Kwanini Wabunge wetu wanakataa ziwa Tanganyika kufungwa kwa muda ila samaki wazaliane?

Ziwa Tanganyika lina wavuvi kutoka nchi za Zambia, DRC, Burundi na Tanzania. Uamuzi wa kuzuia wavuvi kuvua kwa muda fulani, unapaswa kuhusisha nchi zote tatu ili zoezi la kunenepesha samaki lifanikiwe.

Kutangaza kuzuia uvuvi upande wa Tanzania pekee wakati nchi washirika zikiendelea kuvua, haileti maana yoyote wakati samaki hawaijui mipaka ya nchi zetu.

Nadhani uvuvi uendelee ila iwe kwa kudhibiti idadi ya wavuvi kwa siku na kiasi cha kilo za kuvua kwa siku. Wavuvi wafanye shift, mfano wiki hii wavuvi kumi kilo kadhaa au ndoo ...hakuna kuvuka!. Zoezi liende hivyo kwa miedzi sita.
 
Burundi na Congo nako litafungiwa au watatusaidia kuvua na kutuuzia
Kimsingi ni makubaliano ya nchi wanachama wanaozunguka ziwa Tanganyika lakini pia najua wanawalenga zaidi wavuvi wakubwa wanaovua na kuuza samaki nje ya nchi Hawa wavuvi wa ndoano kando ya ziwa wataendlea japo chini ya uangalizi mkali
Na malalamiko mengi pia yametoka kwa hawahawa wavuvi kwamba gharama wanatumia kubwa na hawapati mavuno ya kutosha baadhi wakapendekeza ziwa lifungwe kwa mda
 
Nchi zote nne zimeshaazimia hayo.....

Tanzania ,DRC ,Zambia na Burundi zimeshakubaliana kuwa tumefikia hatua mbaya sana ya kuvua "FRY" samaki wachanga......hili litapelekea kubaya zaidi.....

Hao wabunge WAMESHACHELEWA....

Hao wabunge wanataka tufikie mahali tuache UVUVI kabisa na kuhamia katika KILIMO?!!!!!

Wabunge wetu wawe WAELEWA....
Wabunge wetu wasikilize ushauri huu wa kitaalamu na waache "MBANGO ZA HOVYO".....

#SiempreJMT
#SiempreSSH
#MamaKaja
 
Wabunge wajue KIKOSI KAZI cha nchi 4 kitaingia kazini mpaka mwezi 8 2023......

Vitaruhusiwa tu vyombo vya USAFIRI na si UVUVI...

Tanzania TUMEJIFUNZA yaliyotokea "NYUMBA YA MUNGU"......

#SiempreJMT
 
Ziwa Tanganyika lina wavuvi kutoka nchi za Zambia, DRC, Burundi na Tanzania. Uamuzi wa kuzuia wavuvi kuvua kwa muda fulani, unapaswa kuhusisha nchi zote tatu ili zoezi la kunenepesha samaki lifanikiwe.

Kutangaza kuzuia uvuvi upande wa Tanzania pekee wakati nchi washirika zikiendelea kuvua, haileti maana yoyote wakati samaki hawaijui mipaka ya nchi zetu.

Nadhani uvuvi uendelee ila iwe kwa kudhibiti idadi ya wavuvi kwa siku na kiasi cha kilo za kuvua kwa siku. Wavuvi wafanye shift, mfano wiki hii wavuvi kumi kilo kadhaa au ndoo ...hakuna kuvuka!. Zoezi liende hivyo kwa miedzi sita.
Ni uamuzi wa nchi zote 4.....mpaka mwezi wa 8......
 
Hilo la hao wakazi wa maeneo ya shughuli za kivuvi ndio kilio kikubwa kufungwa kwa Ziwa bila wao kuwa na mbadala wa shughuli za kuwaingizia kipato.

Serikali iwaandalie hao Watanzania wenzetu mbadala watakapofunga hilo Ziwa.
Mkuu hivi janga linapotokea huwa ni lazima kuwe na mbadala mathalani wa kutafuta vipato?!!!!

Hali ya ziwa TANGANYIKA ni ya kusikitisha sana.....imefikia pahala wavuvi wanavua pembezoni kwa kutumia ndoo....

Sasa unapowavua hao "fry-juvenile" ujue balaa la huko mbele ni kubwa zaidi ya kukaa MIEZI 3 BILA YA KUWA NA MBADALA WA RIZIKI UUSEMAO......

#SiempreJMT
 
Si kweli kwamba wananchi wanao ishi ziwa Tanganyika wanategemea kwa asilimia 100 uvuvi tu bali pia wanategemea zaidi kilimo za mazao ya biashara kama mihogo, maharagwe, mahindi, mpunga, na Karanga.

Pia ikumbukwe kuna wakati samaki wanakosekana kabisaaa na wananchi wanaendelea na biashara zingine, hivyo si kweli kwamba eti ziwa likifungwa kwa miezi 3 eti wananchi watakufa kwa umasikini
 
Ni uamuzi wa nchi zote 4.....mpaka mwezi wa 8......
Ok kama hivyo ni sawa, lakini utekelezaji wake ni mgumu, ukizingatia kuwa shughuli ya uvuvi kwa mvuvi ndio uhai wake, ukizuia wasivue lazima uwahakikishie kipato mbadala vinginevyo magendo yatajaza nafasi.
 
Usemayo yana tija....

Tulipofikia ni bora tu MAUMIVU ya miezi 3 kuliko janga litakalotutokea huko mbeleni......
 
Back
Top Bottom