Blender
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 6,839
- 10,954
Sasa vijana wanao fanya internship Katika taasisi na mashirika mbalimbali hutaki wapate priority, unataka waje wapewe wengine waje wafundishwe KAzi.Moja , Na wale mnaojijua hamjajitolea / kuwa na connections kwenye hizo taasisi mjiandae kisaikolojia ,ninyi hata kuwa shortlisted mtasikilizia kwenye bomba ,unajua Kenge huwa hasikii mpaka damu ivuje . Na kama mnavyojua huwezi kujitolea tu kiboya boya kwa mazingira haya ya kibongo unless wewe uwe ni kula kulala au una mtu wa kukupa back up financially .mfumo wa PSRS ulikuwa unampa graduates kufanya shughuli nyingine za kujiingizia kipato in the mean time anapambana na kusaka ajira , huo mfumo wa Taasisi watatoa priorities Kwa hao watu wao wa kujitolea na wenye connections zao ,
Na lingine ni kuwa hata hizo chances za kujitolea ni full connection na miaka saba hii ya ukame wa ajira mkae mkijua definitely kutakuwa na wimbi la watu wengi waliojishikiza hapo kwenye hizo taasisi kwa kigezo cha kujitolea ,so think about yourself na ujitathmini .
Watu wanawachora Tu mnavyojikakamua na kutuma hivyo vi CV uchwara vyenu , kuna kitu hamkijui ,subiri mpewe lessons kwa vitendo .
Pili , Huo mfumo wa kujitolea aka modern day enslavement ndio pia unachangia kiburi kwa taasisi kutoona umuhimu wa kuajiri ,kiufupi inafunga wigo wa ajira zaidi maana interns wanapiga mzigo kama manamba na taasisi nyingine haziooni umuhimu wa kuajiri sababu tu kuna mtu kacover upungufu na kufullfill duties na nafasi kiuhalisia zilizokuwa zinatakiwa zizibwe kwa ajira za kudumu ..
Guys use your time to think the reprecations of this ,msiangalie Tu pua zenu , hili suala la kushindwa kudeal na tatizo na kulikimbia ni chanzo cha matatizo mengi nchi hii , suala lilikuwa kuimprove efficiency ya mchakato hasa kasi ya utekelezaji wa majukumu hapo utumishi ,sasa kuna wahuni wamehijack hiyo agenda na kuweka interests zao ili kubypass restrictions za kubana udanganyifu na rushwa ili iwe rahisi kuweka watu wao kwenye hizo taasisi ,
Muwe mnafikiria Issues kwa umakini sana na kuangalia mambo kwa mapana yake .
Kiufupi labour market ya Tanzania sidhani kama ni rafiki tena kwa vijana kwa vurugu hizi.
Najua kuna watu ni vichwa maji ila soon mtaelewa tu na ninyi ndio mtaanza kutoa vilio humu kuhusu malalamiko ya mfumo wa ajira kwenye hizo taasisi ,mark hii comment
Mkuu hufai kuwa kiongozi, na wala hujui kuishi na watu hapa mjini