Kuna utaratibu wa kuomba uhamisho kwenye utumishi wa umma. Huwezi kujipeleka huko kienyeji! Unaandika barua kwa katibu mkuu Utumishi, ukipitishia barua yako kwa mwajiri wako wa sasa. Hapa comments za mwajiri wako wa sasa ni za muhimu sana. Unaambatanisha barua yako ya placement mpya kuthibitisha kuwa nafasi tayari ipo na umeshaipata. Mwajiri wako mpya unampa nakala ili ajue kinachoendelea. Kama mwajiri wako wa sasa akisema hana kikwazo na anakuruhusu, bila shaka hiyo placement mpya utaipata. Lakini kama mwajiri wako wa sasa akisema anakuhitaji sana kwa sasa na asingependa uhame, uwezekano wa kuhama unakuwa ni mdogo (japo haufi kabisa). Nadhani uhamisho kutokana na double placement wanaweza kuruhusu kushughulikia, otherwise kwa kawaida uhamisho huwezi kuuomba kabla ya kuthibitishwa kazini.