Mama Ananilea Nkya: Kumekuwepo na kigugumizi kwa Wanawake na Vijana wasomi kuwania nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mama Ananilea Nkya kutoka Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uchaguzi na Uongozi ametoa rai kwa wasomi hususani Wanawake na vijana kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mbeleni mwaka.

Amesema kuwa hili kuwepo kwa mabadiliko ya Maendeleo jamii hususani Wanawake na vijana wasomi hawana budi kuingia kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuondokana na dhana ya kuchukulia kawaida nafasi hizo.

"Nawahasa Wanawake wajiandae wa vyama vyote na niwahimize hata Wanawake wasichana ambao wako mtaani wajiunge kwenye hivyo vyama wagombee nafasi kwa sababu pale kwenye Serikali chini ndipo kunatakiwa kuwepo wasomi. Wapo Wanawake na vijana wenye uwezo mkubwa wanaweza kuleta mapinduzi kwa kuleta maendeleo ya vijana, wasichana, watoto pale kwenye ngazi za Mitaa."

Akizungumza Machi 6, 2024 kwenye mjadala ulioandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu (THRDC) kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake Watetezi wa haki za binadamu (CWHRD)Katika kuelekea madhimisho siku ya Wanawake Duniani ambayo ufanyika March 8, kila mwaka amesema watu wengi wamekuwa na mtazamo hasi juu ya nafasi ambazo uwaniwa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

"Watu wanadharau sana kwamba kule ngazi za chini kwenye Mitaa kwenye Vitongoji kwamba sio nafasi nzuri za kugombea. Hizo ndizo nafasi ambazo unaonesha umahili wako wa kuwa kiongozi ambapo tunatakiwa watu waliosoma waende kule kugombea ili wajenge jamii nzuri kutoka kule chini, ili waweze kudai rasilimali zinazotolewa kwenye Halmashauri ziletwe kwenye vijiji kwenye Mitaa na kwenye vitongoji. Bila kuwepo na watu makini waliosoma wakike na wakiume hizo rasilimali nani atazipigania?" amesema

Kufuatia dhima kuu ya mwaka huu isemayo "Wekeza kwa Wanawake harakisha Maendeleo", amedai kuwa ushiriki wa Wanawake katika nafasi za uongozi inaweza kuwa chachu ya maendeleo lakini amedai hili suala hilo liweze kufikiwa lazima Wanawake na vijana waondoe kigugumizi katika kuwania nafasi za uongozi.

Kufuatia mjadala huo ambao umefanyika kwenye ukumbi wa PSSSF Samora Jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha wakurugenzi Wanawake zaidi ya 50 kutoka taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali, Ofisa Uchechemuzi THRDC, Wakili Nuru Maro amesema kuwa kwa umoja wao wanatambua bila kuwekeza kwa Wanawake ni ngumu kufikia Malengo ya Maaendeleo Endelevu 2030.

Mijadala iliyojadiliwa kutokana na dhima kuu ya mwaka huu imejikita kwenye maeneo yafuatayo, Uwekezaji wa miradi ya Wanawake na mashirika ya Wanawake, Masuala ya mabadiliko ya tabia ya Nchi, Maendeleo ya kidigtali, haki za kiuchumi
WOMENSDAY06.03.2024_145.JPG


Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom