Kwanini vyombo vya habari vilimgeuka JK?

Mwanzoni vyombo vya habari vilimpamba sana hadi kuonekana kuramba miguu yake; lakini, ilipofika mwisho wa muhula wake wa kwanza inaonekana ni kama vyombo vya habari vimeonekana kugeuka kabisa.

Ni tatizo la vyombo vya habari, au ni tatizo la yeye mwenyewe au ni kitu gani kimefanya vyombo vya habari vigeuke namna hiyo? What went wrong?

MMJ!!

Wakumbuka winbo wa Mrisho Mpoto?? Ulikuwa ukimwambia Mjomba usikute watu wanakupigia makofi na kukushangilia ukadhani ndio wameridhika na ufanyayo au wanakubaliana na wewe, Usikute kumbe wanaku sanifu tu haoo mjombaa, akamwambia ukitaka kujua vyema uchukuwe mkanda wa hilo tukio na utazame upya uangalie ilikuwaje.

Sasa ndio hayo ya JK kwanza Campaign za kifamilia, kuwatenga wana CCM, na kuweka makundi, Kubeba wasiobebeka kwenye majukwaa, Sidhani kama kuna mwandishe anaeipenda nchi yake ateendelea ku msupport JK kwa yale yaliyotokea kabla ya Campaign wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi kwani walijua fiki ukweli ni upi na ndio maana JK havumi kama 5yrs iliyopita kabisaa na ndio CCM inafia mikononi mwake.

Na wasi wasi wangu mkubwa tusije kuta Serikali ya JK inaongoza na genge la watu walioko nje ya serikali yetu hii na ndio maana kunakuwa na kauri za ajabu na za kupisha kiti ya hawa viongozi wakubwa hapo hakuna cha Utawla bora na washeria kwani haiingi akilini kabisa kwa vitendo vinavyo endelea ndani ya nchi hiii.

 
Payuka umeiweka vizurikuliko mwanakijiji.
Yeye ameseme vyombo vya habari kana kwamba ni vyombo vyote vya habari wakati ni vichache tu. Ukiangalia kwa makini utagundua vyombo vinavyo muandika vibaya jk ni vile vipya ambavyo havikuwepo 2005,mfano Raia mwema haikuwepo.
Lakini vyombo vingi vya habari makini vilvyomsapoti 2005 bado vimeendelea kumsapoti hadi leo.Nitoe mfano tu,Rai,Daily News,Habari leo,Itv,Star tv,Channel 10,c2c,nipashe,the guardian,uhuru,to mention but few..

Kaka sikujua kama hivi ni vyombo vya habari makini. Mara zote nimejua ni vyombo makini kwa Habari za serikali.
Nimeshawishika nitaanza kununua gazeti la uhuru toleo lijalo.
 
katuni_1.jpg
 
Tatizo Jamaa yuko too Predictable..........
Hivyo vyombo vya habari vimekosa cha kuandika kuhusu yeye kwa maana hana mvuto kwa wasomaji wao tena....
 
Mwanzoni vyombo vya habari vilimpamba sana hadi kuonekana kuramba miguu yake; lakini, ilipofika mwisho wa muhula wake wa kwanza inaonekana ni kama vyombo vya habari vimeonekana kugeuka kabisa.

Ni tatizo la vyombo vya habari, au ni tatizo la yeye mwenyewe au ni kitu gani kimefanya vyombo vya habari vigeuke namna hiyo? What went wrong?

kuna chombo cha habari ambacho kili/kimemgeuka jk?
lini kwanza na kipi?

Unataka kusema jk hakubebwa na vyombo vya habari mwaka huu?
No way kama ni kuraba miguu yake nahisi kwa sasa ndio zaidi
 
Mwanzoni vyombo vya habari vilimpamba sana hadi kuonekana kuramba miguu yake; lakini, ilipofika mwisho wa muhula wake wa kwanza inaonekana ni kama vyombo vya habari vimeonekana kugeuka kabisa.

Ni tatizo la vyombo vya habari, au ni tatizo la yeye mwenyewe au ni kitu gani kimefanya vyombo vya habari vigeuke namna hiyo? What went wrong?
Habari Tanzania si Habari ni biashara na wakati wa uchaguzi biashara ilkiuwa nzuri upande wa pili. Kwa vile wale waliokusanya fedha kwa uchaguzi wameshamaliza msimu wao vyombo vya habari vitafuata bahasha za Ikulu huko kila siku kuna shughuli za vibahsha na ili ualikwe basi ionekane jitihada zako.
 
Isipokuwa UHURU, MZALENDO, HABARI LEO na DAILY NEWS, vyombo vingine vinaogopa kupoteza wasomaji maana vimegundua kwamba Watanzania hawataki utumwa wa mawazo, na HAWATAKI KABISA KUDANGANYWA
 
Kawaida yao kuwa maintain wote imekuwa kazi

Besides waandishi ni wale wale nao wanataka mshiko
 
Kikwete aliwahonga waandishi ile mara ya kwanza kwa njia mbalimbali, njia maarufu ambayo imekuwa ikisemwa ni ile ya kutoa ahadi ya vyeo kwa wahariri na senior JOURNALIST , na hii aliitumia sana mwaka 2005. kwakua alikua na marafiki wengi kuliko nafasi , akashindwa kutimiza matakwa na mahitaji ya kila aliemhahidi cheo.
wachache ambao walijitoa Muhanga ndio hao kina Salva Rweyemam wakalamba Vijinafasi.
Baada ya wakati kupita , waandishi wengine wakavunjika moyo, na kua walidanganywa, hawakuambiwa ukweli, walitumiwa kama Kondom, kisha mtumiaji baada ya kukidhi haja na hamu zake akatoweka na kuiacha katika sinki la choo.
kuja hii 2010, waandishi wengi wakamwambia hawadanganyiki, na hawa walikuwamo hata ndani ya gazati la Mzalendo, ndani ya Daily news, ndani kila chumba cha habari.
walijitahidi kudhibiti vyombo vya habari vya umma, lakini wakashindwa, walijitahidi kudhibiti vyombo vya makada, ITV, Radio one , the Gurdian na Vyombo vya Diallo , wakashindwa, kwa kua watendaji waling'amua Fitna na hujuma zao.
Waandishi wa Tanzania wananunulika, hawakumuacha Kikwete kwasababu za Kizalendo, walimuacha Kikwete kwasababu za Kimaslahi na sababu za kiibinafsi.
wajiangalie wanajidhalilisha sana, wanajiabisha sana.
 
walikuja kugundua kumbe ile picha iliyowekwa na zeUtamu ikimuonesha akiwa anashughulikiwa, ni kweli na haikuwa photoshoped
 
ila wapo wafuasi sugu ambao bado wanadhani JK atawakumbuka mkate wao wa kila siku , hawa ni pamoja na Ephraim Kibonde, Manyerere Jacton, ni baadhi tu ya Vilaza waodhani maisha huwa rahisi kwakubebwa na teuzi za Rais.
 
Mwanzoni vyombo vya habari vilimpamba sana hadi kuonekana kuramba miguu yake; lakini, ilipofika mwisho wa muhula wake wa kwanza inaonekana ni kama vyombo vya habari vimeonekana kugeuka kabisa.

Ni tatizo la vyombo vya habari, au ni tatizo la yeye mwenyewe au ni kitu gani kimefanya vyombo vya habari vigeuke namna hiyo? What went wrong?

Mi nadhani si kweli nafkiti vyombo hivi bado vinamwabudu huyu mtu kwani tumeona hilo wakati wa kampeni na hata sasa. Ni vyombo vichache vyenye mlengo tofauti na wa kwake ndiyo siku zote vimebaki kuwa sensible
 
Mzee mwanakijiji vyombo vya habari vingi viliendelea kumbeba Kikwete hata mwaka huu. Bahati mbaya watu hawadanganyiki.
 
Waandishi wa habari (baadhi) walidhani kwa kumpamba JK wangesogezwa Ikulu au wangepewa UDC, URC. Speculators hao. Si unajua trend ya baadhi yao kupewa nyadhifa ambazo ah.... malizia
 
Mwanzoni vyombo vya habari vilimpamba sana hadi kuonekana kuramba miguu yake; lakini, ilipofika mwisho wa muhula wake wa kwanza inaonekana ni kama vyombo vya habari vimeonekana kugeuka kabisa.

Ni tatizo la vyombo vya habari, au ni tatizo la yeye mwenyewe au ni kitu gani kimefanya vyombo vya habari vigeuke namna hiyo? What went wrong?

Kwa sababu Wakuu wa vyombo vya habari vingi au tunaweza kusema "Wikileaks za Tanzania", magazeti yetu mbali mbali kama vile THIS DAY, Mwanahalisi, Mwananchi, Majira, Raia Mwema na vyombo vingine vya habari viliandika mambo mengi ya ufisadi hasa katika awamu ya tatu na ya nne. Wakuu wa vyombo hivyo na Watanzania wengi tulitegemea kuona sheria ikiachwa kufuata mkondo wake katika ufisadi wote ulioanikwa hadharani ukiwemo wa EPA, Meremeta, Kagoda, Ununuzi wa Rada, Magari ya jeshi na helicopters, Ndege ya Rais, Mkataba wa Richmond/Dowans na ile ya kuchimba madini yetu, umiliki wa kifisadi wa KCM, lakini kwa mshangao wa wakuu hao wa vyombo vya habari kama ilivyo kwa Watanzania walio wengi wahusika wote hawakuguswa kabisa na mkono wa sheria. Usisahau pia vitisho mbali mbali vya waziwazi ikiwemo kufungiwa vilivyotolewa kwa baadhi ya vyombo hivyo vya habari ikiwemo magazeti ya Mwananchi na Mwanahalisi.

Nadhani utendaji finyu wa Kikwete katika maswala mbali mbali muhimu ndani ya nchi yetu yakiwemo yale ya kuhusu ufisadi yamechangia sana katika maamuzi ya wakuu wa vyombo vya habari vya kuachana na huyu aliyewahi kuitwa chaguo la Mungu.
 
Waandishi wa habari wa Tanzania ni kama malaya wa baa. Ukiwanunulia bia moja unakuwa "kaka" yake. Ukimuongezea nyingine moja unakuwa "shemeji" na ukiongeza ya tatu unakuwa "shemeji" within a span of 2 hours. Hawa nao walivuta fedha nyingi kutoka "mtandao" na huo "mtandao" ulikuwa unasifika kama ni "mtandao wa vijana" na damu mpya! Sasa mwaka huu CHADEMA wamevuta fedha nyingi kutoka Conservatives wa Uingereza na fedha hizi zimemwagwa kwa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari.

Kama vyombo vya habari "vilimramba miguu" Kikwete mwanzoni mwa muhula wake wa kwanza na tunakubali kuwa wamemgeuka mwaka huu, basi it is equally true walikuwa wanamramba miguu mgombea mwengine. Sasa jiulize kwanini hao waandishi wa habari wawe "wanaramba miguu" ya mgombea mmoja tu na kwanini wasiwe wanaripoti bila ya upendeleo wowote?

Kama unafikiri kuwa tuna waandishi na wahariri HONEST kwenye nchi basi hii Tanzania haujui kabisa!
Acha uwongo. Conservatives wa Uingereza hawakutoa fedha yoyote kwenye uchaguzi wa CHADEMA 2010.
 
Kikwete 2010 alikuwa ni bidhaa isiyouzika. Kumbuka alikuwa na Kikwete Press 2010 wakiwemo akina Michuzi. Kila alilolisema liliripotiwa, kila ahadi aliyotoa ilitangazwa kila tabasamu kuchapishwa. Lakini at the end of the day kama unanunua bidhaa based on matangazo ya kuvutia, unaichukua hiyo bidhaa nyumbani na kuitumia na kukuta it does not meet expectations, utarudi dukani kuinunua?
 
Back
Top Bottom