HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Yaah well said! Kwa kuongezea pia inategemea na Taasisi ikoje, kwa mfano nimewahi shuhudia mtu anakataa promotion ya kwenda Wizarani abaki katika Taasisi yake! Nadhani aliusoma upepo
Wizara na halmashauri usipokuwa mkuu wa idara utaishia TGS I, kama 3.2M hii utafika baada ya kufanya kazi miaka 21.
Kuna baadhi ya taasisi kijana anaeanza kazi fresh anaanza na 2M. Hata Mimi ningekataa promotion
 

CHANGAMOTO NA MAISHA.​


Inabidi watu wajue tu kuwa, changamoto katika maisha huwa haziishi japo makali ya changamoto hutofautiana. Je wewe uko kwenye changamoto ipi?. Changamoto ni sehemu ya maisha ya kila mwanadamu. Usikatishwe tamaa na changamoto ulizo nazo, bali changamoto hizo zikusaidie kutafuta namna ya kukabiliana nazo!! Historia ya binadamu inaonesha kwamba maendeleo makubwa yaliyopo duniani leo, ni matokeo ya majibu ya changamoto ambazo mwanadamu alikabiliana nazo.

Yawezekana kuna watu wanaosaka asali kwa udi na uvumba leo hawatapata kabisa placement! Na watajiona kama watu wenye bahati mbaya sana, na pengine kuona kama vile walipoteza tu muda kusoma hadi chuo!! Lakini baadhi ya watu hao hao ambao watakubali jukumu lao la kupambana na changamoto zao zilizopo leo, miaka kumi hadi ishirini ijayo WATASHUKURU SANA kwa kutokupata placement!! Maana hiyo ilipelekea watoboe sehemu nyingine ambayo asali yake si ya kulamba tu, bali ya kunywa kwa kujimiminia, na kulambisha wengine(watakuwa waajiri)!! Wengine watakuwa wafanya biashara wakubwa, wengine watakuwa wakulima wakubwa, wengine watamiliki viwanda nk. Cha msingi usikate tamaa na ulikubali jukumu la kupambana na changamoto zako!!

Mungu ni mwenye haki, watakaolamba asali wamshukuru Mungu, na watakaokosa kwa sasa wamshukuru Mungu pia, maana kwa hakika watakuwa wameandaliwa yamkini mahali pazuri zaidi.


Lakini kitu kibaya zaidi ni kwamba yawezekana kuna watu pia ambao hawatapata asali wanayoisubiria kwa hamu, na mbaya zaidi ni kwamba, badala ya kukubali kupambana na changamoto zao, watabaki wakilaumu wengine tu. Hata kama hao wengine wanastahili kabisa kulaumiwa, lakini kulaumu pekee hakujawahi kuwa na mchango wowote katika kutatua changomoto zinazomkabili mtu!. Kijana wa kiume pambana, NINAKUAMINIA!!, kijana wa kike PAMBANA, acha kulia lia NINAKUAMINIA pia, wala usijishushe thamani. Amini kwa moyo wako wote kuwa KUTOBOA NI LAZIMA, NI SUALA LA MUDA TU!!​
NAWATAKIA MAFANIKIO WOTE.​
 
Haukumuuliza hili swali kwamba kwa nini wanatumia muda mrefu kutoa placement😂😂😤😤
Honest nilikuwa nime focus kwenye status maana wadau walitaka kuniua kwa presha umu

Ko akalicheki jina langu akaona liko fresh akasema subilia mkeka, kutokana na panelists walivyokujazia

Nikamdadavua kwa mbali kuhusu placement akasema inatokana na burget ya taasisi husika


Huyo jamaa yuko pisi Sana unaweza kumpigia akakupa majibu yote

Ila kuwa mvumilivu huwa anakuwa busy Sana na simu anapokea mara moja moja

Ni mtu safi Sana.
 
Honest nilikuwa nime focus kwenye status maana wadau walitaka kuniua kwa presha umu

Ko akalicheki jina langu akaona liko fresh akasema subilia mkeka, kutokana na panelists walivyokujazia

Nikamdadavua kwa mbali kuhusu placement akasema inatokana na burget ya taasisi husika


Huyo jamaa yuko pisi Sana unaweza kumpigia akakupa majibu yote

Ila kuwa mvumilivu huwa anakuwa busy Sana na simu anapokea mara moja moja

Ni mtu safi Sana.
Dah ayseee kumbe wana response nzuri ivyoo? inabid waulizwe swali la huu uzi????
 
Back
Top Bottom