Huu uzi ni sehemu salama sana kukupa a, b, c kuhusu interview za psrps
Mimi ni mgonga ulimbo ambae sijakata tamaa kwa mara ya kwanza nilishiriki mchakato wa interview za psprs kwa kada yangu ya afya mwezi december nikaliwa kichwa kwenye written tu[emoji16]nilihisi kukata tamaa sema mtu wa maana sana humu Mwifwa katika baadhi ya post zake alisisitiza kutokata tamaa na tusiache kutuma maombi.
Nikatuma maombi kwenye post moja ya chuo cha serikali mjini dsm, Mungu si Athumani nikaitwa kwenye usahili zingatia wanataka mtu mmoja tukaitwa 317
Nikakumbuka tena bro Mwifwa husema hata kama nafasi moja kashiriki interview sikuwa nimesoma chochote nikashiriki na tukafika watu 127 tu kwenye usahili wa written
Nikafanya ila sikuwa na matumaini ya kuitwa oral bahati nzuri tukachaguliwa watu 12 kwa ajili ya oral ambayo naifanya soon.
I wish kupata a, b, c, d kuhusu oral interview za psprs maana hii ndio inaenda kuwa ya kwanza kwangu.
Natanguliza shukrani