Mliomkejeli Hayati Magufuli, Ziwa Victoria lilifunguliwa, Samaki wametoweka

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Moja ya mambo ambayo Magufuli aliyoyasimamia ni pamoja na uvuvi haramu wa samaki katika Ziwa Victoria na Bahari ya Hindi. Jambo ambalo lilipelekea kufungwa kwa shughuli zote za uvuvi nchini kwa takriban miezi sita au zaidi.

Sote ni mashahidi kwamba zoezi lile lilileta mafanikio kwa samaki kuongezeka na hivyo kurudisha uhai katika sekta ya uvuvi nchini Tanzania. Ikiwa pia ni mchango mkubwa kwenye pato la taifa, kupitia kodi iliyopatkana kupitia usafirishaji wa minofu ya samaki kwenda nchi za nje.

Lakini zoezi hilo halikuwa rahisi, kwa sababu wale wafanyabiashara wa nyavu haramu pamoja na mawakala wao, waliwatumia baadhi ya wabunge na viongozi wa vyama pinzani, hususan CHADEMA. Ili kulipinga zoezi lile.

Wakimtuhumu Hayati Magufuli kwamba anawafilisi wavuvi na kuiua sekta ya uvuvi nchini. Hii ilipamba moto hasa pale aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakati huo, Luhaga Mpina, alipoamua kwa ujasiri, kuanzia pale Bungeni kuwapima samaki waliokuwa wanahudumiwa kwenye migahawa kadhaa pale Dodoma, ili kujiridhisha na ukubwa wao kama ni halali na kama wamepitia njia sahihi.

Sasa ni miaka takribani miwili imepita, tangu hayati Magufuli amefariki.

Nchi iko chini ya utawala wa Awamu ya sita, ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Alifungua nchi kama wanavyonadi "Chawa wa Mama".

Samaki Ziwa Victoria wako hatarini kutoweka! Yote hii ni kutokana na uvuvi holela na haramu kupitia nyavu haramu na Baruti, sababu kila kitu kilichofanywa na Magufuli kiliitwa 'Ubabe'.

Sasa nawataka wale waliokuwa wakipinga hatua za udhibiti wa nyavu haramu na uvuvi haramu pia.

Waje watuambie njia mbadala ya kutulisha samaki! Maana samaki wazazi ziwa victoria wamebaki kwa 4% pekee. Muda ni shahidi mzuri sana, maana huwa unaongea kwa vitendo.

Miaka miwili ya ziwa kufunguliwa holela, imepelekea madhara makubwa kwa wananchi mbali na kukosekana kwa kitoweo muhimu kwa afya za Watanzania.

Lakini pia ni pigo kubwa kwenye sekta ya samaki kuhusiana na kukosekana kwa kodi ambayo ingetokana na usafirushaji minofu ya samaki kwenda nje ya nchi.

"Uhuru bila Utii ni Wendawazimu," JK.Nyerere.
 
Moja ya mambo ambayo Magufuli aliyoyasimamia ni pamoja na uvuvi haramu wa samaki katika Ziwa Victoria na Bahari ya Hindi. Jambo ambalo lilipelekea kufungwa kwa shughuli zote za uvuvi nchini kwa takriban miezi sita au zaidi.

Sote ni mashahidi kwamba zoezi lile lilileta mafanikio kwa samaki kuongezeka na hivyo kurudisha uhai katika sekta ya uvuvi nchini Tanzania. Ikiwa pia ni mchango mkubwa kwenye pato la taifa, kupitia kodi iliyopatkana kupitia usafirishaji wa minofu ya samaki kwenda nchi za nje. Lakini zoezi hilo halikuwa rahisi, kwa sababu wale wafanyabiashara wa nyavu haramu pamoja na mawakala wao.

Waliwatumia baadhi ya wabunge na viongozi wa vyama pinzani, hususan Chadema. Ili kulipinga zoezi lile. Wakimtuhumu Marehemu Magufuli kwamba anawafilisi wavuvi na kuiua sekta ya uvuvi nchini. Hii ilipamba moto hasa pale aliyekuwa waziri wa mifugo na uvuvi wakati huo, Mheshimuwa Luhaga Mpina, alipoamua kwa ujasiri, kuanzia pale Bungeni kuwapima Samaki waliokuwa wanahudumiwa kwenye migahawa kadhaa pale Dodoma, ili kujiridhisha na ukubwa wao kama ni halali na kama wamepitia njia sahihi.

Sasa ni miaka takribani miwili tangu Marehemu Magufuli amefariki. Samaki ziwa victoria wako hatarini kutoweka! Yote hii ni kutokana na uvuvi holela na haramu kupitia nyavu haramu na Baruti, sababu kila kitu kilichofanywa na Magufuli kiliitwa 'Ubabe'.

Sasa nawataka wale waliokuwa wakipinga waje watuambie njia mbadala ya kutulisha samaki! Maana samaki wazazi ziwa victoria wamebaki kwa 4% pekee. Muda ni shahidi mzuri sana, maana huwa unaongea kwa vitendo. Miaka miwili.
We jamaa ilibaki kidogo ungekuwa india ungemuabudu huyo JPM kila siku nyumbani kwako.

Kwani samaki wanamfahamu JPM alikuwa raisi.
 
Sasa ni miaka takribani miwili tangu Marehemu Magufuli amefariki.
Samaki ziwa victoria wako hatarini kutoweka!

Yote hii ni kutokana na uvuvi holela na haramu kupitia nyavu haramu na Baruti.sababu kila kitu kilichofanywa na Magufuli kiliitwa "Ubabe"
Kichwa cha habari, kinakinzana na ulichoandika kwenye habari kamili.
 
Yaani yule mtu alikua ni version ya peke yake shida tu siasa zake ndio zilikua mtihani na ilibidi iwe hivyo maana sisi wabongo bila kupata mtu kama yule hatuendi!

Wanyama wenyewe wa porini waliongezeka sana ila sasahv mabucha ya nyama pori yapo mpaka uchochoroni kwa bei sawa na bure
 
Moja ya mambo ambayo Magufuli aliyoyasimamia ni pamoja na uvuvi haramu wa samaki katika Ziwa Victoria na Bahari ya Hindi. Jambo ambalo lilipelekea kufungwa kwa shughuli zote za uvuvi nchini kwa takriban miezi sita au zaidi.

Sote ni mashahidi kwamba zoezi lile lilileta mafanikio kwa samaki kuongezeka na hivyo kurudisha uhai katika sekta ya uvuvi nchini Tanzania. Ikiwa pia ni mchango mkubwa kwenye pato la taifa, kupitia kodi iliyopatkana kupitia usafirishaji wa minofu ya samaki kwenda nchi za nje. Lakini zoezi hilo halikuwa rahisi, kwa sababu wale wafanyabiashara wa nyavu haramu pamoja na mawakala wao.

Waliwatumia baadhi ya wabunge na viongozi wa vyama pinzani, hususan Chadema. Ili kulipinga zoezi lile. Wakimtuhumu Marehemu Magufuli kwamba anawafilisi wavuvi na kuiua sekta ya uvuvi nchini. Hii ilipamba moto hasa pale aliyekuwa waziri wa mifugo na uvuvi wakati huo, Mheshimuwa Luhaga Mpina, alipoamua kwa ujasiri, kuanzia pale Bungeni kuwapima Samaki waliokuwa wanahudumiwa kwenye migahawa kadhaa pale Dodoma, ili kujiridhisha na ukubwa wao kama ni halali na kama wamepitia njia sahihi.

Sasa ni miaka takribani miwili tangu Marehemu Magufuli amefariki. Samaki ziwa victoria wako hatarini kutoweka! Yote hii ni kutokana na uvuvi holela na haramu kupitia nyavu haramu na Baruti, sababu kila kitu kilichofanywa na Magufuli kiliitwa 'Ubabe'.

Sasa nawataka wale waliokuwa wakipinga waje watuambie njia mbadala ya kutulisha samaki! Maana samaki wazazi ziwa victoria wamebaki kwa 4% pekee. Muda ni shahidi mzuri sana, maana huwa unaongea kwa vitendo. Miaka miwili.
Sisi tunaendelea kula samaki pamoja na furu kila siku.
 
Inaweza kuchukua hata miaka 50 au 100 lakini kuna siku tutaelewa huyu mtu alikua ni zawadi kubwa sana kwa nchi. Hata tusipoelewa sisi watoto wetu na wajukuu zetu wataelewa

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
Jambo baya sana kufikiria kumpata mtu kama Magufuri kwenye nchi huru ni umaskini wa mawazo.
 
Back
Top Bottom