UPDATE: Serikali yaahirisha kufungwa kwa Ziwa Tanganyika

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,611
Zikiwa zimebaki siku 10 kabla ya Tanzania kuanza kutekeleza makubaliano ya kusimamisha shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika kwa Miezi 3, Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali imesitisha zoezi hilo ili kuruhusu ushirikishwaji wa Wananchi na kupatikana kwa mipango mbadala

Makubaliano ya kusimamisha shughuli hizo yalifanyika katika kikao kilichofanyika Desemba 2021, kikihusisha nchi za Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zinazolizunguka Ziwa baada ya kupokea malalamiko ya wavuvi ya kupungua kwa mazao ya uvuvi kutokana na uvuvi haramu.

Nchi hizo zilikubaliana kufunga Ziwa hilo kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15, 2023 ili kuruhusu mazalia ya Samaki kwa wingi na kudhibiti uvuvi haramu, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi

...................................

Zikiwa zimebaki siku 11 kabla ya Tanzania kuanza kutekeleza makubaliano ya rasimu ya kusimamisha shughuli za uvuvi wa Ziwa Tanganyika kwa kipindi cha miezi mitatu, wavuvi, wasafirishaji wa mazao hayo na wabunge wamebaki njiapanda wakiomba Serikali itazame upya uamuzi huo.

Makubaliano ya kusimamisha shughuli hizo yalifanyika katika kikao kilichofanyika mwaka jana kikihusisha nchi zinazozunguka ziwa hilo ambazo ni Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Nchi hizo zilikubaliana kanuni moja ya kutambua zana haramu za uvuvi ili kuruhusu mazalia ya samaki kwa wingi na kudhibiti uvuvi haramu, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo, alipoulizwa jana kwa simu, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema leo atakuwa na mkutano na viongozi wa mikoa na wilaya husika, wakiwamo wabunge kujadili utekelezaji wa suala hilo.

“Tunakwenda kujadiliana namna ya utekelezaji au vinginevyo. Tutapata uelekeo kesho (leo),” alisema Ulega.

Kujengewa uwezo
Awali, katika kikao kingine cha kuwajengea uwezo maofisa wanaoshughulika na usimamizi wa rasilimali za uvuvi kwa nchi zote nne, kilichofanyika mjini Kigoma Februari 12, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya ziwa Tanganyika, Tusanga Sylvain alisema makubaliano ya kufunga ziwa hilo yalikuja mara baada ya kupokea malalamiko ya wavuvi ya kupungua kwa mazao ya uvuvi kutokana na uvuvi haramu.

Sylvain alisema nchi zote zimesaini makubaliano hayo na kwamba ikifika tarehe husika iliyokuwa imepangwa nchi hizo zitaweza kutekeleza na kuchukua hatua za kusitisha shughuli za uvuvi katika ziwa hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu.

Majibu ya Waziri Ulega
Kuhusu ziwa Tanganyika Ulega alisema “limesemwa kwa kirefu sana kuhusu Ziwa Tanganyika kufungwa na wabunge wa Kigoma, Rukwa, Katavi, wamesema kwa mapana na wananchi wamewasikia na sisi tumewasikia,” alisema Ulega.

Alisema wa suala hilo ulikuwa na lengo jema lakini haikulazimisha nchi wanachama namna ya kutekeleza itifaki kwa kufanana.

Chanzo: Mwananchi
 
Hii wiki bunge ni la moto kwelikweli, wabunge wameungana kuichachafya serikali. Kuna hawa wa kigoma kupinga kufungwa kwa muda ziwa tanganyika na wale wa tanga kupinga tanga cement isichukuliwe na twiga cement, mijadala ni mikali serikali iko taabani itabidi isalimu amri tu. Wabunge wa majimbo mengine wametulia kana kwamba maeneo yao hayana changamoto kwa wananchi wake
 
Back
Top Bottom