Kuna mwamba yeye alikua wa MWISHO kila siku DARASANI, Tulipomaliza Shule ya msingi, yeye akaamua kutoendelea na SEKONDARI, Maana Baba yao alifariki sisi tukiwa form two, yeye akiwa STREET, alikua anauza duka la baba yake Kariakoo, baada ya Kugawana Hela za urithi, waja wakaanza ooh..huyu jamaa hajasoma Hela zote zitaisha Kwa kula BATA maana yeye ndo alikua mfano wa watoto wa HOVYO mtaani, yani akionekana Rafiki yako basi wote mnaonekana wa HOVYO, hivi ninavyoandika jamaa ana Nyumba Kali, Magari, Familia na Biashara zaidi ya MOJA hapa JIJINI DAR...Baada ya chuo maisha hayana formula, wapo wanaotoboa papo hapo after Uni na wapo wanaopitia mchakato wa kawaida wa kujipata ambao maximum ni 2-5 Years.
Hili kundi la pili, kwa kawaida kuna kipindi cha mpito huwa nakiita (Post-Uni Trauma) ambapo kwa sababu ya presha ya ndani na nje utatamani kila kazi halali na utaomba kila kazi iliyo mbele yako.
Funny part about this ni kwamba, 90% ya hizo kazi hutopata, na utazopata zitaishia kuku disappoint tu maana zote zitakua nje ya expectations zako sababu uliziomba out of desperation etc.
Utashuhudia wenzio/classmates wanaanzisha familia nzuri, wengine wanapata kazi nzuri, wengine utawapoteza mazima, wengine watakua madalali ili mradi kila mtu atapambania ugali wake.
Ukipanic sana unaeza amua kurudi home kwa kipa kuchek mambo yakoje huku unaskiizia ajira za Ajira Portal kama kitu pekee cha maana unachoskiizia ambazo hata ukiitwa interview utakupa posts ni 40 na watu mpo 10,000
Mtaani kwenu utakutana na wanao mlokua na kusoma nao O level, Primary washakua na mifumo yao ya kuishi na kimsingi katika context yao washatoboa.
Wale ulowaonaga miyeyusho kwa kuzaa mapema you'll find out wamekuza na watoto wao ni wakubwa na wazuri kweli kweli. Utakata tamaa, utaichukia elimu yako, utakosa vitu vingi BUT baadae utapiga mshindo mmoja na kila kitu kitabaki history.
One good thing about education is that, inaeza chelewa kukulipa ila siku ikikulipa ni inakulipa mazima mazima na utafanya kila kitu uliwahi tamani smoothly & in a decent manner.
Tuishi hapa. By nkololo
Wale watoto wazuri tuliioendelea na SHULE ndo tunaongoza kumpiga VIBOMU TAJIRI.
Na simu nyingi za BOSS nipo mitaa ya KARIAKOO vipi upo OFISINI....😅😅😅😅