Kwanini wahandisi wa Halmashauri wanasimamishwa sana?

thobias fulano

New Member
Feb 17, 2024
1
0
Wahandisi wanaoajiriwa Halmashauri na Taasisi zingine za kiserikali wanautofauti gani na Kwanini wanasimamishwa sana?

Serikali inajitahidi kuajiri wahandisi (engineers) kwenye taasisi zilizopo chini ya TAMISEMI hasa HALMASHAURI kwa lengo la kusimamia Miradi ya ujenzi ambayo serikali inatumia fedha nyingi sana ili kuboresha na kuchochea maendeleo katika nyanja za elimu na afya.

Lakini kumekuwa na changamoto ya kusimamishwa kazi kwa wataalamu hao wa ujenzi kwa manufaa binafsi ya Wakurugenzi pamoja na kuwatishia kuwafukuza na kuwachongea kwa Waheshimiwa Madiwani ili waonekane tu hawafai.

Swali la kujiuliza kwanini TAASISI zingine ambazo hazipo chini ya Wakurugenzi(Local givernment) wahandisi hawasimamishwi.

Wahandisi walipo chini ya wakarugenzi wamefanywa kuwa mbuzi wa kafala wanatumika kufichia maovu ya wakurugenzi katika utekelezaji wa miradi hii.

Kuna haja sasa ya serikali kulifanyia kazi suala hili kuona namna gani inawasaidia watalaamu hawa wa ujenzi ili wasiendelee kuonewa kwa kubambikizwa kesi zisizowahusu.
 
Back
Top Bottom