Kwanini waislamu hawana imani na vitengo vinavyohusika na takwimu?

Kichuguu, Mkandara, Nguruvi3, Mohammed Shossi,

..jamani hii mijadala ya DINI hamtofikia suluhu hata siku moja.

..unaweza kukuta mtu ni very objective and understanding, lakini linapoingia suala la dini tu anakuwa mtu tofauti kabisa-kabisa.

..binafsi sijui hii nchi inapoelekea ni wapi, lakini mijadala ya dini hapa JF inanipa wasiwasi sana na kinachoweza kutokea huko mitaani.

..baada ya mauaji ya kimbari kule Rwanda, sasa wenzetu wamepiga marufuku utaratibu wa kutaja makabila yao.

..tunachopaswa kufanya ni kuazimia kuishi pamoja kama WATANZANIA na masuala ya dini yawe ya mtu binafsi.
 
Last edited by a moderator:

Joka Kuu unachosema ni kweli kabisa.Imani ni kitu cha ajabu kwasababu inapofika hapo kila mmoja anaacha busara au hekima na hata kupinda ukweli kitu ambacho ni kinyume na dini zenyewe zinavyotaka.

Binafsi nimejitahidi sana kukwepa mijadala ya imani kwa kutambua kuwa hilo ni jambo la mtu binfasi.
Kuna nyakati navutika na kujikuta nachangia kwasababu inafika mahali uongo au uzushi unakuwa kama ni ukweli.
Masuala ya imani yanajadilika sana ikiwa kuna weledi wa kutosha.

Kwa hapa JF mjadala wa kidini imekuwa ni Abdallah, John n.k. imewaacha nje akina Patel, Begin na Lyamfipa.
Kwa bahati mbaya wanaojadili ni vijana ambao nadiriki kusema hawajaona adha ya machafuko achilia mbali kuzijua dini zenyewe.

Lakini pia itakuwa si busara kama tutakaa kimya huku baadhi ya washabiki wanaojiita viongozi wa hizi dini wakiendelea kusambaza ujinga wao. Mathalani, kiongozi anasema katika TV kuwa amewahi kubagauliwa katika huduma kadha ili hali tunajua kuwa kama imetokea ni kwa yeye na si mamilioni wanaopta huduma hiyo hiyo bila ubaguzi.

Pamoja na hayo nadhani niafikiane nawe kuwa haya mambo yawe ya mtu binafsi na kama ulazima wa kujadili upo basi uwepo ukiwa na hoja za maana zenye mashiko.
Tuachane vikundi vinavyochochea udini kwa masilahi yao huku vikiwa haviwezi kusimama na kutetea hoja zao.
 
Kichuguu, Mkandara, Nguruvi3, Mohammed Shossi,

..jamani hii mijadala ya DINI hamtofikia suluhu hata siku moja.

..unaweza kukuta mtu ni very objective and understanding, lakini linapoingia suala la dini tu anakuwa mtu tofauti kabisa-kabisa.

..binafsi sijui hii nchi inapoelekea ni wapi, lakini mijadala ya dini hapa JF inanipa wasiwasi sana na kinachoweza kutokea huko mitaani.

..baada ya mauaji ya kimbari kule Rwanda, sasa wenzetu wamepiga marufuku utaratibu wa kutaja makabila yao.

..tunachopaswa kufanya ni kuazimia kuishi pamoja kama WATANZANIA na masuala ya dini yawe ya mtu binafsi.
Mkuu wangu unaponiona mimi naingia kt mijadala ya dini ni kwa sababu napenda sana tuondoe chuki baina yetu maana imekwisha ingia na inatumaliza. Nimeyasoma na kuyasikia malalamiko ya waislaam pamoja na kutokuwa na wawakilishi wa maana nimewaelewa kama nilivyowaelewa wasukuma wa Bulyahulu au Wamasai wa Loliondo. I have big problem kwa nini ndugu zangu wakristu wanashindwa kuona kwamba swala hili la MuO linavunja UTANZANIA WETU..I have propblem with that.. halafu linapaliliwa sana hapa JF kwamba it's okay hata kama ni kinyume inajaliwa services zake! Hatuwezi kusema sisi Watanzania ikiwa kuna kundi la watu wanadai kubaguliwa halafu hatuna majibu isipokuwa tunawalazimisha wakubali hali hiyo. Tofauti na Kagame ambaye kaweka uwanja sawa halafu kasema nione mtu akizungumzia Ukabila maana hakuna mahala unapoweza kusema Wahutu wanaonewa chini ya Utawala wake. na kinachokatazwa ni kuzungumzia vita ile hasa akiwalenga kabila lake mwenyewe kutolipa kisasi kwa sababu yeye yupo madarakani.

Hatuwezi kutumia maneno matupu basipo vitendo maana waswahili wanasema;- Ada ya mja hunena ya muungwana hutenda. Sina maana mbaya hata kidogo isipokuwa niliyaona haya Bongo ktk vijiwe na kujua kwa uhakika kumbe chuki imeanzia hapa! we never had this thing wakati wa mwalimu isipokuwa toka Kuingia Mwinyi 2nd term tulijikuta ktk hali mbaya sana na Mkapa aliweza nusu japo kwa nguvu lakini hakuyamaliza. Kama navyosema siku zote, mimi sipendi unafiki kuficha kile nacho kiamini kwa kusema uongo na nachelea sana ya Rwanda kutokea sababu ya kitu ambacho tunaweza kabisa leo kukiweka sawa.
 
Nguruvi3, Mkandara, Kichuguu, mohamed Shossi,

..hii mijadala ya KIDINI ni very tempting kuchangia ukifikira kwamba there is something +ve that may come out of it.

..mimi nimeshiriki sana hii mijadala ya kidini hapa JF lakini nilichogundua ni kwamba hakuna kusonga mbele.

..utakuta hoja zilezile zinajirudia tena na tena, na wachangiaji ni walewale, na haionekani kwamba wamebadilika toka kimtizamo toka mijadala iliyopita.

..tuwe wakweli: hivi mjadala huu unaoendelea sasa hivi haujawahi kuwepo hapa JF??
 
Last edited by a moderator:
Mohammed Shossi ukituambia tuende Maktaba ya Taifa sisi tupo mbali ungetuwekea data hizo hapa km hii ya km inaonyesha waislamu bado ni wengi na hakuna mtu anayeipinga
Lakini angalia Madhehebu nimeyaBold Wanatenganisha Catholic, Protestant (Lutheran, AIC, Moravian 7th D.Adventist nk) na Jehova Wittness (PAG, Full / Kakobe, Rwakatare, Mzee wa upako nk) wapo kundi la Indeginous la 35% ambao sio Wakatoliki
Data zote hizo bado unatakiwa uzichimbe zaidi zinazungumzia DINI TANZANIA
mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%;
Zanzibar - more than 99% Muslim

BOFYA
[h=2]Africa > Tanzania > Religion[/h]
Buddhism > By country > Buddhism > % of Buddhists 0.1 %
[54th of 63]
Catholic > Cardinals 1
[36th of 65]
Catholic > Diocesan priests 1,382
[30th of 143]
Catholic > Permanent Deacons 1
[74th of 90]
Catholic > Total Priests 2,080
[32nd of 149]
Catholics
10,313,000
[19th of 140]
Catholics as percentage 25.74

[61st of 150]
Islam > Percentage Muslim
35%

[55th of 168]
Islam > Population 12,868,224
[22nd of 165]
Islam > Shia
1,095,000 [20th of 67]
Islam > Sunni 17,155,000 [17th of 67]

Jehovahs Witnesses
18,250,000

13,697

[60th of 178]

50 %
[40th of 66]
Protestantism > By country > Protestants
5,147,290 [22nd of 167]
Protestantism > By country > Protestants > % Protestant 14 %

[68th of 163]
Religions > All
mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim
Religions > Muslim
35 %

[45th of 100]
Roman Catholicism > By country > Roman Catholicism > % Catholic 25.74 %
[68th of 170]
Seventh-day Adventist Membership 320,643
[13th of 232]

... View all Religion stats
 
Last edited by a moderator:
Kichuguu, Mkandara, Nguruvi3, Mohammed Shossi,

..jamani hii mijadala ya DINI hamtofikia suluhu hata siku moja.

..unaweza kukuta mtu ni very objective and understanding, lakini linapoingia suala la dini tu anakuwa mtu tofauti kabisa-kabisa.

..binafsi sijui hii nchi inapoelekea ni wapi, lakini mijadala ya dini hapa JF inanipa wasiwasi sana na kinachoweza kutokea huko mitaani.

..baada ya mauaji ya kimbari kule Rwanda, sasa wenzetu wamepiga marufuku utaratibu wa kutaja makabila yao.

..tunachopaswa kufanya ni kuazimia kuishi pamoja kama WATANZANIA na masuala ya dini yawe ya mtu binafsi.

Ndugu JokaKuu,

Nilipochangia mada hii sikuwa nadhani kuwa itakuwa ya udini kwani mijadala ya aina hiyoo huwa sichangii; nilifurahishwa sana na ndugu @Mohammed Shossi alipoanzisha mada ambayo kwangu ilionekana kuwa analytical ikiwa supported na takwimu kuwa iwapo data za zamani zilionyesha kuwepo kwa waislamu wengi kwa nini data za siku hizi zionyeshe kuwa waislamu ni wachache? Mohammed aliomba tujadili kwa kama great thinkers na ndiyo maana nikachukua trouble ya kupitia takwimu za zamani na kuzifanyia uchambuzi wangu; ningetegemea mtu ajibu uchambumbuzi wangu kuliko kunishambulia.

Iwapo uchambuzi wangu ulionyesha kudharau waislamu au kuwatetea wakristu basi nimeshaachana na thread hii. Nashukuru sana ndugu JokaKuu kwa kunialika tena hapa, lakini nisingependa kutumia muda kujadili jambo lisilojadilika.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3, Mkandara, Kichuguu, mohamed Shossi,

..hii mijadala ya KIDINI ni very tempting kuchangia ukifikira kwamba there is something +ve that may come out of it.

..mimi nimeshiriki sana hii mijadala ya kidini hapa JF lakini nilichogundua ni kwamba hakuna kusonga mbele.

..utakuta hoja zilezile zinajirudia tena na tena, na wachangiaji ni walewale, na haionekani kwamba wamebadilika toka kimtizamo toka mijadala iliyopita.

..tuwe wakweli: hivi mjadala huu unaoendelea sasa hivi haujawahi kuwepo hapa JF??
Mkuu wangu kuna ukweli mkubwa sana ktk maelezo yako lakini jambo moja tu pengine mimi nitawalaumu moderators kwa sababu wanajua fika kwamba maswala ya imani za dini ni vert sensitive na hayatakiwi kuingia hapa hasa kwenye ukumbi wa siasa.

Ni muhimu sana wawe na control a ukumbi huu la sivyo JF itakuwa chombo kingine cha kueneza Udini maana inaharibu kabisa mada nyingi sana tunapohoji imani za wengine. lakini tutafanya nini ikiwa leo hata CCM, Chadema na CUF ni kama maadui. Pengine hizi sio tamaduni zetu tunalazimisha tu na kujifanya tunajua sana kumbe waja watupu..
 
Mkandara,
Mjadala kama huu unaodadisi mapungufu ya baadhi ya sera za nchi (in this case population census) nafikiri ni wa halali na hakuna sababu ya kuogopa kuujadili eti kwa vile tu unagusia makundi ya dini tofauti. Nafikiri kinachohitajika kujadiliwa hapa ni hayo mapungufu ya sensa, kwa nini yapo, ubora wa kuwa nayo au kutokuwa nayo n.k. Tusiogope kutaja dini as long as tunajadili kwa busara na sio jazba na matusi.

  1. Kwa waislamu kutokuwa na imani na takwimu nadhani sio wao tu bali waTanzania wote hawana imani na takwimu fulani fulani kwa sababu ya kukosekana transparency kwenye maamuzi yanayofanywa na serikali. Sababu za kuondoa kipengele cha dini kwenye sensa sidhani kama kilielezewa kwa wananchi, hata kama suala hilo lilifanyika kwa nia njema.
  2. Binafsi nafikiri uwiano wa sensa ya mwaka 1957 ambayo inaonyesha kuwa, 30.9% waislam, 24.9% wakristo, 44.2% dini asilia na ile ya 1967 inayoonyesha kuwa, 31.7% waislam, 31.2% wakristo, 36% dini asilia na 1.1% others, zinaweza zikawa ni sahihi.
  3. Ongezeko kubwa la wakristo ni rahisi kulielewa kama utaangalia hizo takwimu pamoja na kudadisi historia ya usambaaji wa hizo dini nchini mwetu.
  4. Uislam kwa kiasi kikubwa ulisambaa nchini enzi za biashara ya utumwa na ndio maana utaona mtawanyiko wake kwa kiasi kikubwa nao unafuata maeneo yale yale ambayo hiyo biashara ilikuwa komavu. Hapakuwa na jitihada za waislamu kusambaza dini yao, kwa hiyo ongezeko lao zaidi lilitokana na ongezeko ndani ya familia (uzazi).
  5. On the other hand, ukristo uliingia nchini ukiwa na support kubwa ya nguvu ya dola ya mkoloni na waliouleta ukristo waliuleta kwa nia moja tu, kusambaza dini yao kwenye kila kona ya bara la Afrika. Walifanikiwa sana kwenye maeneo ambayo yalikuwa na watu wa dini za asilia na kwa kiasi kidogo maeneo ya waislamu. Hii iliendelea hata baada ya uhuru na nafikiri bado inaendelea kwenye baadhi ya maeneo hivi sasa.
  6. Kwa hiyo kama trend ya ongezeko la wakristo, linaloonekana kwenye sensa ya miaka ya 1957 na 1967, likitumiwa kama kigezo cha kuangalia uwiano wa wakristo na waislam hivi sasa, sina shaka wakristo watakuwa wengi zaidi.
Lakini swali la kujiuliza ni hili, je tukishafahamu huo uwiano utatusaidiaje? Binafsi naona una manufaa yake, ingawa sio makubwa sana, katika kupanga mipango ya maendeleo. Kujua idadi ya watu wa dini mbali mbali na mahali walipo inaweza pia ikasaidia katika kutafiti na kuelewa mambo mbalimbali yanayoihusu jamii kama magonjwa, matumizi ya huduma na bidhaa n.k. Kwa mfano, tunapochunguza usambaaji wa Ukimwi, unaweza kuangalia trends kutokana na maeneo ya watu wenye imani na mila za aina fulani na ukaelewa ni jinsi gani ya kurekebisha tatizo.

Kwa hiyo utaona kuwa kujua idadi za watu kutokana na imani zao sio jambo baya, bali tunapolifanya kuwa ni siri, ndio mwanzo wa kuleta conspiracy theories na watu kuacha kuiamini serikali yao.
 
Sensa ya mwisho ya Tanganyika chini ya mkoloni wa Kiingereza katika mwaka 1957 ilionyesha kuwa Tanganyika ina Waislamu 58%, Wakristo 32% na Wapagani 10%. Uwiano kati ya Waislamu na Wakristo ilikuwa ni karibu 2:1 yaani kila penye watu watatu, 2 ni Waislamu na 1 ni mkristo, vile vile unaweza kusema waislamu walikuwa ni karibu mara mbili ya wakristo kiidadi Tanzania.

Mwaka 1967 ndio uliotoa matokeo ya ajabu ambayo mpaka leo sio tu Waislamu bali mtu yoyote aliye na akili timamu ana haki ya kuhoji matokeo hayo. Matokeo haya yalionyesha mgawanyiko wa kidini kama ifuatavyo: WAKRISTO: 33.5% yaani wameongezeka kwa 1.5% kulinganisha na sensa ya 1957. WAISLAMU: 31.4% yaani wamepungua kwa 26.6% katika kipindi cha miaka 10 tu. Hii haikuwahi kutokea sehemu yoyote Duniani iwapo sehemu hiyo haikukabiliwa na janga kama vile vita au jambo lolote lilisababisha idadi kubwa ya watu kufariki. Hata china ambayo imeweka sheria ya kuzaa mtoto mmoja tu basi haikuwahi kupungikiwa na watu au kundi fulani la watu katika nchi yao. WAPAGANI: 34.3% yaani wameongezeka kwa 24.3% kwa kipindi cha miaka 10.

Shossi,
Nafikiri umepata takwimu mbovu za sensa ya 1957 na 1967. Takwimu halisi zilizopo zinaonyesha kuwa
mwaka 1957 mgawanyo ulikuwa, 30.9% waislam, 24.9% wakristo, 44.2% dini asilia. Mwaka 1967 inayoonyesha kuwa, 31.7% waislam, 31.2% wakristo, 36% dini asilia na 1.1% others. Kuongezeka kwa wakristo nimeelezea kwa kifupi kwenye post yangu hapo juu.

Kwa waislamu kutokuwa na imani na takwimu nadhani sio wao tu bali waTanzania wote hawana imani na takwimu fulani fulani. Sababu ya kubwa ya kuwa hivyo nafikiri inatokana na kutokuwepo kwa transparency kwenye maamuzi yanayofanywa na serikali yetu. Sababu za kuondoa kipengele cha dini kwenye sensa sidhani kama kilielezewa kwa wananchi, hata kama suala hilo lilifanyika kwa nia njema.
 
Mkuu wangu Kubwajinga naomba source ya takwimu zako.

Mkuu Ngongo,
Hizi ndio source zangu;

  1. National Library of Canada, Ph.D Thesis, 1991, Abdin Noor Chande, Islam, Islamic Leadership and Community Development in Tanga, Tanzania, ISBN 0-315-74635-1. (Document ni kubwa, ila kwa haraka unaweza kuangalia "Notes to the Introduction, pg 31" ina summary ya kutosha).
  2. African Census Report 1957, Dar es salaam Government Printer, 1963.
 
Attachments

  • Islam in Tanga+Tanzania-StreamGate.pdf
    11.6 MB · Views: 33
Mkuu Kubwajinga asante ingawa attachement inagoma kufunguka.

Mkuu Ngongo,
Hizi ndio source zangu;

  1. National Library of Canada, Ph.D Thesis, 1991, Abdin Noor Chande, Islam, Islamic Leadership and Community Development in Tanga, Tanzania, ISBN 0-315-74635-1. (Document ni kubwa, ila kwa haraka unaweza kuangalia "Notes to the Introduction, pg 31" ina summary ya kutosha).
  2. African Census Report 1957, Dar es salaam Government Printer, 1963.
 
Last edited by a moderator:
[video=youtube_share;uPzzGg32H8c]http://youtu.be/uPzzGg32H8c[/video]
 
[video=youtube_share;MIdm1QT9kPc]http://youtu.be/MIdm1QT9kPc[/video]
 
[video=youtube_share;ps7OWXjLWQU]http://youtu.be/ps7OWXjLWQU[/video]
 
[video=youtube_share;uPzzGg32H8c]http://youtu.be/uPzzGg32H8c[/video]
Mkuu Zomba,
Watu kama huyu tapeli anayejiita kuwa ni Shehe ndio wanaoleta vurugu na kuwayumbisha waislamu. Kama waislamu wangeelezwa ukweli ingekuwa rahisi kutafuta ufumbuzi wa mambo mengi yanayowarudisha nyuma.

  1. Hizi hadithi za mkoloni+ukristo vs uislamu, ni za zaidi ya miaka 50, ziwe za ukweli au la, lakini hazimsaidii mtoto wa pale Tanga, Bagamoyo, Kilwa, Mtwara n.k. ambaye shule sio muhimu kama ilivyo madrasa. Wakati huo huo, mtoto wa pale Moshi, Arusha, Mbeya n.k. muda wake wa shule ni shule tu. By the time mtoto aliyetumia muda wake mwingi madrasa anapoingia darasa la 3,4,5 hivi, anakuwa yuko nyuma, kusoma kwa ushindani inakuwa shida na ubongo unakuwa umeshavira. Hapa sina maana kuwa watoto wote wanakuwa hivyo, bali sehemu kubwa sana wanaathirika na hilo. I am talking from experience.
  2. Yapo matatizo mengine mengi tunayoweza kujadili ambayo yanaweza pia kuwa ndio yanawarudisha nyuma waislamu. Lakini kama hii tabia ya kufikiria kuwa wanaonewa bila kuwa na uthibitisho haitaondoka, itakuwa vigumu kutafuta suluhisho na huu umbumbu utaeendelea kwa walio wengi na hatimaye tunaishia kutoamini takwimu kwa sababu sisizo na msingi.
  3. Huyu bwana kwenye video sijui ana elimu ya kiwango gani, lakini sidhani kama ana degree yoyote, kama nitakuwa nimekosea nitaomba kurekebishwa. Lakini utaona wazi kuwa ameweza kuwapumbaza wengi kwenye huo umati wake.
  4. Ingekuwa vema pangekuwa na jumuiya ya wasomi wa kiislamu wa elimu dunia, wanaoelewa historia na makosa waliyofanwya waislamu, hasa ya kutotilia maanani elimu dunia, ili waweze kuelimisha umma wao na kuwapinga hawa wanaotumia umbumbu wa baadhi ya waislamu kuwafanya wajione kutofanikiwa kwao ni kwa vile tu wanaonewa. Hawa wachonganishi wanaotoa hii mihadhara hufanya hivyo kwa manufaa yao binafsi na sio kwa ajili ya waisalamu au kwa ajili ya nchi.
 
1. Kwanini ukweli usisemwe? Si Mkoloni pekee, na wale walioachiwa na Mkoloni wameendeleza, msome Sivalon, Bergen hao wote ambao wewe kwako si matapeli huyo Sheikh anatowa reference, unaweza kuwanukuu japo kidogo kuhusu elimu?

2. Huna uwezo wa kutatua tatizo bila kujuwa chanzo chz tatizo.

3. Wapo wengi tu, wala usiwe na shaka, tulibanwa zamani, sasa tunaibuwa madudu mpaka NECTA. Hujaona? basi hata hujasikia? Hata Slaa hana degree yoyote lakini ana PhD, kwi kwi kwi teh teh teh! kuta nne siyo mwisho au mwanzo wa elimu, huo ni mwanzo wa kuwa "programmed" kama unavojidhihirisha.

4. Ullipoamka wewe, wenzako ndipo walipolala, mwenyewe unaona umetowa wazo la maana? soma hapa: Tanzania Muslim Professionals
 
Mkuu wangu Kubwajinga kwanza nianze mjadala huu kwa kuangalia sababu ulizozitoa kwanini waKristo waliongezeka kwa kasi kubwa between 1957 - 1967 ingawa mpaka sasa bado napatwa na ukakasi wa usahihi wa takwimu zako.Umesema ukristo uliingia nchi na kusambazwa mkoloni [mwingereza &mjerumani] mpaka hapo sina kipingamizi,lakini pia uzingatie mwaka 1967 tulishajitawala kwa zaidi ya miaka sita ?.Sensa ya mwaka 1957 iliendeshwa na wakoloni miaka minne baadae Tanganyika ikajipatia uhuru na miaka mitatu baadae tena tukaungana na Zanzibar yenye waIslamu wengi nadhani hapa ndipo mkuu Mohammed Shossi anapopata ugumu wa kukubaliana na takwimu za sensa ya mwka 1967.

Nitakubaliana na wewe kwamba ongezeko la idadi ya wakristo Tanzania linatoka na mikakati ya wakristo wenyewe kuieneza dini yao na si nguvu za wakoloni kwakuwa ongezeko hilo limetokea wakati tumeshajipatia uhuru.Ni wazi kabisa ongezeko la wakristo limekwenda sambamba na kupungua idadi ya waumini wa dini za jadi[44.2% 1957] & [36% 1967] na si kupungua idadi ya waumini wa dini ya kiislam.Ikiwa takwimu zako ni sahihi na sababu ni hizo nilizosema basi nidhahiri taasisi za kiislamu hazikufanya juhudi kubwa za kuineza dini yao baada ya utawala wa kiarabu kuondoka Tanganyika ukilinganisha na wakristo hasa madhahebu ya wakatoliki,walutheri,waanglican na AIC ambao siku zote wamekuwa na vitengo kwaajili ya kuineza dini katika maeneo ambayo bado kufikiwa na imani yao.

Tusiogope kutaja dini as long as tunajadili kwa busara na sio jazba na matusi.

  1. Binafsi nafikiri uwiano wa sensa ya mwaka 1957 ambayo inaonyesha kuwa, 30.9% waislam, 24.9% wakristo, 44.2% dini asilia na ile ya 1967 inayoonyesha kuwa, 31.7% waislam, 31.2% wakristo, 36% dini asilia na 1.1% others, zinaweza zikawa ni sahihi.
  2. Ongezeko kubwa la wakristo ni rahisi kulielewa kama utaangalia hizo takwimu pamoja na kudadisi historia ya usambaaji wa hizo dini nchini mwetu.
  3. Uislam kwa kiasi kikubwa ulisambaa nchini enzi za biashara ya utumwa na ndio maana utaona mtawanyiko wake kwa kiasi kikubwa nao unafuata maeneo yale yale ambayo hiyo biashara ilikuwa komavu. Hapakuwa na jitihada za waislamu kusambaza dini yao, kwa hiyo ongezeko lao zaidi lilitokana na ongezeko ndani ya familia (uzazi).
  4. On the other hand, ukristo uliingia nchini ukiwa na support kubwa ya nguvu ya dola ya mkoloni na waliouleta ukristo waliuleta kwa nia moja tu, kusambaza dini yao kwenye kila kona ya bara la Afrika. Walifanikiwa sana kwenye maeneo ambayo yalikuwa na watu wa dini za asilia na kwa kiasi kidogo maeneo ya waislamu. Hii iliendelea hata baada ya uhuru na nafikiri bado inaendelea kwenye baadhi ya maeneo hivi sasa.
  5. Kwa hiyo kama trend ya ongezeko la wakristo, linaloonekana kwenye sensa ya miaka ya 1957 na 1967, likitumiwa kama kigezo cha kuangalia uwiano wa wakristo na waislam hivi sasa, sina shaka wakristo watakuwa wengi zaidi.
Lakini swali la kujiuliza ni hili, je tukishafahamu huo uwiano utatusaidiaje? Binafsi naona una manufaa yake, ingawa sio makubwa sana, katika kupanga mipango ya maendeleo. Kujua idadi ya watu wa dini mbali mbali na mahali walipo inaweza pia ikasaidia katika kutafiti na kuelewa mambo mbalimbali yanayoihusu jamii kama magonjwa, matumizi ya huduma na bidhaa n.k. Kwa mfano, tunapochunguza usambaaji wa Ukimwi, unaweza kuangalia trends kutokana na maeneo ya watu wenye imani na mila za aina fulani na ukaelewa ni jinsi gani ya kurekebisha tatizo.

Kwa hiyo utaona kuwa kujua idadi za watu kutokana na imani zao sio jambo baya, bali tunapolifanya kuwa ni siri, ndio mwanzo wa kuleta conspiracy theories na watu kuacha kuiamini serikali yao.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu Kubwajinga kwanza nianze mjadala huu kwa kuangalia sababu ulizozitoa kwanini waKristo waliongezeka kwa kasi kubwa between 1957 - 1967 ingawa mpaka sasa bado napatwa na ukakasi wa usahihi wa takwimu zako.Umesema ukristo uliingia nchi na kusambazwa mkoloni [mwingereza &mjerumani] mpaka hapo sina kipingamizi,lakini pia uzingatie mwaka 1967 tulishajitawala kwa zaidi ya miaka sita ?.Sensa ya mwaka 1957 iliendeshwa na wakoloni miaka minne baadae Tanganyika ikajipatia uhuru na miaka mitatu baadae tena tukaungana na Zanzibar yenye waIslamu wengi nadhani hapa ndipo mkuu Mohammed Shossi anapopata ugumu wa kukubaliana na takwimu za sensa ya mwka 1967.

Nitakubaliana na wewe kwamba ongezeko la idadi ya wakristo Tanzania linatoka na mikakati ya wakristo wenyewe kuieneza dini yao na si nguvu za wakoloni kwakuwa ongezeko hilo limetokea wakati tumeshajipatia uhuru.Ni wazi kabisa ongezeko la wakristo limekwenda sambamba na kupungua idadi ya waumini wa dini za jadi[44.2% 1957] & [36% 1967] na si kupungua idadi ya waumini wa dini ya kiislam.Ikiwa takwimu zako ni sahihi na sababu ni hizo nilizosema basi nidhahiri taasisi za kiislamu hazikufanya juhudi kubwa za kuineza dini yao baada ya utawala wa kiarabu kuondoka Tanganyika ukilinganisha na wakristo hasa madhahebu ya wakatoliki,walutheri,waanglican na AIC ambao siku zote wamekuwa na vitengo kwaajili ya kuineza dini katika maeneo ambayo bado kufikiwa na imani yao.

Mkuu Ngongo,
Nafikiri umenipata vema. Ongezeko la Wakristo Tanzania ni wazi lilitokana na mikakati ya wamisionari kueneza ukristo kila kona ya nchi, tokea enzi ya mkoloni na baada ya uhuru.
  1. Waislamu wa Zanzibar, mwaka 1957 walikuwa ni sehemu ndogo sana ya population kwa ujumla. Ukichanganya Waislamu wa bara na visiwani, asilimia yao ilipanda kwa 3.1% tu na kuwa 34% ya population yote.
  2. Tunaweza kusema kuwa, baada ya uhuru suala la Mwl. Nyerere kuzifungua shule za makanisa na hospitali zao zikawa zinahudumia watu wa dini zote, linaweza likawa lilipunguza kidogo kasi ya uenezi wa ukristo. Hii ni kwa sababu hapo awali, wamisionari walizitumia hizo shule na wakati mwingine hospitali zao, kama vivutio (incentives) au vitamanisho katika kuwaingiza watu kwenye dini yao.
  3. Kwa hiyo tunaweza ku-conclude kwa kusema kuwa, ongezeko la Wakristo limekuwa 'proportional' (sambamba) na upunguaji wa waumini wa dini asilia na pengine pia kwa kiwango kidogo upunguaji wa Waisilamu. Hili sio jambo gumu kulielewa kama mtu ataamua kuliangalia kwa ukweli wake bila kuegemea upande mmoja.
  4. Jambo linalofuata linalohitaji kujadili, kama tutakubaliana juu ya uwiano wa Watanzania wa dini mbali mbali, ni kuangalia kwa nini waislamu na pia baadhi ya makabila wamebaki nyuma kielimu? Je nini nchi ifanye kuondoa hilo tatizo? Maendeleo ya Tanzania yatahitaji wananchi wote wa dini zote na makabila yote kuwa washiriki wakuu katika kuliendeleza Taifa. Kwa hiyo kila mtu anatakiwa kuelimishwa. Bila kuelimisha vema kila kundi la watu, wengine wataachwa nyuma na watakuwa mzigo au kiini cha vurugu kwa taifa.
Kulalamika na kueneza fitina bila kuangalia tatizo kwa undani na ukweli wake haitamsaidia mtu yeyote, awe ni Muislamu au kundi lingine lolote. Wanaofaidika na hizi fitna ni wale tu wanaolipwa kusimama majukwaani kueneza uchochezi kwa manufaa yao binafsi. Ni vema tukajadili jinsi ya kutatua hili tatizo ili tuisukume mbele nchi na tukaachana na fitina na majungu yasiyo na msingi. Mungu ibariki nchi yetu ya Tanzania na watu wake popote walipo.
 
Back
Top Bottom