Sababu Vijana kuchelewa kufanikiwa kimaisha mjini

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Si Mara moja au mbili umesikia au kuagwa na rafiki yako akiondoka kwenda mjini kwa kisingizio cha kusaka maisha.
Pengine ni wewe mwenyewe upo mjini kusaka maisha ukitokea kijijini.
Lakini mpaka Sasa ni muda mrefu haujapata riziki yako "Kutoboa maisha" licha ya kujitahidi kwa kila namna lakini bado mambo ni magumu.
Umewahi kukaa chini ukajiuliza kwanini sifanikiwi, kama sio wewe basi umewahi kujiuliza kwanini wengine hawafanikiwi licha ya kupambana Sana mjini?

Japo sio wote ambao wametoka kijijini wana maisha magumu mjini, kuna vijana waliozaliwa mjini lakini bado nao hawatoboi maisha licha ya fursa kibao kuwazunguka.

Hizi hapa sababu kwanini vijana wengi hawafanikiwi mjini licha ya kupambana Sana.

Utafiti wa maisha ya vijana wengi mjini unaonyesha wengi wao wanapambania muonekano wao na sio maisha yao.
Iko hivi kijana akifika mjini na kuangalia maisha ya vijana Wenzake waliotangulia wanavyoishi anadata.

Utafiti wa kwanza unaonyesha wengi wao wakifika mjini huanza kushindana kupamba magheto yao kwa kununua vitu vya thamani kubwa ambavyo havilingani na hatua ya utafutaji waliyopo.
Kwa mfano kijana ana mtaji wa laki 2 wa kutembeza viatu kama machinga mtaani lakini ukienda ghetoni kwake kwenye nyumba ya kupanga unakuta kitanda cha 6x6 cha laki 4, TV nchi 40 ya laki 5.
Si hivyo tu bado Kuna vikorokoro kibao mara kioo cha ukutani, kabati la nguo la laki moja, na pazia la Elfu 30.
Ukipiga mahesabu thamani ya chumba chake cha kulala ni million kama 2 hivi ambazo ni mara 20 ya mtaji wake.

Utafiti wa pili unaonyesha vijana wengi hukumbana na gharama za kuishi ambazo hawakutarajia mfano ongezeko la Kodi, michango katika nyumba za kupanga kwa mfano unamkuta kijana analipia kodi ya kawaida ya chumba Elfu 40 mpaka 70, analipia umeme na maji elfu 10 kwa Mwezi, analipia hela ya usafi elfu 2 kwa Mwezi, na kila akiamka katiks siku 3 au mbili ndani ya wiki moja uongozi wa mtaa umefika unataka rambirambi mtu kafariki, kila msiba mmoja mia 5 au elfu 1, hapo bado michango ya mialiko ya harusi, bethidei, ubatizo na mingineyo.

Uhaba wa mitaji na elimu pia umebainishwa Kama kikwazo cha vijana kufikia malengo ya kimaisha mjini.
Mfano kijana amefika mjini na mtaji mdogo ambao kwa biashara aliyopanga kuifanya hautoshi ukijumlisha na maisha ya nyumba ya kupanga basi malengo hupotea kijana huanza kushughulika na tumbo lake na mahala pa kulala tu malengo huachana nayo.
Ukosefu wa elimu juu ya maisha ni tatizo lingine ambalo vijana huwatesa na wengi wao huishi kimazoea tu mpaka inapokaribia uzee ndio huanza kushtuka.

Familia kuweka matarajio yaliyopitiliza juu yake, hebu fikiria familia zetu za kiafrika kijana akiaga anaenda Dar es Salaam kutafuta maisha Ikipita miezi 3 tu utaona mzigo wa simu atakazo anza kupokea.

Ataanza kupokea simu hela ya mtoto kafukuzwa ada, hajakaa sawa atasikia baba kaanguka chooni hela ya matibabu inahitajika yani mpaka jasho jembamba linamtoka, ndio maana wengine huamua hata kufunga simu wasijue nini kinaendelea nyumbani ili mradi maisha ya utafutaji mjini yasonge.

Utafiti mwingine unaonyesha kuwa Vijana hukumbwa na jinamizi la starehe katika maisha ya utafutaji mjini hivyo kuingia gharama inayosababishwa na tamaa zao za starehe, kwa mfano kijana mwenye kipato cha chini kuudhuria tamasha la muziki lenye kiingilio cha elfu 50 usiku kwa mmoja.
Kuna ile tabia ya vijana kujitoa ufahamu kwenda kulala nyumba za Wageni na hoteli ambazo gharama zake ni za juu huku wakiwa wameacha magheto yao wamelala mende pesa inateketea.

Utafiti mwingine unaonyesha kuwa Vijana wengi hujipambanua katika kutafuta maisha mjini lakini kichwani mwao hawana malengo na mipango mkakati ya muda mfupi na mrefu, kwa mfano kijana kila siku anatafuta pesa lakini hana lengo maalumu la matumizi ya hizo pesa ndani ya mwaka husika au kwa kipindi kijacho Kama vile kununua uwanja, kumiliki ardhi ya kilimo au kununua vitega uchumi vingine ili kumkuza zaidi.
Kitendo hiki cha kukosa malengo hupelekea matumizi mabaya ya pesa, kisha kuchelewa kufanikiwa kimaisha.

Kukosa msaada, watu wa kusaidiana nao, utafiti pia umebaini vijana wengi hukosa msaada wa watu wa kusaidiana nao kwenye utafutaji "connection" mfano kijana ni mbunifu wa bidhaa lakini anashindwa kufika malengo ya kuuza hiyo bidhaa kwakuwa hana watu wa kumuongezea soko, kijana anatafuta kazi mjini lakini hawezi kupata pasipo watu kumsaidia ajue wapi pana uhitaji hili nalo ni tatizo.

Uwepo wa machangudoa na makundi rika haribifu, hoja hii itaonekana dhaifu lakini ina mashiko hasa ukizungumzia maisha ya vijana wa kiume mjini, kijana anatafuta pesa lakini anakutana na Wadada warembo kwa muonekano lakini mioyoni mwao ni wezi wa mafanikio ya vijana, huwaharibu vijana Kiuchumi na kisaikolojia.

Pia makundi rika hupelekea tabia mbaya kama uvutaji bangi, ubakaji na uovu mwingine ambao hufanya vijana kushindwa kutoboa kimaisha.
Sababu nyingine zilizo fanyiwa utafiti ni ulevi, uvivu na ukaidi wa vijana wanapoishi mjini.

Peter Mwaihola
 
Tunasingia utawazi lakini kwa kizazi cha leo vijana wengi wanwaza kupata pesa na kwenda club ckula maisha
Mwisho wa kufanya makosa ambayo ni obvious kiumri ni umri gani?

Pia kuna gharama za kuruka stages/steps

Kuna vijana at their early 20s, labda 21 mpaka 26 anakuwa keshamiliki kila kitu, na anapifikia 40 to 51 anakuwa keshapoteza kila kitu and vice versa.

Kuna mdau kasema dawa ni kuoa mapema, au kuruhusu hawa vijana waanze tu kuishi kinyumba hata kabla ya ndoa, miaka 22, 23 mpaka 27 wanaakili ya kuhimiliana vizuri tu, hapo kutakuwa na nidhamu flani hivi

Niko kwenye harakati za kutafuta bado na KUOA ni mpaka nikutane na binti ambaye angalau amemaliza kidato cha nne na hajawahi jiunga Facebook😉
 
Si Mara moja au mbili umesikia au kuagwa na rafiki yako akiondoka kwenda mjini kwa kisingizio cha kusaka maisha.
Pengine ni wewe mwenyewe upo mjini kusaka maisha ukitokea kijijini.
Lakini mpaka Sasa ni muda mrefu haujapata riziki yako "Kutoboa maisha" licha ya kujitahidi kwa kila namna lakini bado mambo ni magumu.
Umewahi kukaa chini ukajiuliza kwanini sifanikiwi, kama sio wewe basi umewahi kujiuliza kwanini wengine hawafanikiwi licha ya kupambana Sana mjini?

Japo sio wote ambao wametoka kijijini wana maisha magumu mjini, kuna vijana waliozaliwa mjini lakini bado nao hawatoboi maisha licha ya fursa kibao kuwazunguka.

Hizi hapa sababu kwanini vijana wengi hawafanikiwi mjini licha ya kupambana Sana.

Utafiti wa maisha ya vijana wengi mjini unaonyesha wengi wao wanapambania muonekano wao na sio maisha yao.
Iko hivi kijana akifika mjini na kuangalia maisha ya vijana Wenzake waliotangulia wanavyoishi anadata.

Utafiti wa kwanza unaonyesha wengi wao wakifika mjini huanza kushindana kupamba magheto yao kwa kununua vitu vya thamani kubwa ambavyo havilingani na hatua ya utafutaji waliyopo.
Kwa mfano kijana ana mtaji wa laki 2 wa kutembeza viatu kama machinga mtaani lakini ukienda ghetoni kwake kwenye nyumba ya kupanga unakuta kitanda cha 6x6 cha laki 4, TV nchi 40 ya laki 5.
Si hivyo tu bado Kuna vikorokoro kibao mara kioo cha ukutani, kabati la nguo la laki moja, na pazia la Elfu 30.
Ukipiga mahesabu thamani ya chumba chake cha kulala ni million kama 2 hivi ambazo ni mara 20 ya mtaji wake.

Utafiti wa pili unaonyesha vijana wengi hukumbana na gharama za kuishi ambazo hawakutarajia mfano ongezeko la Kodi, michango katika nyumba za kupanga kwa mfano unamkuta kijana analipia kodi ya kawaida ya chumba Elfu 40 mpaka 70, analipia umeme na maji elfu 10 kwa Mwezi, analipia hela ya usafi elfu 2 kwa Mwezi, na kila akiamka katiks siku 3 au mbili ndani ya wiki moja uongozi wa mtaa umefika unataka rambirambi mtu kafariki, kila msiba mmoja mia 5 au elfu 1, hapo bado michango ya mialiko ya harusi, bethidei, ubatizo na mingineyo.

Uhaba wa mitaji na elimu pia umebainishwa Kama kikwazo cha vijana kufikia malengo ya kimaisha mjini.
Mfano kijana amefika mjini na mtaji mdogo ambao kwa biashara aliyopanga kuifanya hautoshi ukijumlisha na maisha ya nyumba ya kupanga basi malengo hupotea kijana huanza kushughulika na tumbo lake na mahala pa kulala tu malengo huachana nayo.
Ukosefu wa elimu juu ya maisha ni tatizo lingine ambalo vijana huwatesa na wengi wao huishi kimazoea tu mpaka inapokaribia uzee ndio huanza kushtuka.

Familia kuweka matarajio yaliyopitiliza juu yake, hebu fikiria familia zetu za kiafrika kijana akiaga anaenda Dar es Salaam kutafuta maisha Ikipita miezi 3 tu utaona mzigo wa simu atakazo anza kupokea.

Ataanza kupokea simu hela ya mtoto kafukuzwa ada, hajakaa sawa atasikia baba kaanguka chooni hela ya matibabu inahitajika yani mpaka jasho jembamba linamtoka, ndio maana wengine huamua hata kufunga simu wasijue nini kinaendelea nyumbani ili mradi maisha ya utafutaji mjini yasonge.

Utafiti mwingine unaonyesha kuwa Vijana hukumbwa na jinamizi la starehe katika maisha ya utafutaji mjini hivyo kuingia gharama inayosababishwa na tamaa zao za starehe, kwa mfano kijana mwenye kipato cha chini kuudhuria tamasha la muziki lenye kiingilio cha elfu 50 usiku kwa mmoja.
Kuna ile tabia ya vijana kujitoa ufahamu kwenda kulala nyumba za Wageni na hoteli ambazo gharama zake ni za juu huku wakiwa wameacha magheto yao wamelala mende pesa inateketea.

Utafiti mwingine unaonyesha kuwa Vijana wengi hujipambanua katika kutafuta maisha mjini lakini kichwani mwao hawana malengo na mipango mkakati ya muda mfupi na mrefu, kwa mfano kijana kila siku anatafuta pesa lakini hana lengo maalumu la matumizi ya hizo pesa ndani ya mwaka husika au kwa kipindi kijacho Kama vile kununua uwanja, kumiliki ardhi ya kilimo au kununua vitega uchumi vingine ili kumkuza zaidi.
Kitendo hiki cha kukosa malengo hupelekea matumizi mabaya ya pesa, kisha kuchelewa kufanikiwa kimaisha.

Kukosa msaada, watu wa kusaidiana nao, utafiti pia umebaini vijana wengi hukosa msaada wa watu wa kusaidiana nao kwenye utafutaji "connection" mfano kijana ni mbunifu wa bidhaa lakini anashindwa kufika malengo ya kuuza hiyo bidhaa kwakuwa hana watu wa kumuongezea soko, kijana anatafuta kazi mjini lakini hawezi kupata pasipo watu kumsaidia ajue wapi pana uhitaji hili nalo ni tatizo.

Uwepo wa machangudoa na makundi rika haribifu, hoja hii itaonekana dhaifu lakini ina mashiko hasa ukizungumzia maisha ya vijana wa kiume mjini, kijana anatafuta pesa lakini anakutana na Wadada warembo kwa muonekano lakini mioyoni mwao ni wezi wa mafanikio ya vijana, huwaharibu vijana Kiuchumi na kisaikolojia.

Pia makundi rika hupelekea tabia mbaya kama uvutaji bangi, ubakaji na uovu mwingine ambao hufanya vijana kushindwa kutoboa kimaisha.
Sababu nyingine zilizo fanyiwa utafiti ni ulevi, uvivu na ukaidi wa vijana wanapoishi mjini.

Peter Mwaihola
you nailed !

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Huo utafiti namba mbili siyo sahihi kama ulivyoeleza!!

Hizo asset ndugu kuna kipindi vijana tunatumia kama dhamana kukopa kwenye NGOS zinazotoa mikopo siyo hiyo mikopo ya mabenki ya wenye hela tu. Sioni sababu ya kuwashangaa vijana wenye hizo assets. Binafsi na ushahidi na hili.

Kuna rafiki yangu alikopeshwa na alitumia furniture na TV, Fridge, Kabati , Jiko la Gas kubwa, Nk nk kama dhamana plus biashara aliyonayo. Binafsi nawashauri siyo kosa wala chanzo cha umaskini kuwa na hvyo vitu aise vinasaidia saana kwa kiasi hasa sisi Maskini.
 
Nchi yako ina kila rasilimali lakini bado ni masikini na inakopa kila siku.
Kununua vitu vya ndani ndiyo mwanzo wa mafanikio. Pia inakupa msukumo wa kutafuta hela.
 
wakifuta huu usemi "vijana taifa la kesho" kuna mtu alisema leo ndio hii kesho. hiyo ndio sababu ya kuwachelewesha huku mkibaki wazee
 
Back
Top Bottom