Kwanini vijana wengi wa mjini hupenda kuitana Wanyamwezi au kujiita Wanyamwezi?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,183
3,547
Kwanini hapa mjini vijana wengi hupenda kuitana 'Wanyamwezi'? Yaani hadi salamu unakuta wanaitana, mfano unakutana na mtu anakusalimia 'Inakuwaje Mnyamwezi, Au mambo vipi Mnyamwezi!'

Ukiwa umependeza unakuta unaambiwa 'Mnyamwezi umetokea sana'. Au mtu akiwa ametoka ulaya anaambiwa 'Unyamwezini'.

Hivi ni nini siri ya watu kupenda sana 'Unyamwezi' hapa mjini?
 
navyoona mimi.... hilo neno husimama badala ya mshikaji au rafiki na mara nyingi hutumiwa na vijana
 
Mi nadhani ilitoka kwenye wimbo wa temba "Amekoma" . alikua anamuongelea kijana mjanja Side Mnyamwezi..

So, wabongo tunavyopenda kukuza mambo, ikawa kila mjanja ni mnyamwezi.. Ukiwa ulaya ni unyamwezini
 
Kwa nini mnyamwezi na si mzaramo au mnyakyusa?

Sifa za Mmnyamwezi, in this context.

Mnyamwezi ni mtu wa miraba.

Mnyamwezi katapakaa kote tangu enzi za utumwa na vita vya Mirambo na Warugaruga.

Mnyamwezi kachukuliwa utumwa kupelekwa Zanzibar na Uarabuni sawa na Waafrika wa Magharibi walivyochukuliwa na kupelekwa Marekani, hivyo huchukuliwa pia kumaanisha "Mmarekani mweusi" au mtu mweusi aliyesafiri masafa marefu duniani.
 
Okey thank u....
 
Hivi ukienda ughaibuni hasa Marekani na mataifa ya ulaya watu wanasema umeenda unyamwezini. Ukiwa mtu wa huko ama unaishi huko unaitwa mnyamwezi, Je hii origin yake ni nin zaidi ilikuwaje ikawa watu wanaita hivyo
 
mkuu origin ya wanyamwez ni united states kitendo cha mtu especially black kwenda US ni kama anarudi kwao kutoka ugenini (exodus)
 
Wanyamwezi wanafafana maumbo na black Americans,wote warefu na miili mikubwa ndio chanzo cha hill jina.
 
mkuu origin ya wanyamwez ni united states kitendo cha mtu especially black kwenda US ni kama anarudi kwao kutoka ugenini (exodus)

Hawa wanyamwezi ninaowajua Mimi su kuna wanysmwezi wengine?
 
navyoona mimi.... hilo neno husimama badala ya mshikaji au rafiki na mara nyingi hutumiwa na vijana

sio kila mtu anaitwa mnyamwezi au uwe na swagga kama zangu,kama hauna swagga uwe umedondoka kutoka unyamwezini aka mamtoni
 
Jibu la swali lako ni hili:
Umesoma historia? Kama ndio unakumbuka kwamba kwenye biashara ya utumwa Tabora kulikuwa na nini? Jibu ni kwamba Tabora ndipo palipokuwa na kituo cha kusafirisha watumwa kutoka nchi za ukanda wa africa mashariki kwenda nchi za ulaya na marekani, hivyo basi kama mjuavyo wenyeji wa Tabora ni wanyamwezi, na ndio wengi waliokuwa wanachukuliwa kama watumwa na kupelekwa marekani na ulaya, kutokana na suala hili, ikaja kuonekana kwamba kwa miaka ya nyuma, watu weusi wengi walioloea nchi za Amerika na Ulaya, kwa wale wenye asili ya Tanzania utakuta ni wa kabila la kinyamwezi, na ndio chanzo cha vijana wa siku hizi kuitana wanyamwezi wakiwa wanamaanisha mmarekani mweusi.
 
Kwanini hapa mjini vijana wengi hupenda kuitana 'Wanyamwezi'? Yaani hadi salamu unakuta wanaitana, mfano unakutana na mtu anakusalimia 'Inakuwaje Mnyamwezi, Au mambo vipi Mnyamwezi!'

Ukiwa umependeza unakuta unaambiwa 'Mnyamwezi umetokea sana'. Au mtu akiwa ametoka ulaya anaambiwa 'Unyamwezini'.

Hivi ni nini siri ya watu kupenda sana 'Unyamwezi' hapa mjini?

Inakuwaje Mnyamwezini?
 
Back
Top Bottom