Kwanini Wachungaji wengi siku hizi wanahubiri mafanikio ya pesa na sio wokovu wa roho?

Shalom wapendwa, nataka kujua kuhusu hawa Wachungaji wa michongo inakuwaje wajikite kuhubiri mafanikio ya pesa na mali na sio mafanikio ya kiroho.

Leo hii vijana wengi wamekimbilia kuanzisha makanisa huku wakijiita mitume, manabii, maaskofu nk lakini nimejaribu kusikiliza mafundisho yao yapo kinyume na ukweli wa kibiblia yaani hawajui kuichambua Biblia kama neno la Mungu lisilo na ubaguzi ktk kumhudumia muhitaji.

kuna baadhi ya makanisa haya ya Wachungaji wa michongo ni wabaguzi wakubwa wanaotenga hadi viti maalum kwa watu maalum (VIP)

Hapo tusemeje kuhusu Mungu maana Mungu sio wa kubagua bali huwahudumia wote wenye mali na wasio na mali.

Kwanini Wachungaji wa michongo huhubiri pesa zaidi kuliko mafanikio ya kiroho?

View attachment 2079225
Wewe ukiambiwa uuze Makoti msimu wa Joto hapa Dar utakubali?

Wanasoma upepo unavumaje na wao wanajikitia humo humo.
 
Agizo la kuhubiri injili kwa kila kiumbe ni la kila mwanafunzi wa Yesu. Kama wewe sio mwanafunzi wa Yesu halikuhusu, relax!
Hujajibu swali langu mkuu, ila kwa kuwa umelipotezea basi nimeshakujua wewe u miongoni mwa watumishi wa mihemko msio na wito bali ni wapigaji kama wapigaji wengine tu wenye kutapeli watu
 
Ukisema Mungu anaweza nipamoja na mafanikio .Tunaelezwa kufanikiwa ni haki yetu
Ni kweli, ila kuna kujaribiwa pia yaani unaweza kufanikiwa kiuchumi kwa muda fulani hivi, na inaweza tokea siku moja ukapoteza vyote ulivyonavyo ili kupimwa endapo unaamini mali au unamuamini Mungu.
 
Back
Top Bottom