Ujumbe wa leo na siku zote za maisha yako ya duniani

totoadela

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
348
1,072
Heri ya mwaka mpya Wana Jf wenzangu!

Jinsi Ya Kuwa Mtu Mwenye Amani Moyoni. Njia mojawapo ya kujihakikishia unakuwa mtu mwenye amani moyoni ni kuwa mtu unayesamahe wanaokukosea.
Jonathan Lockwood aliwahi kusema...
...“Wasamehe wengine sio kwa sababu wanastahili bali kwa sababu wewe unastaili amani”Kuna watu wengi wanaishi katika vifungo vya uchungu na kutokusamehe.Wengine hata wameapa kabisa......“huyu sitamsamehe kamwe”.
Mara nyingi tunafikiri kutokusamehe huleta madhara kwa yule asiyesamehewa...
...lakini ukweli ni kuwa asiyesamehe ndiye anateseka zaidi.
Na wakati mwingine huweza kuleta magonjwa ya moyo kabisa.
Kusamehe SIO JAMBO RAHISI ila ni la MUHIMU sana katika maisha.
Kusamehe ni kuachilia mtu uliyemshikilia katika moyo wako.Ni kusema kuwa “Najua alifanya makusudi, hajali kama amenikosea, ameniletea maumivu na hasara ila nimeamua kumsamehe”.Mara utakapofanya hivi utashangaa amani ya moyo inaanza kurudi na milango ya baraka inaanza kufunguka.Kumbuka kwa kanuni ya kiroho ni kuwa “Msipowasamehe wengine makosa yenu, nanyi baba yenu wa mbinguni hatawasamehe”.
Hivi kama Mungu asipokusamehe makosa yako hadi yale umefanya sirini na hakuna mtu anajua, UTAWEZA KUFANIKIWA KWELI?
Usiwasamehe kwa sababu wanastahili, wasamehe kwa sababu wewe unastahili AMANI.
Inawezekana ni baba aliyekukataa, ni mwenza aliyekusaliti, ni rafiki aliyetumia kukujua kwako kukudhuru, ni mtu wa kazini aliyekusingizia na kukusababishia matatizo, ni mtoto wako n.k

SAMEHE.
MILANGO MIKUBWA YA MAFANIKIO unayoitafuta imefichwa kwenye UTAYARI WAKO wa kusamehe.
Anza leo, fanya sasa hivi, usisubiri muda upite.
Hata kama haujisikii, mwambie “Nimekusamehe”, tamka kwa sauti “Huyu (hapa unataja jina lake) nimemsamehe”
Wengine watakuona MDHAIFU ila wenye NGUVU tu ndio wana uwezo wa KUSAMEHE.

2024 UWE NI MWAKA MPYA WENYE BARAKA TELE KILA UNALOGUSA LIKAFANIKIWE
 
Kusamehe sio kwa kila mmoja. Wengine mpaka walipize kisasi ndio wanapata amani nafsini mwao.
 
Kawaida ya binadamu hata asamehe bado hata kubwa sawa ndani ya nafsi yake kwa sababu tunapenda kisasi, unaweza usimfanyie wewe kisasi ila akipata harassment yoyote walao moyoni utapata ahueni fulani.
Kawaida ama asili ya kila kiumbe ni kulipa kisasi.

Hata hivyo tunapaswa kusamehe, hata kama nafsi hairuhusu moja kwa moja ishurutishe.

Binafsi nina falsafa yangu ya samehe, sahau, nenda.

Heri ya mwaka mpya nawe mleta mada.
 
Back
Top Bottom