Watu wamesota mtaani tangu 2011, tushauza juice za miwa sana, tushaendesha hadi boda, mwisho wa siku ni kukomaa na tunafanya vitu halali watoto waende chooni.
Kwa kada zetu nafasi huwa zinatoka kwa manati sana..vuta picha Unaweza kukaa miaka mingapi bila kuina nafasi ya afisa maendeleo.
Na hapo zikitoka tunachanganywa Kuanzia na wazee wa Sociology, kuna kozi sitakaa nimshauri mwanangu akasome, kozi zote za Maendeleo ya Jamii sishauri mtu.
Ngoja tusubiri placement za watu 800 tuone kama tutakuwepo.
Nakumbuka siku ya Oral hii ya juzi mwanangu alini wish all the best, kwakwel ilinitia hasira ya kutusua kinoma.
Inshallah Utumishi watutendee yaliyo mema kama wanavotenda.