Huliza
JF-Expert Member
- May 5, 2017
- 392
- 982
Ni utamaduni mpya kabisa wa mahubiri ya Utajiri, Mafanikio na uponyaji tu na Miujiza unaopingana na Imani ya Msalaba,
Eliona Kimaro na baadhi ya watu waliojipa utume na unabii wamelenga kwenye mahubiri ya uponyaji, utajiri, Miujiza na Mafanikio hivyo kuwaaminisha wafuasi wao kuwa njia ya Msalaba na msingi wa imani yetu ni kitu rahisi sana
Imani ya kikristo sio rahisi, Manabii na Mitume walipitia Mateso na shida,
1. Mtazame Ayubu maisha aliyoishi
2. Mtazame Stefano alipigwa mawe, 3.Mtazame Yohana alikatwa kichwa
4. Mtazame Masihi mwenyewe alisurubiwa
Imani ya kikristu inajengwa na Msalaba yaani njia ya Mateso, Njia ya kujitoa sadaka kwa ajili ya Wengine, Ni njia ya maumivu kuelekea ukombozi wa mwanadamu
Hutasikia hawa wachungaji wa kisasa wakienda hospitali ya Muhimbili, Mlongazila au Taasisi ya mifupa Moi kwenda kufanya miujiza na uponyaji wanayowadanganya wafuasi wao wakiwa kanisani
Kama kweli imani ya kikristu inajengwa na utajiri, Mafanikio, miujiza na uponyaji wachague siku moja waende pale Taasisi ya mifupa Moi au pale Muhimbili wakafanye miujiza watu wote wapate uponyaji na kutembea
Tangu enzi za kale manabii waliteuliwa na hawakujiteua wenyewe, Manabii walitumwa kwa kazi maalum na wala hawakujisifia wao
Yohana Mbatizaji au John the Baptist alifanya kazi kubwa ya kumuandalia masihi njia na alikuwa na wafuasi wengi sana lakini hata siku moja hakujisifu kuwa Yeye ndio Yeye mbele ya wafuasi wake, Alibatiza mamia kwa maelfu ya watu
Umaarufu wa Yohana mbatizaji haukumfanya ajione yupo juu ya watu wake na hata wanafunzi wake na wafuasi wake walipohamia kwa masihi hakukasirika
Yohana mbatizaji hata alipofuatwa Kuulizwa wewe Unafanya mambo makubwa hivi, Je wewe ni masihi au tumsubiri mwingine, Yohana mbatizaji alijibu kwa unyenyekevu na kujishusha kabisa kuwa Mimi sio yule, Aliye nyuma yangu ndio aliye mkuu kuliko mimi
Watu wanapoamua kubeba mabango ili mchungaji asiondolewe inafikirisha sana kwenye Misingi ya imani ya kikristo inayojengwa kwenye Msalaba yaani imani yetu tunapitia shida na Mateso kuelekea ukombozi na hata masihi alipitia njia hiyo hiyo ya shida na mateso
Kabla ya huyo mchungaji kulikuwepo watu wengi wamepita na kuondoka na hata Ukitaka abaki atazeeka na kustaafu ataiacha imani ya Msalaba
Wakristo hatuwezi kukwepa njia ya Msalaba, Njia ya Mateso, Kifo na ufufuo
Cha kushangaza na kuchekesha
Mtu anakurupuka alikotoka anajiita mimi ni Nabii alfa na Omega, Yaani Yeye ni nabii mwanzo na mwisho hakuna Wengine zaidi yake
Wakristo tuache kuwaamini wanadamu, Imani ya kikristu haijengwi kwa kupitia Mchungaji au Padri, Imani ya kikristo inajengwa kupitia msalaba
Padri na mchungaji ni njia tu ya kusaidia watu kuelekea ukombozi lakini wao wasitake kutengeneza Umaarufu nje ya Misingi ya imani ya Msalaba yaani shida, Mateso, Kifo na ufufuo