Kwanini Wabunge wetu wanakataa ziwa Tanganyika kufungwa kwa muda ila samaki wazaliane?

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,078
7,647
Sijawaelewa kabisa wabunge wa maeneo ya ziwa Tanganyika kupinga hoja ya waziri ya kulifunga ziwa kwa kipindi Cha miezi 3 ili kuruhusu samaki kuzaliana kwa wingi na kuingezeka.

Sisi wananchi tunakubaliana asilimia 100 na hoja ya waziri kwasababu tunauona samaki wanao vuliwa kwa sasa ni wadogo sana na wameadimika.

Mfano samaki aina ya Kuhe ambao zamani walikuwa wengi sana lakini kwa sasa kadiri siku zinavyo kwenda wanazidi kuadimika!!!

Samaki aina ya migebuka wanao patikana ni wadogowadogo!!!! Bei Iko juu.

Wabunge wetu acheni siasa kwenye mambo ya msingi kuweni wakeeli, Zingatieni masilahi ya wananchi sio kupinga tu kila kitu, hata sisi ambao sio wasomi tunaona kuna manufaa makubwa endapo ziwa litafungwa kwa muda kuliko Hali ilivyo sasa.

Sisi wananchi tunakubaliana na lengo la wizara kwa faida ya wavuvi, ni Bora tuvumilie kwa kipindi Cha miezi 3 ili tupate manufaa makubwa zaidi kuliko kubangaiza kama ilivyo sasa hakuna kitu.

Tunaiomba wizara iendelee na utaratibu ili kuinua uchumi wa wavuvi.

Wavuvi kutoka Pwani ya Kibirizi na katonga mkoani KIGOMA.


Wananchi washirikishwe Kikamilifu ili wajue faida ya zoezi hilo la kufunga ziwa.
 
Tatizo kubwa watu wamekuwa wanafiki sana, hata hofu ya Mungu hawana, hata mambo ya msingi wanapiga na kupotosha ukweli!

Unafiki mtupu!!!!

Tunawaomba wabunge wetu muwe mnatafakari kabla ya kuzungumza lkn pia mjue tunawaangalia live hivyo kuweni makini
 
Sijawaelewa kabisa wabunge wa maeneo ya ziwa Tanganyika kupinga hoja ya waziri ya kulifunga ziwa kwa kipindi Cha miezi 3 ili kuruhusu samaki kuzaliana kwa wingi na kuingezeka...
...Nyinyi 'Wananchi' mnaokubaliana na Hoja ya Waziri, Mko Wangapi ? Usije ukawa wewe peke Yako Nyuma ya Keyboard !
 
...Nyinyi 'Wananchi' mnaokubaliana na Hoja ya Waziri, Mko Wangapi ? Usije ukawa wewe peke Yako Nyuma ya Keyboard !
Wavuvi wote wa samaki kutoka Pwani ya kibirizi na katonga mkoani KIGOMA na katavi tunakubaliana na hoja ya waziri ya kufunga ziwa kwa muda wa miezi 3 ili samaki ziongezeke.
 
Hili suala ni gumu sana halihitaji mihemko ya kisiasa ukweli uliowazi samaki wameadimika sana na wanao vuliwa ni uharibifu.

Lakini najaribu kuwa watu wa maeneo ya Katete,Chongokatete,Isaba,Kazovu,Mvuna,Manda( kerenge na ulwile),Karangu,Kirando,Kipili,Namansi,Kabwe,Korogwe nk watakuwa na maisha ya aina gani ? Na je wizara imejipanga vipi ?
 
Sijawaelewa kabisa wabunge wa maeneo ya ziwa Tanganyika kupinga hoja ya waziri ya kulifunga ziwa kwa kipindi Cha miezi 3 ili kuruhusu samaki kuzaliana kwa wingi na kuingezeka...
Hawa wabunge hawafanyi siasa ila wanalinda biashara zao zinazohusiana na uvuvi.
 
Watu wanapambana kupata ubunge,tunadhani wanakwenda kutusemea kumbe wanakwenda kuatamia makampuni yao na ya washkaji zao.
 
Kule moshi bwawa la nyumba ya mungu lilifungwa kwa muda usiopungua miezi sita ili samaki wazaliane na wakue, ikawa shughuli pevu kwa wananchi wanaoendesha maisha kwa uvuvi wa pale, wengine walienda ziwa eyas, natron na manyara.

Samaki wa nyumba ya mungu ikabidi wavuliwe ki magendo na kuuzwa kama dawa za kulevya. Udhibiti ulikuwa mgumu, wavuvi walivua usiku usiku na kuendelea na mishe zao kama kawaida.

Huko ziwa tanganyika hawatafanikiwa kudhibiti ziwa lote samaki watavuliwa tu
 
Serikali inapaswa iwe makini sana, isibabaishwe na hoja za kinafiki, wizara inapaswa isimamie masilahi mapana ya wananchi na nchi.

Wananchi washirikishwe Kikamilifu ili wajue faida ya zoezi hilo la kufunga ziwa.
Unadhani wanajali wananchi hao
Hakuna kitu kama hicho
Hiyo wizara unayosema ndio vinara wa kupiga cha juu halafu unasema wamuangalie mwananchi
 
Wabunge wapo sahihi,watu wengi wanaoishi kuzunguka hili ziwa ni maskini ambao mahitaji yao ya kila siku wanayapata kwa kutegemea uvuvi kwa kiwango kiwango.

Ukifunga ziwa hili kwa miezi mitatu watu wengi wataishi maisha magumu sana na uhalifu utaongezeka.

Lakini pia ziwa hili linatumiwa na nchi ya Kongo na hatuwezi kuwazuia wavuvi wa Kongo wasivue samaki.

Kama serikali kama inataka kuongeza samaki ziwani basi wajenge mabwawa kuzunguka ziwa Tanganyika ambayo yatakuwa yanatumika kukuza vifaranga wa samaki na kuwaruhusu kuingia ziwani pale wanapokuwa wamekomaa tayari kuvuliwa.

Mpango huu unapaswa kushirikisha nchi zote mbili.
 
Huku mnafunga, kule Congo na Inchi zingine zinazopakana na Ziwa Wanavua, Samaki waliozaliana huku wanakimbilia Congo wanavuliwa , mnakuja kufungulia uvuvi samaki bado adimu kama ilivyo kuwa zamani , Natania Fungeni Muache kuvua mje muungane nasi wala Mchicha
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom