Kwanini Wachungaji wengi siku hizi wanahubiri mafanikio ya pesa na sio wokovu wa roho?

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
12,966
21,068
Shalom wapendwa, nataka kujua kuhusu hawa Wachungaji wa michongo inakuwaje wajikite kuhubiri mafanikio ya pesa na mali na sio mafanikio ya kiroho.

Leo hii vijana wengi wamekimbilia kuanzisha makanisa huku wakijiita mitume, manabii, maaskofu nk lakini nimejaribu kusikiliza mafundisho yao yapo kinyume na ukweli wa kibiblia yaani hawajui kuichambua Biblia kama neno la Mungu lisilo na ubaguzi ktk kumhudumia muhitaji.

kuna baadhi ya makanisa haya ya Wachungaji wa michongo ni wabaguzi wakubwa wanaotenga hadi viti maalum kwa watu maalum (VIP)

Hapo tusemeje kuhusu Mungu maana Mungu sio wa kubagua bali huwahudumia wote wenye mali na wasio na mali.

Kwanini Wachungaji wa michongo huhubiri pesa zaidi kuliko mafanikio ya kiroho?

Screenshot_20220113-100513.jpg
 
Ni kwa sababu moyo wao uko kwenye pesa. Kuna mama mmoja nilikuwa nimepanga naye ndani ya ukuta mmoja (wao - yeye na mumewe - wakiwa na nyumba na mimi na mke wangu nyumba ingine). Baadaye walifarakana, lakini waliendelea kuishi nyumba moja. Maisha yalipoanza kuwa magumu zaidi, huyo mama alitembelewa na ndugu au rafiki yake mwenye pesa na wakaanza mpango wa kuanzisha kanisa. Kama maandalizi walikuwa wakiwaalika watu kuja kuombewa kwenye hiyo nyumba yao, ila mumewe alikuwa akisema waziwazi kuwa "ni utapeli mtupu".

Hata mimi nilijua yule mama ni tapeli kwa sababu hakuwa na maadili ya dini hata kidogo. Ila walioweza kudanganywa naye walikuwa wakifika kwa ajili ya kuombewa! Mradi huu uliposhindikana, alijiunga na NGO fulani ambayo ilikuwa interested mashoga. Hivyo, kazi yake ilikuwa kuwakusanya vijana wenye mwelekeo huo na kuongea nao (sijui alikuwa akiwaambia nini), ila siku moja nilimsikia akimwambia rafiki yake naye afike kwenye mkutano wao aone mikakati yao, akidai ile NGO yao "ina hela chafu" kwa maana kwamba ziko njenje.

Wakati huo ndio tulikuwa kwenye mchakato wa maoni ya Katiba Mpya 2013 na hilo kundi lao nao walikuwa wakipigania haki za mashoga. Baada ya kuhama hapo tulipokuwa tukikaa (maana mwenye nyumba aliiuza) sijui alienda wapi na anafanya nini muda huu. Kwa hiyo, hawa watu wanaoweka pesa mbele ina maana wameanzisha kanisa kwa ajili hiyo na wanafaulu sana kuwadanganya watu wanaojiunga nao. Shame upon them!
 
Wanadanganya watu kwa kweli
 
Kwasababu dini ni utawala na utawala wa Kwanza unaanzia kwenye njaa ya akili yako!

Njaa ya akili zipo nyingi aidha ni ujinga ama ni matamanio yako, baadae inakupeleka katika utumwa.

Social engineering.
Hatari sana
 
wana hela za kula mkuu, kuwa na gari moja au tatu, na nyumba.. nazunguzmzia serious money.. alafu hata ukiwa na pesa standard pepo anatoka kimya kimyaaa bwanasheeee.. hatoki kwa mafujooo 😂😂😂
Halafu wenye hela wote wanapenda sana kula kitimoto, Yesu aliyaamuru mapepo yaingie kwa wale nguruwe wala hakujishughulisha kuyatoa kwa hao nguruwe, hivyo ukila kitimoto mapepo yanakuhusu.

Sikuelewi unaposema wenye hela hawanaga mapepo ilihali ni walaji wazuri sana wa kitimoto 😀😀
 
Shalom wapendwa, nataka kujua kuhusu hawa Wachungaji wa michongo inakuwaje wajikite kuhubiri mafanikio ya pesa na mali na sio mafanikio ya kiroho.

Leo hii vijana wengi wamekimbilia kuanzisha makanisa huku wakijiita mitume, manabii, maaskofu nk lakini nimejaribu kusikiliza mafundisho yao yapo kinyume na ukweli wa kibiblia yaani hawajui kuichambua Biblia kama neno la Mungu lisilo na ubaguzi ktk kumhudumia muhitaji.

kuna baadhi ya makanisa haya ya Wachungaji wa michongo ni wabaguzi wakubwa wanaotenga hadi viti maalum kwa watu maalum (VIP)

Hapo tusemeje kuhusu Mungu maana Mungu sio wa kubagua bali huwahudumia wote wenye mali na wasio na mali.

Kwanini Wachungaji wa michongo huhubiri pesa zaidi kuliko mafanikio ya kiroho?

View attachment 2079225
Huyu ni mchungaji??? labda wa mbuzi
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom