HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hao wengine wako jikoni wakati mwalimu yuko Dinning.
Nakupa mifano miwili :

1. Afisa hesabu wa Halmashauri anaesimamia Zahanati na hospital madokezo yote ya Hela na miradi mbali mbali lazima yapite kwake hapa lazima adake chochote akikusanya Zahanati zote sio haba

2. Procurement hawa ndio hawaendi mbinguni kabisa Kila mradi wa Halmashauri lazima wale. Hawa wanaenda sambamba na wahandisi. Mmoja anakagua utaalamu wa vifaa mwingine anakagua bei. Ukisikia Halmashauri imejenga soko Kwa milioni 800 basi ujue gharama halisi ni milioni 450-500, hizi nyingine mgao umetembea bila kumsahau pacha wao Afisa hesabu na mchumi.
Pia Hawa wa Halmashauri makao makuu wana OT wanajilipa.
Mwalimu Hana kitu chochote mkavu kama mkaa Hadi mwisho wa mwaka apate fursa ya mitihani
Vipi ma auditor wa halmashauri?
 
Habari, mimi ni mhitimu wa chuo fulani. Bado sijaanza kufanya mchakato wowote wa kutafuta ajira popote, natumai nitaanza siku za usoni. But huwa napata faraja sana napoona watu wanasema wamepata ajira japo siwajui wala hawanijui, huwa nawafurahia sana.
Karibu sana
 
Dahh ngoma nzito mpaka sasa mpaka unahisi kama umerogwa au una laana.

Nimepiga oral ya MDA LGA ila kila pdf inayotoka patupu ila wana wanapata na wameshaenda kuripoti kazini.

Nimepiga oral ya takukuru juzi tu hapa nayo matokeo patupu ila wana wamepata na wapo kozi sasa ccp moshi.

Naamini na mimi nitapata kazi hata kama sio leo ila nitapata tu kwa uwezo wa MUNGU.
Utapata usikate tamaa
 
Ety wadau
hivi vyeti ambavyo vinahitajika kwenye hii application lazima viwe certified mana hawajaainisha
Ndio ni lazima bila hivyo hautaitwa kwa usaili, na watakupa sababu kuwa vyeti havija kuwa certified. Hivyo toa kopi peleka kwa wakili au nenda mahakama iliyokaribu nawe
 
Habarini wataalamu
Kwa walioripoti kwa wa ajiri ( Halmashauri).

Naomba uzoefu wenu je tunatakiwa ku ripoti kuanza majukumu baada ya kupigiwa simu na mwajiri au baada ya kuisha tu zile ruhusa za siku 14, tunazoambiwa tuombe?
1. Serikali inafanya kazi kupitia maandishi rasmi. Ruhusa rasmi ni ile ambayo iko kwenye maandishi (barua yako ya ruhusa).

2. Ni kweli kuna mazoea ya "hadi tutakapokupigia (nitakapopigiwa) simu". Hii sio njia salama na ya kuaminika katika utumishi wa umma ya kuwasiliana ili mtu aende kuanza kazi.
Utaratibu huu unaweza kutumika vibaya na "watu wasio na nia mbaya" (wakakuingiza mkenge) na ikaja kukuacha katika mazingira ambayo huwezi kujitetea (kisheria).

NB:
Kama hauna suala ambalo ni la lazima sana la kukufanya usubiri "hadi upigiwe simu", nenda kaanze kazi siku ambayo barua yako ya ruhusa inakutaka ufanye hivyo.

Nakutakia tafakuri njema na utulivu mwanana.
 
Hapa ndipo unakuja ule msemo unaosema "ni nani amfunge paka kengele?". Umesema kweli kabisa kuwa ruhusa rasmi ni ile ambayo iko kwenye maandishi. Lakini nani atajicommit kumwandikia mwajiriwa mpya baada ya kuripoti kazini kwa barua rasmi, ya kumweleza kuwa arudi hadi atakapopigiwa simu? Ule utaratibu wa kumrudisha mtu aliyeripoti kazini bila kumpatia stahiki zake za posho ya kujikimu na nauli aliyotumia ni utaratibu unaovunja sheria. Kwa kuwa ni utaratibu unaovunja sheria hakuna mtu anayeweza kuuweka kwenye maandishi!!. Huyu mwajiriwa mpya pia baada ya kusota muda mrefu akitafuta ajira, si rahisi akamkomalia mwajiriwa wake on day one kuwa hawezi kuambiwa kwa mdomo hadi apewe barua. Matokeo yake anaamua kuwa mpole tu na kuona ni namna gani atapambana hadi atakapopigiwa simu. Wengine huwa wamejipanga vizuri wanarudi zao nyumbani hata kama ni mbali wakasubiri kuitwa kwa simu. Wengine huwa wamejiandaa vizuri wana pesa za kutosha kutafuta chumba na wakaanza maisha. Lakini wengine huwa hawawezi kabisa kurudi nyumbani maana nauli hana!! Utakuta hata nauli ya kuripoti alikopa, anaamua tu kuishi kwa muda kama watoto wa mitaani!! Mchana anazunguka kwenye saiti kutafuta kibarua na usiku anatua zake stendi kulala hadi kesho. Anashindia kwa mkate wa buku na juice ya watoto ile ya 500/=, maji ya ki-download!! Baada ya siku mbili tatu anarudi kuulizia tena kazini kwake na kuambiwa "si tulikuambia tutakupigia simu?". Ataishi hivyo hadi wengine zaidi ya mwezi japo wengi huitwa baada ya wiki mbili hivi. Hii changamoto kusema kweli si ya kitoto **** huna mfadhili wa kukusaidia. Ila angalau wanakuhesabu kuwa uko kazini japo bado unasota mitaani, ukisota mwezi mmoja unajikuta kwenye akaunti yako buyu la asali linatua/mshahara unaingia!!. Kuna wengine wamekula miezi miwili wakiwa mitaani!! Hapo tunashukuru japo ni utaratibu wa hovyo sana!!​
 
1. Serikali inafanya kazi kupitia maandishi rasmi. Ruhusa rasmi ni ile ambayo iko kwenye maandishi (barua yako ya ruhusa).

2. Ni kweli kuna mazoea ya "hadi tutakapokupigia (nitakapopigiwa) simu". Hii sio njia salama na ya kuaminika katika utumishi wa umma ya kuwasiliana ili mtu aende kuanza kazi.
Utaratibu huu unaweza kutumika vibaya na "watu wasio na nia mbaya" (wakakuingiza mkenge) na ikaja kukuacha katika mazingira ambayo huwezi kujitetea (kisheria).

NB:
Kama hauna suala ambalo ni la lazima sana la kukufanya usubiri "hadi upigiwe simu", nenda kaanze kazi siku ambayo barua yako ya ruhusa inakutaka ufanye hivyo.

Nakutakia tafakuri njema na utulivu mwanana.
Baada ya siku 14 kuisha,akienda halafu wakamwambia rudi subiri tukupigie simu?
 
Swali zuri....
Mtu huyu anatakiwa ku "take chances" na kufuata hayo maelekezo.

Lakini ni lazima afahamu kwamba hayo maelekezo, as far as hayapo katika maandishi, hayana uzito wala mashiko mbele ya miongozo, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Hivyo basi, waliomuelekeza wanaweza kumruka kimanga (kumkana) hapo mbeleni (in case of anything).

Hii ni sawa na mwanaume anayetembea na "mke wa mtu". Mke wa mtu akikuambia "njoo nyumbani, huyu bwege (mumewe) kasafiri "... unatakiwa kumuamini (maana yeye ndio anaishi na huyo mumewe), lakini unatakiwa ku "understand the consequences in case things turn."
Samahani kama mfano huu unaweza kuwa na ukakasi, sina lengo baya.

NB:- Kwenye jibu langu hapo juu nilieleza pia kwamba, kama hakuna jambo la "lazima sana" linalomfanya asubiri kupigiwa simu (baada ya zile siku 14 za ruhusa rasmi kuisha) basi aende tu kazini baada ya hizo siku 14.

Tutakupigia simu ni utaratibu wa kawaida (lakini sio wa kisheria) ambao hua unatumika hasa kwa hawa vijana wa ajira mpya. Hivyo basi, likitokea lolote lile, ni "sheria" ndio itakayotumika na sio "ukawaida".

Udumu Ulumbi.
 
Kwa mantiki hii siku 14 zikiisha mtu unazama ofisini unawambia nimekuja kikazi.
 
Halmashaur yangu wameniambia nijaze fomu ya ruhusa ya siku 14, kwa akili yng nilitarajia waniambie watanipigia simu kama wengi wao huambiwa.

Kwa namna nyingine namaanisha kupigiwa simu ni njia bora zaidi maana wakati huo mwajir atakua amejiandaa kukupokea ikiwepo tayari pesa ya kujikimu tofaut na wale wa kuanza kazi pasipo maandaliz ya kutosha.
 
Back
Top Bottom