wakristo wote kujua kama kweli wao hawataki dini zao zisihesabiwe; elewa kuwa watu wa type ya akina Ponda wako katika dini zote.

Mwishoni tena swala linarudi kule kule; serikali ihesabu watu na dini zao ili iweje? lengo la takwimu ni katika kupanga mipango ya maendeleo ya nchi, je ni mapango ipi ya maendeleo itakayotokana na kujua dini za watu? Katika jamii fragile kama za kwetu, mambo yanayotenganisha watu yanatakiwa yaondolewe vichwani mwa watu: ukabila na udini ni vitu ambavyo tusingekuwa tunavipiguia kelele namna hii.

Leo hii kwa vile shule za dini zimesharudi miongoni mwetu; kila dini ina haki ya kuanzisha shule zake, na kila mzazi ana haki ya kuchagua ampeleke mtoto wake shule ipi. Iwapo mzazi akiamua kumpeleka mtoto wake katika shule ya kanisa, serikali itahusikaje kuwashabu watoto hao? Unless swali lako lina maana nyingine

Sidhani kama mtoa mada alikuwa anataka thread yake iende hivi kwani nilipoisoma nilikuwa nimeona kuwa ilikuja na facts zinazo-deserve discussion, ndiyo maana nikachangia kipande kilichokuudhi hapo juu. Alimalizia post yake hivi

"Sisi ni great thinkers tujadili niliyoyaleta jamvini kwa hoja na tafakuri jadidi."

Maandiko yako hayaonyeshi kujadili aliyoleta hapa janvini.
 
Mkuu Mkandara,

Nimekusoma hapo juu na kukuelewa vema tu ingawa umeondoka katika nyuzi yako iliyopita ambayo niliikubali kabisa.
Nyuzi ile ulizungumzia kuwa sensa itumike katika kupanga maendeleo ya taifa na si vinginevyo.

Kipengele cha dini katika sensa sina tatizo nacho kwani ni sehemu ya 'dermograph' ya taifa.
Baada ya kusema hivyo narudi kwenye msimamo wangu wa kila mara kuwa jambo lolote linaloashiria kuvunja umoja wa kitaifa sikubalini nalo.

Mimi kama wewe naamini kuwa wakoloni wote waliofika nchini walitugawa kwa makundi hata kama walikuwa na thamani walizokuja. Ni matokeo hayo ndiyo yanatufanya tusiongelee utaifa na kubaki kuongelea katika imani kitu kinachopswa kuwa cha mtu binafsi.

Kabla sijajenga hoja yangu naomba kusema kuwa haki ni kitu kimoja na kupigania haki ni kitu kingine, na jinsi ya kupigania haki ni kitu kingine. Unaweza kuwa na haki lakini kama hujui haki ipo wapi na jinsi ya kuipata basi utajikuta huna haki. Ndiyo maana hata kama mtu anajua ana haki bado atamweka mtu mweledi (lawyer) kusimamia hiyo haki.
Ni ngumu lakini nitaeleweka kadri ninavyosonga mbele.

Natambua kuwa kuzuia kipengele cha dini si kuogopa kuweka wazi kisichojulikana. Ni jitihada za kuzuia mitafaraku inayoweza kutokea kutokana na baadhi ya watu kutumia mwanya huo kujenga hoja za uzushi, uongo na fitna.
Ni kutokana na watu kupinda ukweli kwa kutumia data.

Tatizo la Waislam ni mchanganyiko wa mambo kadhaa. Nasema tatizo la waislam kwa kuzingatia malalamiko ya hoja zao
Kwanza, Waislam hawatafuti chazo cha matatizo yanayowakabili.
Pili, hawakubali ukweli wa chanzo cha matatizo.
Tatu, wanatafuta njia za mkato kutatua matatizo yao.
Nne, hawakubali kuwa tatizo lipo miongoni mwao na usuluhishi upo miongoni mwao na wanaamini kuwa kutafuta suluhu ya bandia ni njia muafaka.
Tano, Wameachia agenda za issue zao kwa mashabiki na sio watu wenye weledi.

Nina uhakika umesoma maandiko mengi ya waandishi wa kiislam akiwemo Mzee Mohamed Said. Ms kwa mfano, amejenga hoja mara nyingi sana kuonyesha wingi wa waislam ingawa hakuna anayehoji wapi alipata data. Mwaka jana ametoa data hizo hizo katika makongamano hata kama ilikuwa za mwaka 1957, si kwasababu ya kujenga hoja bali kujenga hoja kwa kusaidiwa na wingi wa watu. Mara nyingi sana hoja zake hupoteza mashiko kwasababu hazisimami zenyewe zinasimama kwa kutegemea kitu kingine.

MS anaposema waislam kwa sensa ni wengi na ndio wameachwa nyuma kieleimu na madaraka, hapa anaongelea Quantity. Asichoongelea ni Quality. Ndio maana Mohamed Sosshi hapo juu nimemuuliza, aliposema waislam wengi waliandikisha watoto baada ya uhuru lakini bado wamebaki nyuma licha ya wingi wao,je hao wengi walimaliza shule? walifaulu? walirudi kuisadia jamii yao? Hakuwa na jibu.

Pengine kwa kutumia dhana ya MS yeye anaamini kuwa unaweza kuwa na waziri kwasababu umeandikisha watoto shule hata kama hawajamaliza au kufaulu. Nimetoa mfano wa Kilwa, nikauliza shule inapofungwa kwa kukosa wanafunzi unategemea lini utapata mwalimu, bwana shamba au mhasibu miaka 10 ijayo? Sikupata jibu kwasababu ninaongelea source na nilipaswa niongelee matokeo!!

Hoja ya sensa inaposhikwa na akina Ponda kwa msaada wa wasomi washabiki wengine inapoteza nguvu kwasababu haijengwi katika mantiki zaidi ya ushabiki na uchochezi usio na weledi.

Wanapojenga hoja kuwa tunataka tujue idadi ili tuone uwezekano wa kujiunga na OIC kwasababu ya wingi, ni kosa.
Hivi waislam wakiwa 50% wakristo 30% na wapagani na wasioamini 20% hiyo inatosha kushawishi umma kuwa sasa ni wakati wa kujiunga na OIC?

Wanapojenga hoja kuwa maeneo yaliyo na waislam yameachwa nyuma makusudi, akatokea mtu na kueleza shule zilivyo na matatizo ya kukosa wanafunzi Kilwa, je, hoja hapo inasimama?

Wanapojenga hoja kuwa hakuna mkuu wa NECTA tangu uhuru, akatokea mtu na kuonyesha shule yenye watoto 250 na mwalimu mmoja, je, hoja ina mashiko hapo.
Tatizo ni mkuu wa NECTA au wanafunzi 250 wasiosoma na kufaulu?

Kama watu watajenga hoja za kisayansi zinazoonyesha umuhimu wa kipengele cha dini nadhani kila dini watakubaliana na hilo. Hoja hizo zinapojengwa kwasababu rahisi na za kishabiki zinapoteza nguvu yake. Hapo ndipo tatizo lilipo.
Kwanini mtu alenge data za wakristo na asije nazake kuonyesha mbadala! Kwanini mtu aseme wakristo ni kadha asitaje wapagani ambao ni wengi sana kuliko wakristo na waislam. Narudia wapagani na waisoamini ni wengi sana kuliko waislam na wakristo. Atakayetaka ufafanuzi aniulize!

Nimalizie kwa kusema, Ponda na masheikh kama Halifa na akina Mohamed Said wamekuwa wakimlaani sana Nyerere kwa mambo kama ya kuondoa sensa. Hatujasikia wakisema Kikwete bali wanakwepa kwa kutumia serikali.
Ni hawa wanaosema CCM inaongoza vema, na ni hao hao walisema CCM imewakandamiza waislam kwa kutumia TANU na yenyewe mwaka 2000 na 1995. Na ndio hao hao wanaongoza zoezi la kususia sensa.

Narudi kwenye nukta zangu za awali kuwa kuna tatizo, suluhu si kutafuta mchawi au njia za mkato ni kulikabili tatizo kuanzaia chanzo. Nitue hapa kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Kaka Mkandara,

Wewe nawe upo upande ule ule.

Mimi ninajua sana kutumia muda wangu na wala siwezi kuupoteza kwa kujadili mambo ya dini. Niliweka post moja tu, na wewe ndiwe ukaishupalia. Post yangu ilikuwa inatumia information retrievable kujibu maelezo ya mtoa mada kuhusu kupungua kwa waislamu, nikasema kuwa huenda siyo kupungua kwa waislamu bali ni kuongeza kwa wasilamu kutokana na trend zilzokwisha onekana muda mrefu tangu mwaka 1931. The lwa of trends na historical facts ni toos za kutosha kujibu swali na mtoa mada. Ufutwaji wa matumizi ya dini pia siyo kweli kuwa ilikuwa ni kuficha takwimu bali ni jambo lililotokana na mazingiya ya wakati huo ambapo Nyerere alikuwa anataka watu wote wawe na haki sawa mbele ya huduma za jamii bila kujali dini zao; na akataifisha taasisi zote za dini. Yote hayo yalitokea mwaka huo huo 1967. Kwa hiyo analytically inaonyesha kuwa madai ya mtoa mada huenda siyo kweli kama alivyoweka yeye.

Una haki ya kukubali analysis yangu au kuikataa, lakini usinone kuwa sina la kufanya kuwa nimetumia muda mwingi kwenye thread hii kubuni namba wakati nimeweka quote unayoweza kuipata kutoka maktaba. Mtoa mada alikaribisha michango yenye maana siyo ya kushambuliana kama unavyonifanyia.

Kudai kuwa waislamu wanataka dini ihesabaiwe kwenye sena na wakristo hawataki ni generalization mbaya sana ambayo mtu mwenye akili kama wewe hatakiwi kuitoa. Siyo kweli kuwa waislamu wote wanataka dini ihesabiwa na wala siyo kuwa ni wakristu tu wanaopinga hilo. Generalization za namna hiyo huwa zinasababisha tafsri nyingine ambazo baadaye zinasababisha vurugu. Kikwete aliyepinga kipengele cha pia ni mwislamu tena mwenye power ya kuamua lolote nchini. Hujakagua wakristo wote kujua kama kweli wao hawataki dini zao zisihesabiwe; elewa kuwa watu wa type ya akina Ponda wako katika dini zote.

Mwishoni tena swala linarudi kule kule; serikali ihesabu watu na dini zao ili iweje? lengo la takwimu ni katika kupanga mipango ya maendeleo ya nchi, je ni mapango ipi ya maendeleo itakayotokana na kujua dini za watu? Katika jamii fragile kama za kwetu, mambo yanayotenganisha watu yanatakiwa yaondolewe vichwani mwa watu: ukabila na udini ni vitu ambavyo tusingekuwa tunavipiguia kelele namna hii.

Leo hii kwa vile shule za dini zimesharudi miongoni mwetu; kila dini ina haki ya kuanzisha shule zake, na kila mzazi ana haki ya kuchagua ampeleke mtoto wake shule ipi. Iwapo mzazi akiamua kumpeleka mtoto wake katika shule ya kanisa, serikali itahusikaje kuwashabu watoto hao? Unless swali lako lina maana nyingine

Sidhani kama mtoa mada alikuwa anataka thread yake iende hivi kwani nilipoisoma nilikuwa nimeona kuwa ilikuja na facts zinazo-deserve discussion, ndiyo maana nikachangia kipande kilichokuudhi hapo juu. Alimalizia post yake hivi

"Sisi ni great thinkers tujadili niliyoyaleta jamvini kwa hoja na tafakuri jadidi."

Maandiko yako hayaonyeshi kujadili aliyoleta hapa janvini.
Kichuguu,
mkuu wangu nilikuaminia sana ktk maswala haya lakini nashangaa ulipokwenda. Ni wewe uloniuliza mimi swali ya kuwa serikali ikisha jua ili iweje? Na kama kawaida yangu huwa sikimbii swali. Hujibu swali na kuelezea zaidi mtazamo wangu ktk hali halisi ya hoja nzima kwa maana ya kutotaka kurudia rudia maswali na majibu. Hivyo hueleza kila nachokiamini ama kukifahamu ili upate picha kamili..Nilichofanya mimi ni kuelezea umuhimu wa sensa na kuwa na vipengele vyote ndani ya mfumo huu wa utawala usio tofautiana na ule wa Mkoloni. Unaweza kuutumia kuwakandamiza watu ama unaweza mkutumia kuweka usawa baina ya jamii, hivyo kuwa na takwimu kamili ni muhimu sana.

Sijasema mahala popote kwamba Nyerere alifanya hvyo kuficha kitu isipokuwa Nyerere aliondoa kipengele cha dini kwa sababu aliukataa mfumo mzima wa kikoloni, kisha mfumo wake wa Ujamaa na Kujitegemea ulichukua jukumu la serikali kupeleka maendeleo kwa wananchi wote pasipo kujali dini zao, rangi zao ama makabila yao. Nyerere hakutumia mfumo wa kikoloni akakpinga kipengele cha Udini isipokuwa alipinga kwanza mfumo wa kikoloni na kuweka vizingizi kuudhibiti mfumo huo ili kuleta usawa katika jamii yetu. Na ndio maana alitaifisha shule na Hospital zote za kidini ama kikabila ikabakia private schools zenye kumilikiwa na watu binafsi tu, sisi wote tukaitwa Wanzania, wajamaa lakini hilo halipo tena leo.. kwa nini mnashindwa kuelewa hili...

na nimekueleza vizuri jinsi mfumo uloasisiwa mwaka 1992 ulivyoturudisha ktk Utawala wa kikoloni na kuacha maswala muhimu kaa ELIMU na AFYA kuwa majukumu ya wananchi wenyewe.. Sasa Ikiwa ndivyo hivyo kuna kila sababu ya Waislaam kutaka kipengele cha dini kiwekwe maana tumerudisha mfumo wa kikoloni ktk utawala na athari zake tunazijua. KUJUANA lazima kutakuwepo hata kama mtajitetea vipi na nakuhakikishia kwamba haya mambo yanafanyika..

Kikwete ni Mnafiki mwingine hivyo kuwa yeye Muislaam haina maana atawajali waislaam. kwani Kikwete sio Mtanzania mbona anawaachia mafisadi wakiiba maliasili zetu? Kina Mkapa na Chenge wanaoiba na kuficha wafedha Uswiss hawa sio watanzania? kwa hiyo nashindwa kuwaelewa wenzangu mnapotumia jina la mtu kw Uislaam wake au Ukirstu wake kuwa kielelezo cha matendo yake.. hapana nachosema mimi ni mfumo uliopo, ni system nzima ya utawala inawakumbatia watu gani.. Hivyo tunaweza kukesha hapa JF kama nitaamua kuwatetea Mafisadi lakini haina maana hawa watu wanathamini ama wana Uzalendo kwa sababu ni Watanzania.

Sensa ni lazima iwe na vipengele vyote ikiwa tunatumia mfumo huu wa kikoloni ambao elimu inaongozwa na kanisa kama ilivyokuwa kabla ya Uhuru na Waiuslaam wana historia kubwa ya utawala ule. Huwezi kuepuka hili unless turudi ktk mfumo wa Nyerere ambao serikali ilichukua jukumu hilo ndipo tunaweza tena kukataa tofauti zetu na kudai UJAMAA.. TOGETHER we stand by inclusive na sio exclusive..hapo lazima utaweka utata.

Nguruvi3,
Mkuu wangu hakuna record yoyote diuniani ilioonyesha sensa ilokuwa na kipengele cha dini imesababisha vurugu ama utengano. Leo hii mimi hapa naelewa vizuri Kichuguu au Mwanakijiji ni mkristu na kutokana na kuelewa huko tumejenga hekima na fursa ya kutambua haki na usawa baina yetu. Tumeweza kujua mipaka ya mazungumzo baina yetu, tunajua hata kesho nikiwakaribisha nyumbani au wao wataandaa nini kwa ajili yangu ama yao.

Ni kutambua mwenzako na kumkubali alivyo ndio hukuza UMOJA wetu kuliko kutojua ama kukataa kujua. sensa hii ni sawa na kufagia chumba ukaficha uchafu uvunguni.. Itakuja kula kwetu na nawahakikihshia itafika wakati mtayakumbuka maneno yangu maana Udini huanza kwa maneno kisha itafika siku uchafu ulofichwa uvunguni utajulikana.. Hapo ndipo hatutakuwa na simile tena. na wala sikushangai wewe ama Kichuguu kwa sababu mara zote ninaposema mimi watu wengi huwa hawanielewi hadi siku jambo linapotokea ndipo hujirudi na kusema Mkandara aliwa kusema haya.. Kwa leo hutanifahamu lakini, Inshallah ipo siku utayakumbuka maneno yangu..
 
Kaka Mkandara;

Ninajua sana ubishi wa dini huwa unazidi kutenganisha watu na ndiyo maana mara yangu ya msiwhso kujadili mambo ya kidini hapa ilikuwa mwaka 2006 ningali mgeni sana. Sikuwa nimeweka post yangu ya kwanza kama kujadili dini, bali nilikuwa najadili swali la msingi kuhusu takwimu zilizoletwa na mleta mada.

Kwa sasa hivi nashauri tusiendelee na mjadala kwa upande huo wa kutaka kulinganisha waislam na wakristo. Mambo ya hiyo huwa hayana majibu wala suluhu kwa sababu kila upande hutaka kuwa mshindi; ndiyo maana nikauliza tena serikali kujua idadi ya waislamu itasidia nini.
 
Mkuu Mkandara,
Kama umenisoma vizuri hakuna mahali niliposema sensa huleta vurugu. Nilichosema ni kuwa kuna viashiria kuwa sensa yetu na shinikizo la kipengele cha dini hailengi kutafuta kile kilichokusudiwa bali kitu kingine.

Nimesema na narudia sioni tatizo la kipengele cha dini, tatizo ninaloliona ni la agenda hiyo kushindwa kuelezeka kitaaluma na kwa mantiki.Fikiria mtu anapokuja na hoja kuwa sisi ni wengi na tunaonewa hapo ipo heri au shari. Tumekosa elimu licha ya wingi wetu, hatuna madaktari wengi kwasababu tunakandamizwa n.k.

Hoja yangu ni kuwa ni lazima kuwe na watu wanaoweza kujenga hoja kwa mantiki na sio wanaoweza kuongea ongea bila mpangilio au mantiki.

Nitakupa mfano mmoja niliowahi kuuongelea hapa. Kipengele cha Kadhi mkuu kilikuwepo kuanzia zama za mkoloni.
Baada ya hapo hakikutumika tena. Nasema hakikutumika kwasababu bado kipo katika taratibu kama ilivyokuwa wakati wa mkoloni.

Kwasababu tu watu wenye agenda hii hawana mpangilio wa kujenga hoja, kila mara hoja zao zimeonekana kama kutafuta shari. Huwezi kusema mahakama ya kadhi inazuiwa na watu wa dini fulani wakati mtu huyo hajui kama kitu hicho kipo au hakipo. Kwa vile watu wanaongozwa na jazba zinazotokana na kukosa weledi basi kila mtu amebaki kudai mahakama ya kadhi. Unadai vipi kitu kilichopo?

Juzi tumesoma katika magazeti malumbano kuwa walioteuliwa kuwa makadhi utaratibu haukufuatwa.
Unaona mkuu hapa jinsi watu walivyojichanganya! utaratibu upi wakati utaratibu upo kuanzia wakati wa mkoloni?
Hii ni kwasababu hoja hazijengwi na kuelezeka, zinajengwa kwa ushabiki tu. Hakuna tafiti kilichobaki ni mbona fulani hana hiki fulani ana kile.

Mkandara, hivi unaamini kuwa ipo haja ya kudai mahakama ya kadhi ili hali mahakama ya kadhi ipo!
Watu hawajui kwamba ipo wanadai nyingine na tayari wameshapata makadhi wapya.
Endapo kungekuwa na utaratibu wa tafiti hakukuwa na haja ya kudai mahakama ya kadhi iliyopo tayari.

Mimi ningeelewa kama yupo ambaye angesema, tuna tatizo nchini na ili kutatua tatizo hilo lazima twende deep.
Kuna maeneo yana umasikini kuliko mengine, kuna maeneo yana ujinga kuliko mengine na kuna maeneo yana maradhi kuliko mengine. Tunahitaji wataalamu wasaidiae kubaini tatizo ni nini?

Na kwa vile tunamchanganyiko wa factors lazima tuanze ku-eliminate moja baada ya nyingine.
Sensa ni kitu kinachoweza kutupa mwanga wakati tunatafuta suluhu ya Epidemiology, illiterate na poverty na ni muhimu tuwe na qualitative na quantitave data.
Sensa inapaswa iwe na vifungu kama kabila, dini, umri, jinsia n.k ili tuweze kwenda kwenye tatizo na kuacha ku-duplicate kazi.

Lakini mtu anapoibuka redioni na kuanza tumekandamizwa tunataka kipengele cha dini, tunataka madaraka n.k ana dilute maana nzima ya hoja yake, anaonekana kuligawa taifa na ni ngumu kueleweka.
Nani amesema kuwa umasikini wa Ninjilinji ni tofauti na ule wa Kinesi musoma!
Nani anasema umasikini wa Mtimbira ni tofauti na ule wa Kwedikwazu au nyumbani Mkuzi
 
@Nguruvi3, Kama ungekuwa Muislaam ungeelewa jinsi system hii inavyowakandamiza. Nitarudia kusema mfumo uliopo nchini ndio unaojenga Udini sio swala la Muislaam kuulizwa msingi wa kuweka kipengele hicho akiwa katika hasira.. Mahakama ya kadhi ipo kivipi? na ni utaratibu gani wa kumchagua Kadhi ulikuwepo toka mkoloni maana hata sielewi kama unajua Kadhi huchaguliwa vipi kulingana na misingi ya kiislaam na sio ya mkoloni.

Labda nikuulize wewe na wengine wote wanaosema kuna Kitu Utanzania ama jamii moja ya Watanzania.. Inakuwaje waislaam wanapolalamikia muafaka wa MoU wanaambiwa na NYIE ombeni mtapewa mahala ambapo sheria ya katiba imekiukwa?..Sasa Waislaam nao waombe kama kina nani? Je wanatazamwa kama Watanzania au Waislaam!. Hii ni kila mahala wanapodai usawa. Nachokataa mimi ni kuficha uchafu, hii tabia ya kufagia uchafu na kuuficha uvunguni ili tusionekane nje kwa kuhofia Udini wakati tunaujenga kwa chuki. Mnapoitazama mahakama ya Kadhi mnasema mbona sisi WAKRISTU tunafanya hivi ama vile kwa nia ya kwamba Waislaam nao wafuate mfano wao wakati hizi ni traditional za Wakatoliki na sii za Muislaam au MLutheri. Hivyo mila zao are accepted lakini sio za wengine zitatuletea vurugu, halafu tunadai Utanzania wenye Diversity..Nisingependa kwenda deep maana nitatoka nje kama alivyosema Kichuguu..

Tazama leo CCM wanajiona wao kundi jingine la Utanzania, Chadema vile vile, CUF kwa upande wake kinajiengua kama chama cha Wazanzibar, Na kila mmoja wetu anaidai haki kuwa yeye ndiye msimamozi wa jumuiya ama Watanzania.. Who are we really?..Kwa nini wewe kama Mtanzania usikubaliane na mtanzania mwenzako who happened to be Muislaam anayeiomba serikali na sio kanisa au wakristu kuweka kipengele cha dini halafu wanaotoa majibu kwa niaba ya serikali ni wakristu hivyo hoja nzima ya kuwepo kipengele hicho inasomeka kama hoja ya WAISLAAM na sio Watanzania. Maandamano ya Arusha, Dodoma na Iringa yanaitwa ya Chadema japokuwa waliohudhuria ni Watanzania wengi wao hawana hata kadi za Chadema lakini maadam wameafiki ya Chadema basi hawa sii upande wetu. Why can't we just listen to them and solve our problems..Tutaendelea kuficha achafu huu hadi lini?
 
Mkuu Mkandara,
Niliposema kipengele cha kadhi kipo na utaratibu wa kumpata upo nilijua kuwa swali litafuta.
Mkoloni alipoweka mahakama ya kadhi alishauriana na waislam na wao wakatengeneza utaratibu wao wa kumpata kadhi.
Hakuna hata siku moja utasikia malalamiko kuwa kadhi alitumia taratibu za wakoloni.
Kilichofanyika ilikuwa kutambua uwepo wake na kutambua huduma zake kisheria.

Mkandara, unafahamu kuwa baada ya uhuru kuna sheria zilitungwa za Tanganyika na zingine zakarithiwa kutoka kwa wakoloni. Mfano sheria ya miji inayohusu usumbufu ikiwemo kelele, Baa n.k. zimerithiwa.

Mkuu, labda unionyeshe sheria iliyoondoa uwepo wa kadhi. Tunafahamu kuwa sheria haifutiki hadi pale inapokuwepo nyingine ya kuifuta. Sasa nifafanulie (pengine kwa mimi kutoelewa), ni sheria gani ya mwaka gani ilizuia kutambuliwa na uwepo wa Kadhi Tanzania.

Baada ya hilo,niseme kuwa sioni tatizo watu wakieleza concern zao.
Kama unanielewa, tatizo ni pale hizo concern wanapokabidhiwa watu waisojua kuzieleza.
Mara nyingi huharibu hoja kwasababu mtu anadhani kuwa kutanguliza ushabiki ndiko kunasimamisha hoja.

Umetoa mfano wa MoU ya serikali na wakristo. Kauli hiyo tu inaweza kuwa na mapungufu kwasababu tayari imeshalenga eneo na si tatizo. Ukweli ni kuwa kuna MoU na Agakhana Foundation na mwaka huu wamesaini kitu kingine kinachofanana na hicho. Mimi nilidhani hoja ilikuwa kwanini wenzetu ABC wana MoU ambayo inakiuka katiba na kama sivyo iweje isiguse imani nyingine.

Sikiliza redio na soma magazeti, utaona hoja kabla haijajengwa itatafutiwa namna ya Kumtaja Nyerere halafu ukatoliki, siyo ukristo, ni ukatoliki kisha hoja inafuata.
Kama kuna kipengele kinakiuka katiba kiwekwa wazi kwa kuiangalia katiba,siyo kutanguliza kundi fulani badala ya makundi yanayohusika kama Agakhan.

Hoja ya kuwa waislam wanataka ruzuku za kuendesha mahakama za kadhi kwasababu wapo wanaopewa ruzuku kwa kuendesha shule na mahospitali inaweza kuwa na nguvu ikijengwa katika ukweli usiotanguliza chuki, jazba n.k.
Mfano, kama waislam watasema tunaomba ruzuku ili kuhudumia huduma za jamii kama ilivyo huduma nyingine kuna msingi wa hoja, siyo kwamba wale wanapata ruzuku na sisi!

Mfano wa pili, Zbar wameanzisha baraza la mitihani kwa sababu watoto wao 'wamefelishwa' kisa ni waislam.
Hakuna data za kisayansi bali tu hisia. Inaweza kabisa kuwa hilo ni kweli lakini hakuna aliyeshughulisha akili kufikiri kuwa ni kweli mitihani inaibiwa, je, ni kweli watoto wameiba? Ni kwanini mwaka huu tu? Wangefanya tafiti kwa watoto wale wale kwa kuwapa mitihani inayolingana na ilewaliofeli ili kuwa na ushahidi kwanza, halafu waende mbele zaidi kutafuta chanzo.

Si mara mojau mbili shule zimefutiwa matokeo. Ninayo mifano zaidi ya 100. Hata watahiniwa waliofutiwa wapo akiwemo January. Ilitakiwa ithibike na si kudhani kuwa uwepo wa Baraza la mitihani Zbar ndio suluhu. Wataiba tena mitihani, kufaulu na wakienda vyuo vya juu ni disco, tunarudi kule kule wanaonewa.
Hoja hapa ni kuwa uonevu unaweza kuwepo au la, tatizo ni kuwa badala ya kujenga hoja Uislam ndio umetangulizwa kulinda hoja.

My main point is, hoja za waislam zimekabidhiwa watu wasio na weledi pengine kwa vile tu wanasauti nene na kubwa.
Kwa mantiki hiyo hoja inaweza kuwa na nguvu sana, tatizo anayeiwakilisha anajenga hofu hata kabla ya hoja kuangaliwa.

Mtu hawezi kunishawaishi kuwa uwepo wa mkuu wa NECTA mwislam utaondoa tatizo la watoto wa Kilwa kukimbia shule.
Badala ya ku address real problems and analyze the data methodically and scientifically washabiki wanakimbilia maandamano. Wakifika kule hawawezi kutetea hoja zao hata kama ni nzito kiasi gani.

Mimi sikatai uwepo wa concern au umuhimu wa kuzieleza na kuzishughulikia, ninachokataa ni ushabiki, na watu wasiojua lolote kuwa ndio viongozi wa hoja nzito. Ninajua wapo waislam wenye uwezo sana wa kuenga kutetea na kuanisha hoja, bahati mbaya hoja zimetekwa na kikundi au vikundi vya watu wanaoishi mjini kiujanja ujanja.

Huwezi kuniambia Sheikh aliyeiona CCM mbaya kwa miaka 40, leo anasema ni nzuri sana. Akirudi upande wapili anasema Nyerere mbaya sana, kesho anasema serikali mbaya na si Kikwete. Ili mradi tu wajanja hawa wanaishi.
Huwasikii kwenda Kilwa kuangalia tatizo la elimu, utawasikia Zbar wakielezea umuhimu wa Zbar!
 
Naunga mkono hoja ya Nguruvi kwamba inawezekana waislam wana hoja nzuri na nzito-tatizo ni namna na watu wanaoziwasilisha. Hoja yoyote ikitangulizwa na vitisho inapoteza maana. Mfano, Mkandara anaoonesha umuhimu wa sensa kwa kurejea mfumo wa Ujamaa na Ubepari inaleta maana, lakin sensa ikiongelewa kama kigezo cha kujiunga na IOC, pamoja na supremacy za dini, inakuwa inaletwa shida kidogo kwa watu wengine. Some of us are worried of what is up the sleeve..
 
Mohammed Shosi, Naungana mkono na wewe kuhoji usahihi wa volatity ya idadi ya waislamu katika sensa ya mwaka 1967, hata mimi hainiingii akilini.

Na pia hainiingii akilini ni kwa nini kipengele cha dini ya mtu kiondolewe kwenye zoezi la sensa?

Lakini pia hainiingii akilini ni kwanini vyombo vinavyosimamia imani ya kiislamu havielewi idadi ya waamini wake?

Na pia ni kwanini waislamu wang'ang'anie kipengele hiki kiwepo huku ikijua kwamba huko nyuma serikali hii hii ilitoa takwimu ambazo wao hawakubaliani nazo? ni nini kinawafanya waiamini serikali sasa?

Lakini pia, sioni tatizo la serikali kukiondoa kipengele hicho kama inajua hawakihitaji kwenye matumizi yoyote yale ya takwimu hizo.
 
Mkuu wangu Mohammed Shossi nilikuomba source ya sensa ya mwaka 1957 na 1967 mpaka leo umeshindwa kuzitoa au na wewe nikuite mvivu ?.Msingi wa mjadala huu ungenoga sana iwapo ungezileta hizo data hapa jamvini ili tujadili kitu chenye mashiko badala ya kujadili hisia za kina sheikh Ponda na Mohamed Said.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu kwanza samahani sikuweza kupitia hapa kwa muda..Na bahati iliyoje nimepitia hapa na kukuta kumbe ulinitupia maswali na sikuyaona. safari nyingine nadhani jaribu ku quote jina ili nipate kujua jkuna ujumbe.

jambo muhimu la kuzingatia hapa ni KUHITILAFIANA kunakubalia na ni sehemu ya kujifunza. na husababishwa na mambo mengi sana yakiwemo upeo wa kufahamu, kupenda, matamanio ya nafsi, mielekeo ya kifikra, kiimani, Ustaarabu, kuiga, ubwana, Falsafa, Itikadi na mengineyo mengi chungu nzima. Hivyo wenye kuhitilafiana tunaweza kabisa kusikilizana na kuelewana ikiwa hapana CHUKI baina yetu.

Chuki inapoingia tunavunja mawasialiano inakuwa hakuna tena kusikilizana wala kufamaniana. Chuki huondoa mapenzi na kuvunja uhusiano mwema na kuzaa kero, bughudha na hata ukifungua mdomo tu watu wanachukia hata sauti yako.. Hii ndio tatizo la chuki na mara nyingi chuki ktk hitilafu za masilikizano huwa na dalili za maswali na majibu ya Ubishi na jeuri. Ukiona hayo tu ujue tayari chuki imeshaingia vichwani kwa wahusika. Nashukuru Mungu toka nianze kujadilaian a wewe tumekuwa na mawasilano mazuri sana na tumejifunza toka kwa kila mmoja wetu. Hilo namshukuru Mola taala kwa kutujalia uvumilivu.
Haya Bismillah nakujibu hoja zako hapa chini.
 
Kwanza nianze na Kadhi, huyu ni hakimu wa maswala ya dini infact cheo hiki kiliondolewa tu baada ya UHURU hivyo ktk utunzi wa katiba wakijaribu ku reunify sheria zetu ili kukidhi mahitaji yetu wote irrespective of our religious inclinations. Kwa hiyo ktk sheria zilizoondolewa ni pamoja na mahakama ya kadhi. Sasa sielewi ulitaka kadhi awepo vipi ikiwa hakuna mahakama ya kadhi wakati unification process ndio ilotuleta Law of Marriage Act ya mwaka 1971 na toka hapo mahamaka za kesi za madai ndio zilipokea kesi hizi.

2. Swala la MoU mkuu wangu unashindwa kuelewa nachozungumzia hapa. AghaKhan ni foundation ya mtu ambaye anaingia nchini kama NGo nyingine zote. In fact zipo NGos kibao za watu na madhehebu mbalimbali ambazo zinafuata sheria za serikali kulingana na katiba. hakuna haa moja iloingia Muafaka na serikali maana muafaka You become partner kama walivyofanya CCM na CUF au Chadema na CUF hivyo muafaka haufungwi na sheria ya serikali bali makubaliano ya partnership..

Hapa ndipo tunapoliona tatizo na nitarudia kusema muafaka wowote baina ya serikali na hata Bakwata sintokubaliana nao kwa sababu zozote zitakazo tolewa. Katiba inasema nchi yetu haina dini hivyo kushirikiana kw aserikali na dini kama milivyokuwa wakati wa mkoloni tunajua madhara yake.

Sikatai kwamba matumizi ya hili neno 'mfumo kristu' huwagusa sana waumini wa Kikristu lakini ndivyo navyoweza kusema kuhusu matumizi ya neno 'Sharia law'. japokuwa neno hilo huwagusa waislaam na tupo wengine wengi tu hatukubaliani na Sharia Law, hivyo kinachotakiwa ni kutoka ktk sanduku la kiimani na kulitazama swala hili nje ya box hilo..

Binafsi yangu nisiwe mjinga zaid nadhani wakristu wangefurahia zaidi Christian values ambazo zinaambatana na dini kutoa uduma ya Elimu na Afya wakati waislaam kazi ya dini ni kufundisha tu the Gospel yaani kuna separation of Church and state. Hapa ndipo mnapotupiga bao kidini maana sisi tunaitegema serikali wakait nyie hakmuoni kosa kwa kanisa kuchukua dhamana ya elimu na Afya. Pia huwashangaa waislaa wanapiga makelele inapozungumziwa Sharia law badala ya kujivunia na wakatueleza uzuri wake.. anyway I might be very wrong on this, ni mtzamamo wangu tu.

3. Kuhusu ruzuku mkuu wangu ni trahisi kwanza kukubali hata hao waliopewa wamechukua kwa nia ile ile unayoiweka kwa waislaam. haiwezekani mtu akiomba mahakama ya kadhi iwe anaitaka ruzuku lakini yule aliyepo ktk muafakla tayari tunawatungia sababu na sio ruzuku. Kama kweli ni aya CSSC ni kutoa huduma basi hawana sababu ya kuchukua ruzuku. tena wao kwa nchi zote fedha zinatoka Vatican na ukitaka kusoma itakugharimu.

Hapa Canada mtoto hawezi kwenda kusoma shule ya Kikatoliki (private school)) unless mmoja wa wazazi wake ni mkristu na wananchi walipa kodi hawana tatizo na hilo maana fedha inatoka mifukoni mwao na wanaweza fanya watakavyo.. Ulkilalamika utaambiwa hujakatazwa na wewe jenga zako na kwa watu wako!. Hivyo Wayahudi, kina AghaKhan, na madhehebu mengi tu yamefungua shule zao na hata Hospital zao lakini hakuna yeyote aliyekuwa na mufaka na serikali isipokuwa wote wana mikataba sawa na kwa wote kulingana na sheria.

Kama kuna umuhimu wa kwenda shule/Hospital zao, basi serikali hulipia gharama za matibabu ya mtu huyo hivyo mchango wa serikali ni kwa mlipa kodi na sio kuwapa ruzuku tangulizi ya huduma.

4. Kuhusu Zanzibar na swala mla watoto wao ku fail mitihani nadhani hili swali unewauliza wao wakupe takwimu wao zinazothibitisha kuwepo kwa tuhuma hizo. nachoweza kusema mimi ni kwamba tusidharau kero za wananchi na maadam hatuna database utaweza vipi ku analyze data methodically na scientifically wakati huna takwimu zinazotakiwa isipokuwa hearsay.

Bado nasisitiza umuhimu wa serikali yetu kuwa na majibu yanayoridhisha yenye ushahidi wa kisayansi kama ulivyosema wewe, lakini sio serikali kuomba wao ushahidi wakati haina facts, ya ushahidi wa kupingana na shutuma hizo..Waungwana husema kama huna Alibi u become a suspect na hii inaweza kukuweka pabaya zaidi ikiwa tuhuma zitaonyesha ulikuwepo, ulihusika na ukashindwa kujibu..Hata hearsay inabidi tujitetee dhidi ya tuhuma sio kukaa kimya na kuwaita wao washabki ilihali kinawatokea wao na ndio maana wanalalamika.

Nikikuuliza hapa Wazanzibar wangapi wameenda vyuoni waka disco sidhani kama unazo idadi zao kamili kuonyesha kweli hawakuonewa..na huwezi pia kujua kwa uhakika kwa sababu hujui hesabu ya Waislaam nchini japokuwa asilimia 99 ya Wazanzibar ni Waislaam..Je, hao walio disco ni Wazanzibar, wabara ama wazanzibara!

Kuhusu hawa masheikh mkuu wangu pengine unasahau kwamba NDIVYO TULIVYO sisi wote.. wangapi wanapiga kelele CCM imeturudisha nyuma? wanpgapi lakini tazama mikutano yao, tazama uchaguzi wanavyotupeleka mbio na wanachaguliwa na watu hawa hawa wanaolalamika.. Hivyo kwa ushindi wa CCM haimaanishi hakuna watu wameachwa nyuma. Tazama mikoa yote iliyobakia nyuma kimaendeleo iwe Kigoma, Tabora au Songea kote huko ndiko CCM walikozoa kura lakini pia tukumbuke kwamba Udini unaweza kuwa sababu na it is becoming a problem..
 
Back
Top Bottom