Kwanini waislamu hawana imani na vitengo vinavyohusika na takwimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini waislamu hawana imani na vitengo vinavyohusika na takwimu?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mohammed Shossi, Aug 27, 2012.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  KWA NINI WAISLAMU HAWANA IMANI NA VITENGO VINAVYOHUSIKA NA TAKWIMU?

  Hili ni suala muhimu kulipatia jibu na kulifahamu kwa kina sisi kama Waislamu. Wengi wana maoni kuwa kitendo cha Waislamu kuomba kushirikishwa katika Sensa na kuomba kuingizwa kwa swali la Dini ni ukorofi tu wa Waislamu.

  Ukweli unafichwa na makala hii ina lengo la kuwajuza watu vipengele kadhaa juu ya hila katika sensa zilizopita. Makala hii itadhihirisha "uchakachuaji uliofanyika na ofisi za serikali katika kutangaza mgawanyiko wa watu kwa mujibu wa dini kabla ya serikali ya Mwalimu Nyerere kuamua kulifuta swali la dini katika sensa ya Tanzania iliyofanyika mwaka 1978.

  Tanganyika au Tanzania imeshafanya sensa mara 6. Mara mbili za mwanzo sensa ilifanyika kama Tanganyika chini ya mkoloni wa Kiingereza yaani mwaka 1948 na mwaka 1957. Kisha sensa nne zilizobaki zilifanyika Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zikiwa zimeshaungana.

  Sensa ya mwanzo ya Tanzania huru iliyoungana iifanyika mwaka 1967 na hii ilikuwa ni sensa ya mwisho kuuliza swali la dini. Sensa zilizobaki zilifanyika mwaka 1978, 1988 na 2002. Sensa ya mwaka huu, 2012 itakuwa ni ya saba katika historia ya nchi yetu na ya tano ya Tanzania huru iliyoungana.

  Sensa ya mwisho ya Tanganyika chini ya mkoloni wa Kiingereza katika mwaka 1957 ilionyesha kuwa Tanganyika ina Waislamu 58%, Wakristo 32% na Wapagani 10%. Uwiano kati ya Waislamu na Wakristo ilikuwa ni karibu 2:1 yaani kila penye watu watatu, 2 ni Waislamu na 1 ni mkristo, vile vile unaweza kusema waislamu walikuwa ni karibu mara mbili ya wakristo kiidadi Tanzania.

  Mwaka 1967 ndio uliotoa matokeo ya ajabu ambayo mpaka leo sio tu Waislamu bali mtu yoyote aliye na akili timamu ana haki ya kuhoji matokeo hayo. Matokeo haya yalionyesha mgawanyiko wa kidini kama ifuatavyo: WAKRISTO: 33.5% yaani wameongezeka kwa 1.5% kulinganisha na sensa ya 1957. WAISLAMU: 31.4% yaani wamepungua kwa 26.6% katika kipindi cha miaka 10 tu. Hii haikuwahi kutokea sehemu yoyote Duniani iwapo sehemu hiyo haikukabiliwa na janga kama vile vita au jambo lolote lilisababisha idadi kubwa ya watu kufariki. Hata china ambayo imeweka sheria ya kuzaa mtoto mmoja tu basi haikuwahi kupungikiwa na watu au kundi fulani la watu katika nchi yao. WAPAGANI: 34.3% yaani wameongezeka kwa 24.3% kwa kipindi cha miaka 10.

  Haya nayo ni maajabu, yaani unaweza ukadhani labda Tanzania ina tatizo la Waislamu kuwacha dini yao na kuwa wapagani. Hili nalo halina ushahidi wowote kuwa lilitokea katika kipindi hicho.

  Athari kubwa ya kimabadiliko iliyotekea katika sensa hii ni kujumuishwa kwa Wazanzibari katika sensa kwa mara ya kwanza. Kwa vile Wazanzibari karibu 98% ni Waislamu tegemeo lilikuwa Waislamu Tanzania wapindukie angalau 65% (kutoka 58% ya mwaka 57 ambayo haikujumuisha Wazanzibari) ya watu wote lakini badala yake wakashuka hadi 31.4%

  Tukumbuke kuwa Waislamu ndio watu ambao mara nyingi hulaumiwa kutofuata uzazi wa majira, hulaumiwa kwa kuozesha mabinti zao mapema na ni dini inayoruhusu mume mmoja kuoa wake wanne, haya yote hupelekea ongezeko kubwa la idadi, lakini ajabu ni kuwa Waislamu walipungua, si kwa asilimia 2 - 3% bali kwa 26.6%! Hivyo ni wazi Takwimu zilizotolewa na serikali ya Mwalimu Nyerere ama zilikuwa ni za uongo wa makusudi ya kupotosha au zina makosa.

  Lakini cha kushangaza ni kuwa baada ya sensa hiyo Serikali ya Mwalimu Nyerere iliamrisha kipengele cha dini kuenguliwa kwenye sensa bila ya kueleza Watanzania lengo la kukiondoa kipengele hicho. wakati huo tayari Tanzania ilishaanza kugubikwa na wingu la udini baada ya Mwalimu Nyerere kuamua kuivunja Jumuiya adhimu ya Waislamu East Africa Muslim Walfare Society (EAMWS) na serikali kuunda Jumuiya ambayo mpaka leo waislamu wana mashaka nayo ambayo ni BAKWATA.

  Naomba sana tuzingatie nukta hii kuwa BAKWATA haikuundwa na Waislamu bali iliundwa na Serikali iliyoongozwa na Mwalimu Nyerere. Kudhihirishwa kuwa mwaka 1967 udini ndio ulikuwa unaanza kushamiri Tanzania sio tu katika sensa na kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA, mwaka 1967 ndio mwaka wa Azimio la Arusha na mwaka wa kesi ya uhaini iliyojumuisha Waislamu na wengi wakawekwa rumande kwa tuhuma hizo akiwemo wanasiasa maarufu ambao waliiunga mkono EAMWS akina marehemu Bibi Titi Muhammed na Tewa Said Tewa. Hivyo leo utaweza je kuwalaumu Waislamu kwa kukosa imani na serikali katika hoja ya sensa?

  Mara nyingi panapotokea badiliko kubwa kama lile ambalo linaaminika kuwa ni la kuchakachuliwa yaani Waislamu kupungua Tanzania kwa 26.6% na wapagani kuongezeka Tanzania kwa 24.3 katika kipindi cha miaka 10 (jambo ambalo mtaalamu yoyote wa sensa au takwimu hawezi kukubaliana nalo) palitegemwa pafanyike utafiti wa sababu za mabadiliko hayo, lakini hakuna aliyeamua kufanya hivyo na sababu kuu ni kuwa watu walijua wazi kuwa takwimu hizo ni za kupika.

  Sisi ni great thinkers tujadili niliyoyaleta jamvini kwa hoja na tafakuri jadidi.
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa mimi ndio serikali ningetaza asilimia ya waislamu ni 60 ili presha iwashuke wenzetu. Sioni benefit yoyote as individual ya kuwa asilimia 10 au 40 au 60 ya dini ninayoiamini mimi...Njaa zangu zinanihusu mimi as individual na sio group ninalokwenda kusali nalo na haina maana asilimia kubwa itakuwa kigezo cha kupewa free lunch anywhere in Tanzania. Kila mtu akili mu kichwa chake.
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kusema takwimu hazina maana unakosea kwani kama hiyo Serikali itaamua kuwapa waislam 60% Swali ambalo linaogopwa kitakwimu ni kwamba laiti sensa ingefichua idadi kubwa ya Waislamu nchini, hoja ya msingi ingekuwa hii; kwa nini kielimu na kimadaraka Waislamu walikuwa wachache?

  Wabunifu wa Mfumo uliojengwa kwa misingi ya dhuluma dhidi ya kundi la Waislamu katika jamii ya Watanzania waling'amua kuwa mikakati yao ya kuwapunja Waislamu taaluma na madaraka ingefichuka kirahisi kama sensa ingeonesha idadi kubwa ya Waislamu nchini.

  Hivyo, kwa maslahi ya mkakati huo wa dhuluma, ilibidi wafiche Idadi ya makundi ya dini ili umma usije kuhoji mbona katika daftari la sensa Waislamu ndio wengi lakini katika nafasi za elimu, utumishi na madaraka ni wachache?

  Wakati vigezo vya sensa vya Umoja wa Mataifa vinajumuisha utambulisho wa dini, Tanzania licha ya kuwa mwanachama wa Umoja huo, ikakiuka utaratibu huo wa kuweka wazi hesabu za watu wa makundi ya dini. Kwa bahati mbaya, mwamko kwa Waislamu ulikuwa bado mdogo au hafifu juu ya ajenda ya kuondosha utambulisho wa dini katika sensa za Kitaifa, hivyo, jambo hilo halikupigiwa sana kelele.

  Laiti ingetosha kuwa, Idadi za Watu wa makundi ya dini hazifahamiki kwa sababu hazijumlishwi kupata wastani katika daftari la sensa, huenda kila mmoja angeamini kuwa uamuzi huo ulikuwa wa kizalendo.

  Lakini ajabu ambayo imeonekana Kitaifa na Kimataifa ni kwamba, taasisi kadha wa kadha zimekuwa zikitoa au kutumia takwimu zinazoonesha kuwa kundi la Wakristo ndilo linalounda jamii kubwa ya Watanzania likifuatiwa na lile la Waislamu!

  Hiyo ni kusudi ya wabunifu au tuseme waasisi wa mfumo kandamizi uliohujumu nafasi ya Waislamu kielimu na kiutumishi katika nyadhifa za juu na madaraka. Kwa nini walifanya kusudi hiyo? Kwa sababu walitaka jamii na dunia iamini kuwa uchache wa Waislamu katika maeneo hayo ni matokeo ya uchache wa idadi ya jumla!
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Kwani madaraka watu wanapena tu hata kama hawana sifa za kupewa hayo madaraka? Halafu suala la elimu, huoni kama nalo linabaki ni suala la kuhimizana familia, na jamii kwa ujumla? Umewahi kujiuliza kwanini kuna tofauti say ya waislamu wa machame na Same na wengine wa pwani?

  Halafu wale huwasikii kupiga kelele maana kwao maisha ni kazi na tamaduni zao zinawahimiza hivyo. Mwisho wa siku hakuna mtu atakayekupa kitu ambacho yeye mwenyewe hana...serikali itakayojaribu kutoa madaraka kwa kuangalia dini badala ya uwezo wa mtu itakuwa muflisi.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mohammed Shossi ningeomba source ya hizo takwimu za mwaka 1957 na mwaka 1967 kwanza kabla sijaanza kujadili.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani takwimu ni muhimu sana. Umuhimu wake ni kukidhi matakwa ya pande zote si mbili zinazokizana bali zote kwenye mzunguko.

  Nionavyo mimi, takwimu muhimu ni ile yenye maslahi yangu. MAISHA YANGU YOTE NI TAKWIMU. Mimi binafsi, kwa msingi huo Serikali ina maslahi kwenye takwimu za nchi si zangu. Tatizo ni maslahi gani? Kama ni serikali wakilishi, basi ni kwa masilahi ya walioiweka madarakani. Nina wasi wasi kama serikali yetu ina dhamana hiyo.

  Takwimu binafsi ni kama 1. Imani yangu, 2. Kipato changu, 3. Familia yangu 4. Mila na nasaba yangu etc. Takwimu za Kitaifa ni kama Kipato cha kaya, kiwango cha msambao wa elimu, shughuli za uchumi, huduma za kijamii ni baadhi tu.

  Hoja yako ina rutuba ya historia ya sensa, kama nilivyo tanguliza hapo juu, zote zilizofanyika huzijabainisha matakwa na masilahi ya serikali kwa baadhi yetu. Maana ya hoja yangu kwenye matokeo ya sensa zote hizo sijasikia hoja ya serikali kuwa kulingana na matokeo hayo, mipango ya maendeleo ikoje kwa misingi ya madokezo ya sensa. Tuseme ni udhaifu wa serikali yetu. Ingawaje piia ni udhaifu wetu wananchi kwa kushindwa kuibana serikali kutokana na matokeo ya takwimu hizo.

  Hapa nataka kujenga hoja kuwa si suala la vitengo vya serikali vinavyohusika na takwimu bali ni suala la dhamira na maslahi ya sensa. Hapa kuna wimbo wa kupanga maendeleo ya wananchi kulingana na matoke ya sensa; lakini unakosekana ushahidi wa sensa zilizotangulia kukidhi hayo mahitaji. Suala la dodoso za kiimani(dini) linatupa shida wengine kwa sababu ile ile kuwa lina masilah gani kwa nani, lini kwa muda gani.

  Takwimu kupanda au kushuka kwangu mimi halinigusi kwa sababu ya serikali yetu kutokuwa wazi na matokeo ya sensa. Kibaya zaidi fursa nzima ya kuhoji matokeo ya sensa au haipo au haidaiwi.

  Mohamed naguswa sana na mtazamo wako wa kufa kwa EAMWS na kuanzishwa BAKWATA. Nina sababu nyingi nitataja baadhi.

  1. Mwenendo wa sasa wakudai Mahakama ya Kadhi na kuwekwa kwenye ilani ya CCM ni kiashirio tosha kuwa hakukuwa na umakini wa kufikia lengo muafaka la kupata au kuundiwa hizi taasisi za kiislamu. Upande wa pili wakati serikali ilikuwa na mapungufu waumini wa kiislamu walikuwa na fursa zipi na gani?

  2. Fursa zipi zilizopo kufikia lengo kuu tarajiwa? Hapa nazunguzia kujua idadi halisi ya watu wa dini fulani. Mimi naona waumini wa dini zote wana fursa sawa za kujua idadi yao kwa dhamira na maslahi yao. Kuna sababu moja ya msingi kwenye hili; nayo ni kuwa SERIKALI KAMA KWA DHAMIRA AU KWA UDHAIFU haina maslahi na hili kwa sababu haina uwezo nalo, pia ni kwa sababu linaweza kufanyika na wenye masilahi nalo bila kuihusisha serikali.

  Maoni yangu binafsi suala siyo kwa nini waislamu hawana imani na taasisi za takwimu, bali suala ni kwa nini waislamu hawachukui fursa au hawavalii njuga suala la takwimu za waumini wake. Hilo naona litatoa mwanya wa kujenga hoja kusudiwa na idadi linganishi. Hapo kwangu mimi kutaifanya serikali ijitetee na hitilafu yo yote ya takwimu zake.
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu Shossi ina maana hujui mpaka leo sababu ya hili? Elimu na madaraka hayafuati imani ya mtu bali uwezo na kujituma kwake! Huwezi kukaa tu na kuamini kuwa kwa kuwa Muislamu basi utapata elimu na madaraka. Jengeni shule, vyuo na muhimize watoto wenu wasome shule badala ya madrassa ! Hata hivyo vyuo vichache mlonavyo mnasoma Arabic language na Islamic Knowledge.

  Mimi katika maisha yangu ya utu uzima sijawahi kusikia kiongozi wa kiislamu akihimiza kupata elimu dunia kwa dhati. Ndugu yangu mmoja Muislamu nilipata kumuuliza kuhusu mustakabali wa mwanawe akanijibu kuwa siku hiyo ameenda shule ya ''kizungu'' kwa huzuni kubwa sana.Akalalama kuwa hizi shule za ''kizungu'' zitamuharibu mtoto. Hakika nilisononeka sana!.

  Wingi wa waislamu katu hautowasaida kimaisha.
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mohammed Shossi Mkuu, kuna siku niliwahi kutoa maoni yangu kwenye makala ya Mzee Mwanakijiji, kuwa linapokuja suala la idadi ya waumini wa dini Tanzania, tunakuwa tunajichukulia kama TZ nzima ina dini mbili tu, Wakrsto na Waislamu, tukiwaweka upande wale wa imani nyengine na kuwaweka wote katika kapu moja la Wapagani, ndio maana ukaona hakukuwa na hata kipengele cha jumla ya dini nyengine licha ya kuzitaja. Kwa hivyo, pamoja na dhana kuwa watu pangine walijibainisha/kubainishwa kama "hawana dini" ama zao wenyewe kwa sababu hakuona umuhimu wa dini, au kwa watu wa data kuchakachua kwa makusudi.

  Kutokana na sababu hizo hapo, pamoja na ukweli kwamba miaka ya 60 watu wengi walikuwa wafuasi wa ukomunisti na walijisifia kutoamini Mungu, pamoja na kutohesabu wa dini nyengine, ndio maana kukaonekana na ongezeko hilo la Wapagani ingawaje wengi wao kiuhakika walikuwa wa dini nyengine ambao hawakutajwa katika sensa. Kama kulikuwa na ukweli kuwa katika sensa ya mwaka huo Wakristo waliongezeka kwa asilimia 1.5, uwekeano mkubwa ni kwa Waislamu kuongezeka asilimia kubwa kidogo ya Wakristo lakini sidhani kama ingezidi asilimia 2.5 kwa vigezo hivyo ulivyosema vya kuzaliana bial mpango, kuoa wake wengi, kuozesha wasichana wadogo.

  Lakini nikija suala lako la kwa nini aislamu hawana imani na takwimu nchini TZ, inasikitisha lakini ndio ukweli kuwa si Waislamu tu bali Watanzania wote hawana imani na takwimu zote za taifa, ziwe za sensa ziwe z matokeo ya uchaguzi. Viongozi na wenye uwezo wanachakachua kila kitu, hata kwenye manunuzi ya serikali na matumizi ya serikali. Mtu ananunua au kutumia cha 100,000, kwa huruma ataongeza vijizero angalau viwili, yaani kutoka 100, 000 hadi milioni moja hadi kumi. Hii ndio bongo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ukitaka kufanya confirmation nenda maktaba kuu ya taifa utapata kila kitu pale. Usiwe mvivu kujisomea.
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Umechangi vizuri sana especial mwisho!

  Kuhusu kutokupanga uzazi na maswala ya kuoa wake zaidi ya mmoja.... mfano mimi wale tuliomaliza nao Dodoma Sec miaka zaidi ya 12 iliyopita marafiki zangu "wakristo" wengi wao hawajaoa/olewa na walio oa/olewa hawana mtoto zaidi ya mmoja! Lakini rafiki zangu wa kiislam wake kwa waume nikiwamo mimi tuna watoto zaidi ya mmoja! Madhalan mimi nina wake wawili in ten years siwezi kuwa sawa na Rafiki yangu ambae hana mke wala mtoto maana mimi dini yangu hainiruhusu kufunga uzazi kwa njia yoyote ile! that means nitakuwa na watoto wa kutosha tu!

  Take from me then zidisha kwa hao waislam wachache uwajuao wewe.
   
 11. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wewe ni GT kuwa na akili kama GT hoja za kuwa waislam hawasomeshi watoto wao si za kweli hizo ni propaganda zenu tu.

  Swali kwako bwana mkubwa Waislam wamegomea Serikali katika Sensa sijui Wakristo kinawauma nini? Au kuna ndoa baina yenu na Serikali? au kuna agenda iliyojificha baina yenu? Waachwe waislam wagome kama ni ujinga wao wabaki na ujinga wao ninyi wajanja bakini na ujanja wenu.

  Kuhusu kutowasomesha watoto wao Mwanzo, ilidaiwa kuwa mfumo wa Kikoloni uliwabana Waislamu kielimu kwa sharti la kuritadi ili wapewe elimu, sawa kabisa, mtu angekubali kuwa katika miaka ya awali ya uhuru nafasi za madaraka zingejazwa na Wakristo waliopendelewa kielimu na mkoloni. Lakini hoja ambayo ingewashinda Wabunifu wa mfumo wa dhuluma ni kwamba mbona hata baada ya uhuru Waislamu wameendelea kuwa wachache katika nyanja za elimu? Kama nyuma kulikuwa na sharti la kubatizwa, je baada ya uhuru sharti hilo lilikuwepo? Lakini bado hilo nalo lingesutwa na idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi.

  Waislamu waliandikisha watoto wao kwa wingi katika ngazi ya msingi nchini kote. Sasa, swali lingekomaa zaidi, kwa nini Waislamu waendelee kuwa wachache hata baada ya miaka mingi ya uhuru? Ni wazi mfumo wa dhuluma ungebainika kirahisi. Ndio maana waasisi wake wakawa makini na sensa ya Taifa ili wajenge hoja ya jumla kuwa Waislamu ni wachache katika nyanja za elimu na madaraka kwa sababu jamii yao ni ndogo kama zilivyo jamii za watu wa makundi mengine madogo. Na Wakristo ni wengi kwa sababu wao ndio wanaounda asilimia kubwa ya Watanzania. Angalau kwa kuficha takwimu za Waislamu walijiridhisha kuwa dhuluma waliyowafanyia Waislamu ingehalalika kwa mdadisi au mtafiti yeyote yule ambaye angetaka kuhoji kwa nini Waislamu ni wachache madarakani?

  Nimeileta hoja hMwanzo, ilidaiwa kuwa mfumo wa Kikoloni uliwabana Waislamu kielimu kwa sharti la kuritadi ili wapewe elimu, sawa kabisa, mtu angekubali kuwa katika miaka ya awali ya uhuru nafasi za madaraka zingejazwa na Wakristo waliopendelewa kielimu na mkoloni.

  Lakini hoja ambayo ingewashinda Wabunifu wa mfumo wa dhuluma ni kwamba mbona hata baada ya uhuru Waislamu wameendelea kuwa wachache katika nyanja za elimu? Kama nyuma kulikuwa na sharti la kubatizwa, je baada ya uhuru sharti hilo lilikuwepo? Lakini bado hilo nalo lingesutwa na idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi.

  Waislamu waliandikisha watoto wao kwa wingi katika ngazi ya msingi nchini kote. Sasa, swali lingekomaa zaidi, kwa nini Waislamu waendelee kuwa wachache hata baada ya miaka mingi ya uhuru? Ni wazi mfumo wa dhuluma ungebainika kirahisi.

  Ndio maana waasisi wake wakawa makini na sensa ya Taifa ili wajenge hoja ya jumla kuwa Waislamu ni wachache katika nyanja za elimu na madaraka kwa sababu jamii yao ni ndogo kama zilivyo jamii za watu wa makundi mengine madogo.

  Na Wakristo ni wengi kwa sababu wao ndio wanaounda asilimia kubwa ya Watanzania. Angalau kwa kuficha takwimu za Waislamu walijiridhisha kuwa dhuluma waliyowafanyia Waislamu ingehalalika kwa mdadisi au mtafiti yeyote yule ambaye angetaka kuhoji kwa nini Waislamu ni wachache madarakani?

  Mwanzo, ilidaiwa kuwa mfumo wa Kikoloni uliwabana Waislamu kielimu kwa sharti la kuritadi ili wapewe elimu, sawa kabisa, mtu angekubali kuwa katika miaka ya awali ya uhuru nafasi za madaraka zingejazwa na Wakristo waliopendelewa kielimu na mkoloni.
  Lakini hoja ambayo ingewashinda Wabunifu wa mfumo wa dhuluma ni kwamba mbona hata baada ya uhuru Waislamu wameendelea kuwa wachache katika nyanja za elimu? Kama nyuma kulikuwa na sharti la kubatizwa, je baada ya uhuru sharti hilo lilikuwepo? Lakini bado hilo nalo lingesutwa na idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi.

  Waislamu waliandikisha watoto wao kwa wingi katika ngazi ya msingi nchini kote. Sasa, swali lingekomaa zaidi, kwa nini Waislamu waendelee kuwa wachache hata baada ya miaka mingi ya uhuru? Ni wazi mfumo wa dhuluma ungebainika kirahisi.

  Ndio maana waasisi wake wakawa makini na sensa ya Taifa ili wajenge hoja ya jumla kuwa Waislamu ni wachache katika nyanja za elimu na madaraka kwa sababu jamii yao ni ndogo kama zilivyo jamii za watu wa makundi mengine madogo.

  Na Wakristo ni wengi kwa sababu wao ndio wanaounda asilimia kubwa ya Watanzania. Angalau kwa kuficha takwimu za Waislamu walijiridhisha kuwa dhuluma waliyowafanyia Waislamu ingehalalika kwa mdadisi au mtafiti yeyote yule ambaye angetaka kuhoji kwa nini Waislamu ni wachache madarakani?

  Nimeileta hoja hii kwenye jukwaa la Great Thinkers kwa kujua kuwa nitajibiwa kwa hoja zenye mashiko na sio hoja nyepesi nyepesi zenye chembe chembe za kudhihaki waislamu na uislamu.
   
 12. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kwa kipindi cha miaka yangu 45 duniani nikiwa hapa tanzania, sijawahi kuona nimepewa favour ipi kw akuwa mimi ni mkristo au nimenyimwa favour au haki gani kwa kuwa muumini wa dini hiyo au kwa kutokuwa muumini wa dini nyingine. na kwa kipindi chote hicho sijawahi kuwa na hisia chanya au hasi kwa mtu kutokana tu na dini yake. kwangu mimi wote ni watu na kama mtu ntamuamua kwa jinsi atakavyokuwa kwenye fursa iliyotuweka pamoja.

  juzijuzi wakati wa uhamaishaji wa sensa nilisikia caption ya hotuba ya Nyerere enzi hizo akisema kwa nini waliamua kuliondoa swali la dini kwenye dodoso la sensa. alisema serikali haipangi mipango yake kwa kuangalia dini, na wala haina hoja ya kujenga misikiti au makanisa au mahekalu. wenye kutaka kujua idadi ya waumini wao ni viongozi wao wa dini na hilo walifanye wao kwa vile wanawajua na wanakutana nao (akatania wanaenda hata kuuungama huko!)

  Nadhani ni dhana sahihi kabisa tena kwa nchi kama zetu hizi 'changa' ambazo hisia za kidini zinaweza kuwagawa wananchi kwenye makundi pinzani, kama alivyosema yeye mwenyewe nyerere.

  Mwisho kwa kuendelea kumjibu mtoa mada, kama waislamu hawana imani na taasisi za serikali kwenye sensa, kwa nini wanaishinikiza serikali hiyo hiyo kuweka kipengele cha dini kwenye dodoso?
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  nimekuelewa mkuu....bakia hivohivo....hukuwa na haja ya kurudiarudia lakini....ila jana waislamu wengi sana walihesabiwa
   
 14. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nisingependa kuchachahua uzi wako, lakini hilo katika red, pamoja na uumini na imani zetu, ruhusa haina maana ya lazima. Nakusudia kusema kuwa sio lazima kuoa mke zaidi ya mmoja au kuwa na watoto zaidi ya wawili ikiwa mtu hataki.
  Watu huchukulia tafsiri ya juu juu tu kauli za kuwa "Zaeni ili muujaze ulimwengu" na " Mtume Muhammad (Amani Iwe Juu Yake) atafurahishwa na wingi wa umma wake," bila ya kujali wale wanaozaa umma huo kwa wingi wana uwezo gani wa kuwapa matunzo wanaowazaa.

  Na hapo blue nina mashaka napo kidogo kwani nilidhani uzazi wa mpango umeruhusiwa katika Uislamu, tafauti ni mbinu tu za kufuata.
   
 15. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani hisia hizi za waislamu zinaweza kumaanisha jambo lingine, na hili la sensa likawa ni aidha ghiriba za macho au linatumika kama sababu ya kuelezea hisia nyingine kubwa zaidi na yenye kuuma zaidi.

  Kwa mawazo yangu nadhani waislamu kama kikundi kinatoa 'frustrations' zao za kushindwa kwa serikali tawala tena hususan za 'mwislamu' mwenzao kuweza kuwanufaisha zaidi au kupata mgao mkubwa zaidi wa keki ya taifa na au kuwatoa kwenye 'umasikini' na hali nyingine mbaya za maisha. Kwa maana nyingine ile dhana ya maisha bora kwa kila mtanzania imeshindwa na sasa kila mwenye eneo lake la kuonesha 'frustration' kwa kushindwa huko anatumia hicho alichonacho mkononi mwake kuonesha hisia zake.

  Sidhani kama dhana ya maisha bora kwa kila mtanzania ingefanikiwa tungekuwa na haya yote
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mohammed Shossi mimi si mvivu hata kidogo ila niko mbali na maktaba kuu ya taifa fanya utaratibu ikiwezekana tuwekee hapa jamvini.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kuna kitu inaitwa "Abuja declaration" ya mwaka 1989 ya kuhakikisha kuwa Africa yote inakuwa ya kiislamu. Sasa nahisi hawa wanaong'ang'ania kipengele cha dini kiwekwe dodoso la sensa wanataka kupima mafanikio ya harakati zao hizo.Tumewashtukia.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mohammed Shossi,

  Mkuu wangu unayafanya makosa yale yale yalofanywa na watu wasiokuwa GT..hii ni tuhuma zilizojaa udini kabla na baada ya Uhuru kuhusu tofauti zetu na hasa baina ya Waislaam na Wakristu. Mimi husema wazi kwamba haijalishi waislaam wako wangapi hata wakiwa asilimia 80 haina maana nafasi zao ktk ujenzi wa Taifa lazima ifikie asilimia 80 isipokuwa kuwepo kwa usawa equal opportunity ndio kipimo halali cha uhuru na haki walopewa wananchi. Wingi wa watu hakuwezi kuhalalisha nafasi yao ktk ujenzi wa Taifa haya ndio yale maswala ya Rwanda na Burundi unajaribu kuyajengea hema.

  Umuhimu wa takwimu hizi kuwa na kipengele cha dini unatokana tu na mfumo wa kiuchumi unaotumika leo hakuna ziada. Nyerere aliondoa kipengele cha dini kwa sababu alichukua siasa ya Ujamaa na Kujitegemea uliotaifisha shule zote zinazomilikiwa na vyombo vya dini ili maswala yote ya Elimu na Afya yawe mikononi mwa serikali akiamini kwamba ni serikali pekee inayoweza kutoa haki sawa kwa wote wenye utengano wa kiimani na makabila. Sisi tulio soma enzi ya mkoloni na Nyerere tuliona tofauti ya mfumo huo ukitupa waislaam fursa ya kukaa viti vya mbele na wakristu. Kwa wenye biahsara hizo hawakufurahia lakini ukweli utabakia kwamba the means did justify the end.

  Toka mwaka 1967 hadi mwaka 1984 Tanzania tuliondokana kabisa na Udini na Ukabila kiasi kwamba hata Mkristu alikuja mtafuta Muislaam amchinjie kuku wake. Mwezi wa Ramadhani tulifunga na marafiki zetu wakristu tukajenga Uzalendo wa kuipenda nchi yetu dhidi ya makundi ya watu. Ujamaa ulitufundisha zaidi kuondokana na ujinga na umaskini zaidi maana mtu mjinga na maskini ni sawa na mtoto mdogo au kilema. Huyu mzazi anatakiwa kumweka chini ya mwavuli wake hadi anapokuwa na kuweza kujitegemea ndipo huondoka ktk kinga ya mzazi.

  Tatizo la sisi wengine kuhusu sensa hii ni kwa kuzingatia kwamba sasa hivi tupo ktk mfumo wa kibepari. Mfumo unaoweka mamlaka ya kuzalisha na ugawaji mikononi mwa wananchi na sio serikali tena. Hivyo kazi kubwa ya serikali ni kuandaa sera na mikakati itakayo mwezesha mwananchi kuzalisha na usambazaji kwa kujenga miundo mbinu na msingi wa maendeleo yao.. Sasa unapoondoa kipengele cha dini wakati sheria inaruhusu tofauti zetu kuwa nyenzo za maendeleo yenyewe hapo ndipo utata unapojitokeza.

  Na ndio maana leo hii imekuwa mwenye nguvu ndiye hula nyama na sidhani nkama waislaam wanalikubali hilo kutokana na kwamba mfumo wa ELIMU na AFYA umerudishwa kama ilivyokuwa wakati wa mkoloni, wakristu wakipewa kipaumbele na nguvu ya kumiliki sekta hizo. Kuweka swala la ELIMU na AFYA kusambazwa na vyombo vya dini kunarudisha udhalilishaji wa Waislaam kabla ya Uhuru hivyo kuwanyima nafasi sawa ktk ujenzi wa Taifa hili, na hofu kubwa ya serikali na wakristu ni pale itakapo gundulika kwamba Waislaam wametengwa.

  Takwimu hizi zitajieleza wazi na hivyo kuzua udini ambao kumbe huwa wanaufanya makusudi laa sivyo hawana sababu ya kuogopa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Mie nina mashaka na takwimu za enzi ya mkoloni.

  Sensa ilifanyikaje?
  Elimu ya watanganyika ilikuwaje?
  Miundo mbinu je?
  Tukiangalia influence ya ukoloni wa kiarabu ktk afrika mashariki utaona maeneo ya mwambao yaliegemea dini ya kiislam zaidi, mbali na pwani kulijaa wasio na dini sasa iliwezekanaje wasio na dini wakawa 10%?

  Kama Nyerere aliondoa kimakosa kipengele cha dini, nini kilimshinda Mzee wetu Mwinyi kukirejesha?
  Hata Mh. Kikwete ameshindwa, nae hawapendi waislam?

  Brother ktk historia yako, umewahi kukosa huduma kutokana na dini yako?

  Wakiweka kipengele cha dini nitapenda waweke na cha kabila kabisa ili tuheshimiane!
   
 20. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mohammed Shossi

  Kwa great thinkers lazima kutakuwa na majibu. Kwanza sitaki kuamini kuwa waislamu wamegomea sensa, hilo wazo la kugomea sensa linaletwa na watu wenye ajenda zao, watu ambao ni mufilisi, wanajua wanataka nini. Unaposema waislamu ni wachahce madarakani sijui unazungumzia madaraka yapi, wakati rais, makamu wake, mnadhimu mkuu wa jeshi, ofisa mkuu wa TISS, kamanda mkuu wa polisi ni waislamu, nyadhifa zote za juu wako waislamu. Hakuna wadhifa wa juu hapa Tanzania kuliko urais, na yeye amejitahidi sana kuwaweka wasialmu kwenye milango yote muhimu, labda ameshindwa tu kumuweka kadinali mwislamu.

  Mkuu ukitaka kujua tofauti ya wakristo na waislamu nenda Uingereza, uangalie wakristo wanafanya nini na waislamu wanafanya nini. Kule hakuna serikali ya Tanzania, au nenda Marekani ukaone watanzania wakristo na watanzania waislamu wanafanya nini, ukitumia kioo hicho ndio unaweza kujua hali halisi. Angalia watanzania walio magarezani nje ya Tanzania uone kama serikali za huko huwa zinachagua wahalifu kwa sababu ya dini, au angalia ni kwanini waislamu wenyewe hawataki kwenye nchi za kiislamu wanakwenda kwenye nchi za "kikristo" na kikafir. Ukipata takwimu za haya machache, jaribu kujiuliza ni kwanini.

  Unaweza kuona wazi kuwa hapa Tanzania matajiri wakubwa sana ni waislamu, angalia elimu za watoto wao. Au angalia wanawekeza kiasi gani katika elimu, au wanachangia kiasi gani katika elimu.....then angalia wanawekeza kiasi gani katika kujenga misikiti, au kufuturisha.

  jaribu hata kuangalia elimu za watoto wa viongozi waislamu na wasio waislamu uone ni wapi wanachangamkia zaidi elimu. Unaweza kushangaa sana, au angalia baba zao wanawekeza zaidi kwenye nini. nyumba, nyumba ndogo, elimu au burudani. Ukipata majibu hayo unaweza kuona ni swala la utamaduni.

  Kuna wengine wanathamini elimu, wengine elimu ni by the way tu. Watu wengi wa pwani (sio wote) hawathamini elimu, tena wote wakristo na waislamu. Sababu kubwa ni kwamba they have that mindset by deafult, kuna mambo wanayoyapa kipaumbele, si elimu. Kuwapeleka watoto shule ya msingi kunatokana na kuwa wanabanwa kisheria kama wasingebanwa wasingepeleka watoto wao shuleni. Kama utakuwa unafuatilia habari kuna kundi fulani kule Nigeria linaitwa Bokoharam, ni kundi la kiislamu ambalo linapinga wazi elimu ya kimagharibi, wao wanataka elimu ya kiislamu ndio ifuatwe.

  Au hapa kwetu angalia shule zinazoitwa za kiislamu, Al haramain, ubungo na Kinondoni muslim,(huko hawabatizwi na wala hawalishwi nguruwe) angalia jinsi zinavyoendeshwa, na jinsi zinavyofundisha na jinsi matokeo yake yalivyo.

  Hata ukiangalia among waislamu wenyewe unaweza kuona tofauti. Ukiangalia unguja na pemba unaweza kuona waislamu wa Pemba wana elimu zaidi kuliko wale wa unguja, kwanini? hapa dini sio factor kwa kuwa wote ni waislamu.

  Au jaribu kutafuta Profesa wa pwani na wa bara, bila kujali dini zao, hata wawe wamesoma darasa moja unaweza kuona wana tofauti sana, toka mavazi hata vichwani, hata argument zao ukipima unaweza kuona zina tofauti sana. Tatizo ni nini?

  Jibu rahisi kwa hoja yako ni utamaduni. Dhuluma unayosema inatendwa dhdidi ya waislamu inweza kuondolewa tu kwa elimu. Utamaduni wa kupenda na kuthamini elimu has to be deep rooted for it to flourish, it is not something that can just harvested without putting any efforts. You always rip what you sow.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...