Sio kwamba wamengeuka bali ni nyakati zimebadilika.
1. Waandishi walitumiwa sana na wanamtandao kwa kununuliwa ili wampambe JK. Yakazuka magazeti kazi yao ilikuwa kuwamamliza wapinzani wake kisiasa ''Character assassination'', Salim A. ni muathirika namba moja.
2. Waandishi wetu wengi hawaandiki habari za uchunguzi ila wanaripoti nani kasema nini. Hii iliwanyima fursa ya kumjua JK mapema.Hali haionekani kubadilika. Waandishi wanaandika sensational news na sio investigative news.
3. Hata wale wachache wanaochambua habari, sasa wamechoka. JK anapowaambia watu Dowans haijulikani mmiliki, halafu PM anasema tutawalipa 'maruhani'', Werema anasema mjadala umefungwa, ni mwandishi gani atakayeweza kubeba mkanganyiko kama huu.
4. JK amewatumia waandishi kwa manufaa yake, linapokuja suala la Richmond mathalani, anaongea Katibu mkuu kiongozi au mwandishi wa rais. Hali hii inawaudhi sana waandishi wachache makini, na wamegundua wanatumiwa. Wamegundua pia usanii uliokithiri wa serikali kuwageuza watu wajinga ikiwa ni pamoja na kuunda tume zisizo na maana.(mfano, tume ya Luhanjo kuhusu Richmond)
5. Kama wanakijiji wanahoji utendaji dhaifu wa serikali hii , ni mwandishi gani atakayeandika habari ikanunuliwa kwa kupulizia perfume rundo la uozo!!